Katika nchi ambayo watu wanatekwa na kuuawa bila uchunguzi, wanapotokea mashujaa na kutangaza mgomo kwa lengo la kuchagiza madai yao ni lazima wapongezwe
Nachukua nafasi hii kuwapongeza Madereva ambao pamoja na hatari ya kutekwa na kuuawa lakini wamegoma. NCHI IMEFIKA PATAMU
UJUMBE: WENYE NCHI NI WANANCHI
Hata siongezi nenojamaa hawaelewi kabisa, test tu ya dereva kuendesha gari pale kwa mkoloni wetu U.K hata uchukue madereva nguli wa hapa nchini wengi wanaweza wasitoboe, maana checklist ya siku ya kutest dereva ili apate leseni ni ngumu kwelikweli kama dereva anachojua yeye ni kukanyaga mafuta tu.
hao si wazungu , tuchukulie wawe wametoka United Kingdom UK, nakupa homework nenda hata google, youtube kaangalie driving test zao tu, alafu uje hapa tujadili kama hao wazungu hapo hawawashangai hao madereva.
kule hata mtu akurekodi unaendesha hovyo akituma clip polisi adhabu unapewa. watu wanathamini sana leseni kwa kua inawapa matumaini wote waliopo barabarani ya kua salama
ndo maana umeshindwa kuelewa ile post ya kwanza inalenga nini, niliandika "nakupa homework" sikubahatisha.Kabla sija google naomba unisaidie kwanza wewe una hiyo leseni ya UK?
Unaongea nini bro? hapa nilipo nchi ya watu wanagoma maea kibao. Si kila taratibu inayowekwa na serikali inakubalika, even haPA Uk watu wanaandamana.Hao wazungu wanawashangaa sana na kuwaona wa hovyo. Maana sheria zilizopo kwao na hao wazungu zikitumika Tanzania hakuna gari itatembea barabarani. Hao Chadema waache kudandia hoja za watu, watawaharibia bure.
Kukwepa kwako swali kulionyesha wazi kuwa huna hiyo leseni ya UK na unajifunza mambo haya Google. Mimi nilikuuliza kwasababu nilitaka kuona kama una uzoefu halisi. Mimi sihitaji Google; nimeishi UK na kupitia huo mfumo hatua kwa hatua.ndo maana umeshindwa kuelewa ile post ya kwanza inalenga nini, niliandika "nakupa homework" sikubahatisha.
na wewe unaweza ukawa dereva au unasupport madereva ila hufahamu nchi kama UK vitu vingi tumeiga kwao
Mwanasheria tunae. We endelea na uchawi wako. Sisi tunapigania haki na maslahi yetu kwa vitendo. Pumbavu zako.We wapongeze tu, lakini pia viongozi wa madereva wakipelekwa kwa Ndunguru wanahamasisha/wanachochea madereva kuitisha the Executive, uwape wanasheria wa kuwatetea sasa.
Unapongeza mgomo? 😂😂Katika nchi ambayo watu wanatekwa na kuuawa bila uchunguzi, wanapotokea mashujaa na kutangaza mgomo kwa lengo la kuchagiza madai yao ni lazima wapongezwe
Nachukua nafasi hii kuwapongeza Madereva ambao pamoja na hatari ya kutekwa na kuuawa lakini wamegoma. NCHI IMEFIKA PATAMU
UJUMBE: WENYE NCHI NI WANANCHI
Hata wananchi wa kawaida kwa ujumla wote wakiamua kuigomea CCM inawezekana kabisa kuwatoa kwenye mizinga ya asali pamoja na kuwa wanamiliki dola, ni maamuzi tu ya pamoja.Katika nchi ambayo watu wanatekwa na kuuawa bila uchunguzi, wanapotokea mashujaa na kutangaza mgomo kwa lengo la kuchagiza madai yao ni lazima wapongezwe
Nachukua nafasi hii kuwapongeza Madereva ambao pamoja na hatari ya kutekwa na kuuawa lakini wamegoma. NCHI IMEFIKA PATAMU
UJUMBE: WENYE NCHI NI WANANCHI
Umeongea pointi kubwa sana Detective Jr, naunga mkono hoja yako 100%. Watu wanakariri mifumo ya wazungu kwenye Google bila kujua uhalisia wa maisha ya huko UK.Unaongea nini bro? hapa nilipo nchi ya watu wanagoma maea kibao. Si kila taratibu inayowekwa na serikali inakubalika, even haPA Uk watu wanaandamana.
Ni serikal kuja namna ya kutekeleza hilo suala
sasa kama wewe umekaa UK, itakua ni ajabu kushangaa hoja nazotoa.Kukwepa kwako swali kulionyesha wazi kuwa huna hiyo leseni ya UK na unajifunza mambo haya Google. Mimi nilikuuliza kwasababu nilitaka kuona kama una uzoefu halisi. Mimi sihitaji Google; nimeishi UK na kupitia huo mfumo hatua kwa hatua.
