Isanga family
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 22,981
- 47,826
Upo sahihi Mkuu ila usitoe sana mifano na Ulaya kwa sababu wale jamaa bara bara zao nyingi zina bara bara ndogo ya waendesha baiskel,wanariadha au wanaofanya mazoezi naona tutolee mifano wa bara bara zetu chakavu na chache..naam watu wanabeza jambo hili kama kuikomoa serikali wakati barabarani ni mvurugano tu huko.
yani dereva anagoma kisa sheria kali zinakuja za kumtaka yeye afunge mkanda, au kuzingatia alama za barabarani
wakati huohuo kipanya akichora katuni kwamba tanzania kuvuka barabara kwenye zebra ni changamoto tunamuunga mkono kwamba kweli ni changamoto, sasa changamoto yenyewe si ndo madereva hawa.
jamaa wanataka kusema ulaya huko mvuka barabara anahangaika kama hapo dar
sawa mkuu hilo ntalizingatia, lakini mpaka sasa waziri wa mambo ya ndani mjadala wake wa madereva umeibua hoja mbalimbali naamini watafika muafaka kwa pande zote kukutana katiUpo sahihi Mkuu ila usitoe sana mifano na Ulaya kwa sababu wale jamaa bara bara zao nyingi zina bara bara ndogo ya waendesha baiskel,wanariadha au wanaofanya mazoezi naona tutolee mifano wa bara bara zetu chakavu na chache..
yupo aggressive sanaMwaipaya ni mpumbavu
Kuna wakati Mbowe akiwa Chair.yupo aggressive sana
Kanuni inasemaje? Kwani haki ya kusikilizwa kwa madereva haipo? Wakikatwa point hawaruhusiwinkwenda mahakamani kudai?Kwanza kabisa naomba unieleze ni madereva gani hao ninaowatetea unaodai wanavunja sheria? Hapa hatutetei uvunjifu wa sheria, bali tunatetea haki ya msingi na ya kikatiba ya madereva kufanya maandamano na migomo pindi wanapoona mifumo inakandamiza maslahi yao ya kazi. Hapo hata kama ulikuwa na pointi nzuri, unajikaanga na kupuyanga kwa kuchanganya kupigania haki na uvunjifu wa sheria.
Sipingi hata kidogo kuwa adhabu za UK zipo na ni kali; kule faini ya makosa ya utupaji hovyo wa taka (Littering au Fly-tipping) inaweza kufikia hadi £2,500 au £5,000 mahakamani, na gari lililotumika kutupa taka kiholela linaweza kutaifishwa na kupondwa na mamlaka za eneo husika (Local Authorities). Hilo liko wazi kabisa na silitetei uvunjifu wa sheria.
Hoja yangu tangu mwanzo haikuwa kutetea madereva wanaovunja sheria, bali ilikuwa ni kuonesha tofauti kubwa ya kiutendaji na mifumo ya haki (Due Process) iliyopo kati ya nchi hizo mbili:
Zaidi ya yote, tunapaswa kujiuliza swali la msingi la kiutawala na kiuwajibikaji: Katika mazingira ambayo viongozi na mawaziri wanabadilisha taratibu mara kwa mara bila tathmini ya kina (impact assessment) na bila kuchukuliwa hatua pale mifumo yao inapofeli, na huku kukiwa na malalamiko ya muda mrefu ya changamoto za kiadilifu na kimfumo ndani ya jeshi la polisi kutoka ngazi mbalimbali, huoni kwamba kuleta mfumo mkali wa kukata points kidijitali bila haki ya rufaa kutageuka kuwa mradi mwingine wa kujinufaisha badala ya chombo cha usalama barabarani?
- Haki ya kusikilizwa UK: Kule UK, wanapotumia kamera kukunasa, hupati adhabu hiyo ya juu kabisa ya £2,500 au kupondewa gari papo hapo barabarani kiholela. Unapewa notisi, na ukikataa kosa, unapewa haki ya kwenda mahakamani (Magistrates' Court) kujitetea na kuwasilisha ushahidi wako.
- Mazingira ya Tanzania: Hapa kwetu, madereva wanapogoma, hawagomi kwasababu wanataka kuvunja sheria au kwasababu wanapenda spidi 30 au 50 kwenye highway. Wanagoma kwasababu mfumo mpya wa kidijitali wa VTS unalalamikiwa kuwakata points moja kwa moja kwenye leseni zao kulingana na hizo spidi za konokono, bila kuwepo kwa mfumo wa uwazi wa dharura au mahakama huru ya rufaa ambapo dereva anaweza kujitetea kabla ya kufutiwa leseni yake.
Ndio maana nikasema, tunapochukua 'Adhabu za UK' tukazileta huku bila kuleta 'Mifumo ya Haki, Uwazi na Miundombinu' ya UK, tunatengeneza mazingira ya kuumiza watu badala ya kusimamia usalama. Sio kwamba ninatetea makosa; ninaeleza ukweli wa jinsi sheria inavyotakiwa kusimamiwa kwa haki pande zote mbili. Ni vizuri kwamba sote tunaona changamoto zilizopo, na hapo ndipo tunapokutana kwenye hoja.
