Wadau wa utalii mna mtazamo gani kuhusu uamuzi mpya ukusanyaji wa mapato yanayotokana na utalii?

Naam ndio hao hao wazee wa vikao vya dubai.

Yaani huo mpunga ukishaingia mikononi kwa Tra mara paap unakutana na miradi kibao ya bwn Jo' then kifuatacho Itv ni tanapa/ncaa wajiandae kisaikolojia.
 
hahah tena asali ya nyuki wadogo aina ya nyori itawafaa mkuu.
 

Mambo ni mengi sana mkuu kwa miaka mingi hizi taasisi zilikuwa ni kama zimemilikishwa kwa watu fulani fulani, hata uingiaji wa tanapa, na mamlaka wengi tunajua ni wa kujuana sanaa, kama mzee wako hayupo hifadhini au hana connection za huko utaishia kwenda kupiga paper pale Arusha kila mara lakini nafasi utazisikia kuziota tu, kijazi na Manong wana mazuri yao mengi ila kuna lawama nyingi hawawezi kuziepuka.
 
Umenena mkuu, hali itakuwa mbaya sana TANAPA, NCAA bora wenzao TFS na TAWA washazoea kupiga madili.
 
Hahaha halafu sijui kwa nini maconsaveta wote wa NCAA wanakuwaga viwembe au ni mfuko ndio huwa unaongea? Mabwana nyama sasa hivi hata bia hazishuki😁
Hahah hela automatically inaleta nguvu za kiume mkuu,halafu na wanawake ni wataalam wa sana kuna kunusa mahali hela ilipo.
 
Kweli kabisa mkuu mambo hayaishi kiukweli... Ila naamini kiongozi shupavu akiwepo kama ilivyo mh. John anapangua na kunyambulisha kila sehemu iliyoonekana kuoza inaleta afya kiasi flani.

Maana mfumo wa ujima wa kurithishana kazi haupo kwenye dunia hii au unabaki makanisani tu huko, kwenye ajira ni hapana.

Nakupa mfano huu hapa; TANAPA Wamekuwa na tabia ya kuwakusanya wahariri wa vyombo vya habari na kuwapeleka kwenye hoteli mojawapo nchini ili kuwapa elimu/mafunzo nk, kwa mwenye akili timamu unajua hakuna mafunzo hapo zaidi ya kushikwa mkono ili usiingie huko ndani.
 
Well said chief, ukweli mtupu.
 
Tunapunguza miria ya mapato yanayopotea kwa wizi tuna miradi inayohitaji sana pesa, optimal revenue collections
 
Fafanua kidogo hapa Mkuu..

Hizo taasisi ni vyanzo vikubwa vya mapato, sasa yawezekana wameona haja ya kusimamia na kuidhibiti ukusanyani, nahisi report zao za expenditure na pia matumizi ya miradi mikubwa ya kimkakati ni pasua kichwa, nadhani cash flow kwenye bajet imeonekana sio sustainable undulating cash flow graph imewasha taa
 
Hilo kweli lipo wazi ingawa wasiwasi ni kua hizi taasisi zikitegemea budget toka serikali kuu haya mapato yanayopatikana sasa hivi yanaweza yasipatikane unless wawe na mpango kazi maalumu kwa sekta utalii.
 
Hilo kweli lipo wazi ingawa wasiwasi ni kua hizi taasisi zikitegemea budget toka serikali kuu haya mapato yanayopatikana sasa hivi yanaweza yasipatikane unless wawe na mpango kazi maalumu kwa sekta utalii.

