TODAYS
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 14,747
- 24,250
Mkuu tupo pamoja, nakumbuka kuna vigogo wamefaidi sana huu mfumo, mfano mmoja tu; kuna mzee mmoja wa TANAPA anastaafu soon kiukweli ametengeneza maisha ya kizazi chake kutokana na mfumo huo, wao pesa walikuwa wanaiona na kuamaua wafanye nini ili kuitumia.Mkuu Cvez kwa NCAA na TANAPA naona anguko kubwa sana, hawa jamaa kwa miaka mingi fujo zao za pesa zimetokana na ukusanyaji wao wa pesa kupitia shughuli za utalii ukizingatia asilimia zaidi ya tisini utalii wa nchi hii unategemea wanyamapori basi iliwapa nguvu kubwa sana, hili la kucentralize ukusanyaji kwenda TRA then hazina utawanyima fursa nyingi za upikaji hawa jamaa, nadhani serikali iliona vurugu zile za pesa zilizofanywa na "machief", nawaza tu maisha baada ya hilo, kwa wazee wa game TAWA hili ni pigo jingine kubwa baada ya lile la kupokonywa maeneo yao muhimu ya upigaji pale Selous.
Mfumo wa decentralisation ulikuwa mzuri endapo waungwana wangekuwa wanaiba kwa heshima, tatizo wanaiba kwa "ndiyo ule mfumo alio..uongea mbunge Kishimba" so inaweza kuwa msaada endapo serikali kuu nayo baada ya makusanyo isiwe na roho ngumu kutoa fedha za maendeleo kwa sehemu husika ktk hizo.
Nawaangalia TAWA hawa nao hawavumi lakini wamo, kuanzia pale makao makuu Morogoro mpaka ofisi ya Arusha kuna kitengo kina urasimu sana kutoa vibali mpaka utumie ile slogan ya 'ongea tuongee.'