Nilipoenda UK, nilitumia leseni ya Tanzania kwa mwaka mmoja kabisa, nikapata Provisional License, nikafaulu Theory na Practical tests. Nakupa hadi mfano halisi: wakati natumia leseni ya Bongo, nilipata kesi ya trafiki ya kuendesha bila MOT (vipimo vya ubora wa gari). Nililimwa faini ya £200 na pointi 3. Nilikata rufaa mbele ya Mahakimu watatu; walipunguza faini lakini zile pointi 3 zilihamishiwa moja kwa moja kwenye Full License yangu nilipoipata.
Haya ndiyo mambo ya kiutendaji ya UK ambayo huyajui. Kule kuna miundombinu, uwazi, na mifumo ya kukata rufaa yenye haki. Sasa unaposema 'tumeiga kwao', ukweli ni kwamba Tanzania tumeiga adhabu lakini tukaacha mifumo ya haki na uwazi. Madereva huku hawagomi kwasababu hawataki sheria, wanagoma kwasababu mfumo wetu una mianya ya rushwa na hauna haki kama wa UK. Ndio maana hata hao wazungu hawawezi kushangaa mgomo, kwasababu kwao mgomo ni haki na chombo cha kupigania mfumo wa haki!
Safi sana, hatimaye umekubali kuwa hujawahi kukanyaga UK na unaishia kuangalia klipu za YouTube na makaratasi ya Google. Ndio maana unashindwa kutofautisha sheria zilizoandikwa na jinsi zinavyotekelezwa kwa haki barabarani.sasa kama wewe umekaa UK, itakua ni ajabu kushangaa hoja nazotoa.
mimi kutofika UK hakunifanyi nisifahamu utaratibu huko upoje wakati mamlaka zote husika wanaweka document zote mtandaoni, ukifika hapo youtube channel kibao za driving schools zinaelimisha kila siku mambo hayo.
sasa dereva anakwambia VTS iondolewe kwakua ni kamali kwasababu anashindwa kumaintan 80,dereva kama huyu hata wazungu wenyewe wakimsikia wataridhia aendeshe gari nchini kwao?
dereva anagoma kwakua sheria zinataka kua kali ili atekeleze wajibu wake? wazungu wasishangae jambo hili? punguza mizaha
Ni kweli kabisa, kwa UK watu wanatumia miaka mingi kupata leseni. Huo mtihani wa theory kufaulu tu ni kwa mbinde. Hapo bado hujaenda practical.jamaa hawaelewi kabisa, test tu ya dereva kuendesha gari pale kwa mkoloni wetu U.K hata uchukue madereva nguli wa hapa nchini wengi wanaweza wasitoboe, maana checklist ya siku ya kutest dereva ili apate leseni ni ngumu kwelikweli kama dereva anachojua yeye ni kukanyaga mafuta tu.
hao si wazungu , tuchukulie wawe wametoka United Kingdom UK, nakupa homework nenda hata google, youtube kaangalie driving test zao tu, alafu uje hapa tujadili kama hao wazungu hapo hawawashangai hao madereva.
kule hata mtu akurekodi unaendesha hovyo akituma clip polisi adhabu unapewa. watu wanathamini sana leseni kwa kua inawapa matumaini wote waliopo barabarani ya kua salama
usinichukulie poa kwa vitu nilivyovifatilia kisa sijafika hizo nchi. dunia imehama ipo kwenye teknolojia,Safi sana, hatimaye umekubali kuwa hujawahi kukanyaga UK na unaishia kuangalia klipu za YouTube na makaratasi ya Google. Ndio maana unashindwa kutofautisha sheria zilizoandikwa na jinsi zinavyotekelezwa kwa haki barabarani.
Kuhusu hoja yako ya VTS (Vehicle Tracking System) na hiyo spidi 80 unayodai ni 'kamari', hapo ndipo unapoonyesha usichokijua kuhusu UK:
Madereva wa Tanzania hawaandamani kwa sababu hawataki spidi 80; wanagoma kwa sababu mfumo wa VTS unalalamikiwa kuwa na makosa ya kiufundi yanayokata points za madereva hata pale wanapojaribu kukwepa dharura, bila uwepo wa mfumo wa uwazi wa kukata rufaa kama ule niliokwambia wa Mahakimu watatu wa UK.
- UK hakuna spidi ya kulazimisha ya 80 nchi nzima: Kule UK, mipaka ya kasi (Speed Limits) inabadilika kulingana na aina ya barabara—kuna barabara za makazi (20-30mph), barabara kuu za A-roads (60mph), na Motorways (70mph ambayo ni sawa na spidi 112 km/h). Serikali ya UK haikurupuki kuweka kifaa kinachomfunga dereva kwenye spidi moja ya 80 nchi nzima hata pale ambapo barabara inaruhusu kwenda kasi zaidi kwa usalama.