Tanzania haithamini watu wake leseni ambayo wao waliikataa kunirudishia daraja E,E hiyo hiyo iliyo expire ndio nilifanyia test SA na kupewa code 14 ambayo naendesha truck wao wapo busy nikasome wiki mbili huku unapewa vitabu nenda kwenye test uki fail unarudia mara mbili ukishindwa basi tena sasa sisi wakongwe ni moja tu unapata wao wanakuona sio dereva ili watusumbue tu..sawa mkuu hilo ntalizingatia, lakini mpaka sasa waziri wa mambo ya ndani mjadala wake wa madereva umeibua hoja mbalimbali naamini watafika muafaka kwa pande zote kukutana kati
Sawa mwenye akili. Kama unazo na unajiamini una akili huna haja ya kuambia wengine akili finyu. Itakuwa huna hizo akili ndo maana unajishtukiaakili finyu ungekua smart ungegundua kwanini nimeandika hivi
Kwa aina ya barabarani zetu polisi wakiamua kufuata sheria wengi watapaki magari. Madereva wawe wapole na wajadiliane au wangeomba majadiliano na wahusika. Na wenzao wanaanza kuwaharibia eti wanamtaka Rais au Waziri Mkuu. Waambiane waache kutafuta umaarufu utawaponza baadhi yao, nchi zetu za afrika tunajuana.+ rushwa
Wadau humu wanangangania point point
Wakati kuna changamoto nyingi pande zote mbili
Ova
Juzi kati kuna dereva alikuwa anang'ang'anizwa aingizwe kwenye gari la watekaji wakatoka wakadai ni bastola bandia ......na kesi haieleweki imeishia wapi kwa ufupi madereva wana haki ya msingi kugoma maana kama ni rushwa wanatoa ila bado faini zinaongezeka saizi hadi wameziwekea pointi sasa watafuta leseni ngapi?Katika nchi ambayo watu wanatekwa na kuuawa bila uchunguzi, wanapotokea mashujaa na kutangaza mgomo kwa lengo la kuchagiza madai yao ni lazima wapongezwe
Nachukua nafasi hii kuwapongeza Madereva ambao pamoja na hatari ya kutekwa na kuuawa lakini wamegoma. NCHI IMEFIKA PATAMU
UJUMBE: WENYE NCHI NI WANANCHI
Isivyo bahati kwa policcm ilikuwa jumba hili bovu wamuangushie Lissu kuwa hotuba yake iliwachochea madereva.Katika nchi ambayo watu wanatekwa na kuuawa bila uchunguzi, wanapotokea mashujaa na kutangaza mgomo kwa lengo la kuchagiza madai yao ni lazima wapongezwe
Nachukua nafasi hii kuwapongeza Madereva ambao pamoja na hatari ya kutekwa na kuuawa lakini wamegoma. NCHI IMEFIKA PATAMU
UJUMBE: WENYE NCHI NI WANANCHI
Unaweza kufuta ajali zisitokee kwa sheria kali tuu?Kumekuwa na makosa ya kizembe sana na mengine ya kujurudiarudia, haya ndiyo yanafanya adhabu hizi ziwe kali mpaka kufikia kulalamika. Kama wangekuwa wanafuata sheria vizuri, basi hizi adhabu zisingefikia huku.
Watu wengi wamepoteza ndugu zao, wengine wanahudumia walemavu, kisa ajali za kizembe, ndiyo maana sheria ikaongezwa kuwa kali.
Hata huu mwendo mwisho 80 km/h haukuwa wa kisheria kabla, ila ajali za kizembe zilipozidi wakaamua kupunguza na kuweka ukomo.
Yaani hizo kukatwa point pia imeletwa kutokana na uzembe wao wenyewe, lau kama wangekuwa na weledi na kufuata sheria yasingekuwepo hayo.
Huku naona ni kudeka na kama wakidekezwa watakuja kufikia pabaya hawa, wafuate sheria bila kulalamika.
Yaani hayo makosa yao mengine ingekuwa nchi za Ulaya wangekuwa jela wengi sana, wengine wangefutiwa leseni zao kabisa. Kule hakuna kubebana wala kuoneana huruma au kutoa kitu kidogo. Kosa dogo tu unajikuta jela. Hapa wanawalea vibaya hao.
Kama wanajua mengine itaathiri majukumu yao kwa familia watulize wenge njiani basi, wajue wamebeba roho za watu.
mawazo kama hayo ndo yanahitajika kupewa hizi mamlaka zetu,Tanzania haithamini watu wake leseni ambayo wao waliikataa kunirudishia daraja E,E hiyo hiyo iliyo expire ndio nilifanyia test SA na kupewa code 14 ambayo naendesha truck wao wapo busy nikasome wiki mbili huku unapewa vitabu nenda kwenye test uki fail unarudia mara mbili ukishindwa basi tena sasa sisi wakongwe ni moja tu unapata wao wanakuona sio dereva ili watusumbue tu..
Si zilihakikiwa?Unaweza kufuta ajali zisitokee kwa sheria kali tuu?
Hivi unajua nani anawapa leseni wasiostahili kwa rushwa tuu?
Huna ubongo?Unapongeza mgomo? 😂😂
So wanagomea nini kwani?
Vibaka kaziniMbezi Louis
Dar es Salaam
29 September 2026
Polisi wang'oa namba za magari, madereva waliogoma kuondoa mabasi Stendi Magufuli
View: https://m.youtube.com/watch?v=WbBE42a9T60
Kwani naye ni dereva?yupo aggressive sana