wadau wa IT wa jamiiforums, Israel ipo kwenye level zipi kwenye masuala ya teknolojia za udukuzi na mambo ya cyber ?

wadau wa IT wa jamiiforums, Israel ipo kwenye level zipi kwenye masuala ya teknolojia za udukuzi na mambo ya cyber ?

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
download.jpg

Israel imekuwa ikidukua simu zinazotumia internet na minara ya simu kufuatilia mawasiliano na location.

Kikundi cha Hezbollah waliamua kukwepa tundu hili kwa kutumia pagers zinazotumia mawimbi ya redio pamoja na radiocalls kuwasiliana lakini bado Israel iliweza kudukua mawasiliano, kujua locations zao na ku trigger milipuko iliyojeruhi members wengi wa Hezbollah.

Tukitilia maanani udogo wa nchi na population yake, Israel wapo level gani kwenye haya mambo kidunia ?
 
Israel imekuwa ikidukua simu zinazotumia internet na minara ya simu kufuatilia mawasiliano na location za Hamas,

Hezbollaha waliamua kutumia pagers na radiocalls zinazotumia mawimbi ya radio lakini bado Israel iliweza kudukua mawasiliano, kujua locations zao na ku trigger milipuko.

Israel wapo vizuri kihivyo kwenye teknolojia ?
Hao jamaa wako too far now, in terms of cyber ni nothing but incredible. Wana kikosi maalum cha jeshi kwa ajili ya cyber warfare na wanao toka huko baada ya kutumikia jeshi huwa wakonin high demand duniani. Huajirika sekta binafsi. Wana value skills zao
 
Nilisikia wanajeshi baadhi yao wanamiliki makampuni ya IT kama software, antivirus, apps, n.k. kuna ukweli ?
 
Nilisikia wanajeshi baadhi yao wanamiliki makampuni ya IT kama software, antivirus, apps, n.k. kuna ukweli ?
Actualy hawaruhusu active military member kumiliki kampuni. Hao ni ex-military au wastaafu. Wanakuwa wameshatoka jeshini

Mfano mzuri ni NSO group, with famous product pegasus virus
 
View attachment 3100451

Israel imekuwa ikidukua simu zinazotumia internet na minara ya simu kufuatilia mawasiliano na location.

Kikundi cha Hezbollah waliamua kukwepa tundu hili kwa kutumia pagers zinazotumia mawimbi ya redio pamoja na radiocalls kuwasiliana lakini bado Israel iliweza kudukua mawasiliano, kujua locations zao na ku trigger milipuko iliyojeruhi members wengi wa Hezbollah.

Tukitilia maanani udogo wa nchi na population yake, Israel wapo level gani kwenye haya mambo kidunia ?
Mimi nadhanj kinachiwasaidia ni mwingiliano wa CIA ya marekan. Mfano sisi tunaotumia Google na android tuko Uch usa akiihutaji taarif zetu ni rahis san kuzipta
 
View attachment 3100451

Israel imekuwa ikidukua simu zinazotumia internet na minara ya simu kufuatilia mawasiliano na location.

Kikundi cha Hezbollah waliamua kukwepa tundu hili kwa kutumia pagers zinazotumia mawimbi ya redio pamoja na radiocalls kuwasiliana lakini bado Israel iliweza kudukua mawasiliano, kujua locations zao na ku trigger milipuko iliyojeruhi members wengi wa Hezbollah.

Tukitilia maanani udogo wa nchi na population yake, Israel wapo level gani kwenye haya mambo kidunia ?
Think out of the box, sio kwamba Mossad, ili hack simu zaidi ya 2000+, solar panel, pagers no, na kuzilipua, unawezaje kuvikia vifaa vyote hivyo kwa watu tofsuti, it's impractical,
Walichofanya Mossad, walipata taarifa za kijasusi kwamba, Hezbollah, inategemea kuagiza simu, pagers, nk,hapo ndio Mossad wakaingia kazini, wakatengeneza shell company, huko hungary, maofisa wa Hezbollah, bila kujua, wakaagiza mzigo, wakawa wanafsnya mazungumzo na hiyo kampuni, bila kujua ni front ya Mossad, mzigo ukatayalishwa, simu zikawekwa explosive material, mzigo ukaingia Lebanon, ukagaiwa kwa kila member wa Hezbollah, myahudi akasubili ahakikishe, kila kenge wa Hezbollah kapata ya kwake, then wanafsnya Yao, hii operation ni takribsn miezi 3
 
View attachment 3100451

Israel imekuwa ikidukua simu zinazotumia internet na minara ya simu kufuatilia mawasiliano na location.