- VTS ya UK haitumiki kukata points bila ushahidi na haki: Kule UK, mifumo ya 'Telematics' au 'Black Box' inatumiwa zaidi na makampuni ya bima (Insurance) au makampuni binafsi kusimamia magari yao. Polisi wa UK hawatumii data za VTS kukata raia points kiholela bila uwepo wa Speed Camera iliyokaguliwa kisheria, au ushahidi usio na shaka ambao dereva ana haki ya kuuona na kuupinga mahakamani.
Ukiendelea kulumbana na mimi, nitakuletea mifano hai ya jinsi madereva na raia wa UK wanavyogomea na kuhujumu sheria wanazoona ni kandamizi. Nitakupa mifano ya jinsi walivyopinga vikali sheria ya ULEZ (Ultra Low Emission Zone) hivi karibuni, na jinsi walivyopambana na kukataza mifumo ya Speed Cameras miaka ya 90 hadi leo kwasababu tu waliona inatumika kama mradi wa serikali kujipatia pesa (cash cow) badala ya usalama. Wazungu wanajua fika kuwa sheria kandamizi au zisizo na haki zinapingwa, hawajifanyi 'ndio mzee' kama unavyodhani.
Kimsingi, unabishana na mtu aliyeshuhudia migomo hii kwa macho yake pasipo kuhitaji kuitafuta kwenye Google, kiongozi. Nimerudi Tanzania hivi sasa, na nina uhakika kabisa kuwa kama nisingeishi huko na kuona kwa vitendo jinsi haki, uwazi na miundombinu vinavyolindwa na kupiganiwa, huenda na mimi ningekuwa na mtazamo kama wako wa kukariri maandishi. Endelea kusoma YouTube, sisi tuliishi kule tunajua uhalisia!
Sijakataa kugoma ni haki ya msingi lakini soma hoja yangu na uielewe. Waambieni hao wanaharakati njaa wasijiingize kwenye hoja za watu watawaharibia. Wajifunze kuwa na mipaka na masuala ya watu wengine ambao hawajawaomba msaada wa kupush hoja zaoUnaongea nini bro? hapa nilipo nchi ya watu wanagoma maea kibao. Si kila taratibu inayowekwa na serikali inakubalika, even haPA Uk watu wanaandamana.
Ni serikal kuja namna ya kutekeleza hilo suala
Tatizo lako unasoma andiko bila kuelewa mwandishi kamaanisha nini. Soma vuzuri, unang'ang'ania hizo adhabu kwani hujaona nilpoaandika kuhusu mahakama zetu na mapolisi wetu na miundo mbinu? Unaleta jedwari bila kuzijibu hoja zangu?usinichukulie poa kwa vitu nilivyovifatilia kisa sijafika hizo nchi. dunia imehama ipo kwenye teknolojia,
kujua nini kinaendelea nchi fulani si lazima sana kufika kuna vyombo vya habari na kadhalika,
mfano mdogo tu mimi sijawahi kwenda bungeni dodoma, ila haimaanishi kwamba tukiongolea mwaka jana tuseme katika kufunga bunge nini kimeonglewa wakati website ya bunge inaweka hansard za vipindi vyote, achilia mbali hansard pia youtube channel ya bunge zote zinarushwa kule live na mpaka sasa bado zipo, hivyo hii hata mtu awe mongolia muda kama ana access za internet anaweza jadili muenendo wa bunge la tazania kwa sababu document kutoka chanzo halali zinapatikana.
kujumuisha mada yawezekana umeikurupukia na umeshindwa kuelewa hoja nayojenga.
wewe kwa kukaa kwako UK na kuendesha gari + kwenda kufanya test, test hapo UK si zile za kubook appointment na siku ya test mnaendesha kwa dakika 30-40 examiner anakua na checklisb yake, kama umepitia test ile
unaungaje mkono madereva hawa wanaogomea mfumo wa points
View attachment 3680444
hivi vitu hivyo vilivyopo kwenye jedwali nitajie kitu gani hapo UK kinaruhusiwa , yani sio kosa.
Je na Machawa wanaosifia kila sheria hata kama ni ya kijinga nao tuwaambie nini ni njaa ama?Sijakataa kugoma ni haki ya msingi lakini soma hoja yangu na uielewe. Waambieni hao wanaharakati njaa wasijiingize kwenye hoja za watu watawaharibia. Wajifunze kuwa na mipaka na masuala ya watu wengine ambao hawajawaomba msaada wa kupush hoja zao
Hapo ndo mnakosea na kuharibia watu wanaopambania masuala yao. Nyie kama mna hoja za kuwasaidia wapelekeeni siyo kuchukua suala lao na kuanza kulifanya kama la kwenu.Je na Machawa wanaosifia kila sheria hata kama ni ya kijinga nao tuwaambie nini ni njaa ama?