Itapendeza kama wizara ya fedha itahusika pia moja kwa moja na malezi ya karibu ya hifadhi za taifa, itakuwa muhimu sana. Ipo haja pia kudadisi zaidi nafikiri mijadala ya ndani kuhusu implications za mabadiliko hayo zilijadiliwa, mpango mpya wa usimamizi wa mapato na uendeshaji ni vema ukawa wazi kwa ajili ya angalizo kutoka wadau wa nje esp.gen.public
 
Hilo kweli lipo wazi ingawa wasiwasi ni kua hizi taasisi zikitegemea budget toka serikali kuu haya mapato yanayopatikana sasa hivi yanaweza yasipatikane unless wawe na mpango kazi maalumu kwa sekta utalii.
Hofu ni mabya sana. Kwani hao watu watawakataza wateja wasije hifadhini? maagent ndiyo wanawaleta watalii, mtalii asipokuja inamaana agent hataki ajira, flycatcher na tour company zitakosa wateja, organizer wa kuleta wateja ni tour operators na sio hizo taasisi kama unavyodhani. Hapa ni changa la macho tuu hakuna jipya, wacha tra wakusanye maana ndiyo wenye dhamana ya kukusanya kodi na maduhuli. Serikali imesema itawapa bajet waliyoomba wanaogopa nini, wasitishie nyau bhana
 
Ujangili haukuisha kwa sababu ya bajeti ya hao jamaa wa mambo ya hifadhi. Hao hawakuweza chochote kwenye ujangili na ndio walikua wanahifadhi ujangili.

John alipoingia aliamua kutumia kikosi kazi cha watu wenye roho mbaya nje ya hizo taasisi kupambana na majangili. Majangili wengi wamekufa, wamefungwa na wengine wamepotea hawajulikani walipo.

Wale majangili wa nyama wao huruma yao ni kupelekwa mahakamani na kufungwa miaka 20 ila wale wa ndovu, faru wao ilikua either kuzimu au ukimbie nchi.
 
Kwa sasa taasisi pekee zitakazoachwa zipokee mapato yao wenyewe ni taasisi za kibiashara na elimu tu. Hizi za huduma watapewa bajeti na serikali.
 
'Serikali imesema itawapa bajet waliyoomba wanaogopa nini'

Naona mzee baba umeamua kujisemea kirahisi rahisi tu,mpk sasa quarter ya mwisho inaisha kuna taasisi zimeishia kupewa 23% only ya approved budget zao.

Mfano mwingine:Tbc walitakiwa kupewa Tsh.5 bil kwa ajili ya kufanyia mambo yao ya kimaendeleo lkn mpk sasa wamepewa Tsh.0

Kuna maelfu ya mifano ya dizaini hio.
 
Miundo mbinu kama barabara TARURA wapo kila wialya, hotel zinajengwa na wawekezaji, nyumba vijana wa JKT wapo watajengewa. Doria ni kazi yao walioajiriwa nayo kama mkataba unavyosema, utalii wapo TTB watawatafutia wateja hapo wajipange labda kama wanampango wa kufoji hizo Billions of dola/TZS waseme tu. Mshahara watalipwa na serikali, ukiwa kama shuhuda wa bunge kuna mama mmoja alikuwa anasema wameshindwa kujilipa mshahra miezi miwili, sasa hapo serikali ilaumiwe nini? . Washukuru serilkali imesema itawalipa mishahara wampongeze JPM kwa uhamuzi huo
 
Issue si wageni kua wanaletwa na hifadhi. Ngoja nikupe elimu kidogo kuhusu utalii inacho itofautisha na sekta nyingine za uchumi utalii ni service industry meaning production na consumption vinatokea at the same time, basically you're selling experience. Now assume njia ya kutoka Ngorongoro to Serengeti imeharibika urequest funds toka serikali kuu kutatua tatizo ikichelewa kidogo tu hapo ushaharibu experience ya mgeni. Atachelewa kufika anapotaka on time, second mgeni analimited time kuwepo Tanzania hivyo akichelewa atamiss flight, au kama siku ikipita reservation ya mgeni isha expire na agents watakua na burden kurefunds, itinerary ya mgeni itafanyiwa mabadiliko, na kufanyiwa mabadiliko huko utafanya last minutes bookings which is expensive na huna uhakika wa kuipata. Hivyo kama unafanya biashara ya utalii kitu cha kwanza ni uweze kutoa exceptional customer experience na kuwezesha hilo uwe na sufficient cash flow unayoweza kuipata on time.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…