Kikundi cha Hezbollah waliamua kukwepa tundu hili kwa kutumia pagers zinazotumia mawimbi ya redio pamoja na radiocalls kuwasiliana lakini bado Israel iliweza kudukua mawasiliano, kujua locations zao na ku trigger milipuko iliyojeruhi members wengi wa Hezbollah.

Tukitilia maanani udogo wa nchi na population yake, Israel wapo level gani kwenye haya mambo kidunia ?
wapo level za juu sana.
 
Hao wana front company nyingi za tech, kama ujuavyo tech ina players wengi wanaotegemeana hivyo ni rahisi kupenya kama tu Kuna watu wenye ujuzi waliowezeshwa na serikali inayojua inafanya Nini...kiukweli mambo hayo ya tech Kwa Israel yamefikia mbali Kwa maana ya kuanza wakiwa teenager around 20 na kuendelea, wana vijana wadogo wengi wanaolelewa na "mfumo"...hao ndo roho ya nchi.

Kuna wanafunzi wengi tu wa kiisrael wanakwenda western countries kusoma vyuo lakini tayari washakuwa wataalamu wa tech na basics mbalimbali kitambo sana, hivyo wakihitimu vyuoni hugombewa na kuanza kufanya kazi na makampuni mengi tu ya tech duniani hivyo ni faida Kwa Tel Aviv, wengine hurudi nyumbani kuendelea kufanya kazi, wengine wanawezeshwa na kuanza kufungua vikampuni vyao (startup co) sehemu mbalimbali duniani hasa Ulaya na nyumbani kwao Israel

Kuna makampuni makubwa ya wanajeshi, watu wa taasisi za usalama wa zamani wa Israel usije ukadhani ndo wamestaafu bali hapana kazi inaendelea kama kawaida, humo ndani wapo waisrael wengi tu ambao ni intelligence officers Kwa majina bandia na uraia wa kufoji wa nchi tofauti tofauti za ulaya (mashariki na magharibi), Kwa hatua hiyo basi si ajabu kukuta Kila kampuni kubwa duniani Kuna watu wa Tel Aviv tena nafasi nyeti then ndio wanategemewa na kampuni, hivyo ukichanganya na usaidizi kutoka Kwa baadhi ya mataifa inakuwa ni chemistry ya maana.

Hakuna kitu muhimu kama taarifa, tena zikiwa taarifa sahihi zilizokuja Kwa wakati sahihi, hivyo basi wao taarifa ndio kitu cha kwanza cha msingi na ndio maana wanasambaza watu wengi hasa Ulaya na arabuni, Nchi iliyozungukwa na maadui Kila pande kuishi Hadi Leo si Kwa kudra bali ni Kwa mambo kama hayo.

Vita middle east sio ya kuisha Leo, tutakufa tutaiacha, unaoitwa ustaarabu ulianza middle east na utafia middle east.
 
Huku Bongo tutafunga mkia...
Hakuna Progressive yoyote...mi ngoja mtoto wangu nimpelekee Japo Japo South
 
Hatari Sana Wapo Sijui Hatua Ipi Tuseme Tu Mbali Sana Sana
 
Haijatangazwa na haitatangazwa lkn ninauhakika 99% US ametuma vijana wa NSA kufanya kazi na Israel and hata Ukraine wapo wakutosha kussidia behind ya scene,kuna vijana wengi the best brighter toka hilo eneo wanatumika huko kufanya cyber attack ya vitu vyote vya electronic and anything inayotumia umeme,nina uhakika hata yale mauaji ya viongozi wa hezbulla jamaa wanatumia mifumo ya simu/gps tracer kujua hawa watu wapo wapi nakutuma drone kuwaua
 
Back
Top Bottom