Mtu wangu anapenda sana vazi la dera; akitoka ni dera tu na mara chache ni sketi au gauni.....anasema kanga au kitenge haviwezi kuvaa kwa maana hajavizoea na huwa vinampa shida sana anapovaa safarini ikiwemo kutomshika vizuri hali inayopelekea kutaka kumvuka hivyo kumkosesha utulivu.
Katika hisia zangu, ndani kabisa huko kwenye akili, silipendi vazi hili kwani mi huwa naona ni kama vazi fulani la kihuni hivi........wanaosasambua huko uswahilini nawaona wakipendelea sana madera; mashangingi nawaona wakipendelea sana madera (kama sikosei); n.k.
Maoni yenu wadau, maana isije ikawa ni 'ushamba' unanisumbua na hatimaye ukaniharibia mahusiano siku moja