Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 10,509
- 16,734
Viongozi na wanajamii wa Druze huko kusini ya Damascus wameweka wazi kuwa wao wapo pamoja na serikali mpya Syria katika kujenga Syria mpya.
Siku chache zilizopita kulisambaa ujumbe wa sauti maeneo ya Ashrafieh Sahnaya ukihusishwa na kiongozi wa jamii ya Druze kumtukana mtume Muhammad saw.Jambo hilo lilipelekea kutokea mabishano kati ya waislamu wa madhehebu ya sunni na jamii hiyo na kupelekea mapigano.
Vikosi vya jeshi la nchi hiyo vilipeleka askari wake kutuliza ghasia ambapo wakati huo huo jeshi la Israel lilishambulia eneo hilo na kusababisha vifo vya askari 10 pamja na watu wengine 6 waliokuwa na silaha.Baada ya tukio hilo jeshi la Israel likaahidi kuendeleza mashambulio iwapo jamii ya Druze itaendelea kuonewa.
Kinyume na madai ya Israel,kiongozi wa jamii ya Druze amesema hana taarifa na rekodi hiyo na akashutumu kuwa imetengenezwa ili kuchochiea machafuko ndani ya Syria.Kiongozi huyo akazidi kusema kuwa jamii yake haitaki misaada ya kichonganishi kutoka Israel na kwamba wao wako pamoja na uongozi wa serikali mpya ya Syria.
Kamanda wa vikosi vya serikali anayehusika na usalama wa eneo hilo amesema nchi yake inalaani mashambulio ya mara kwa mara ya Israel kwa visingizio mbali mbali na kwamba usalama wa wadruze na wananchi wa Syria ni jukumu lao wanalolifanya bila upendeleo.