Wadudu wa Arusha ni uchafu wa kijamii, sio sifa njema kwa Arusha. Ududu upigwe vita!

Pale Ugunja mji upo sehemu gani au soko la darajani?
Namaanisha mjini magharibi, ndio mkoa katika Zanzibar wenye kubeba kitovu cha Zanzibar yote (na ndipo kiasili panaitwa Zanzibar), soko la darajani ni sehemu tu katika hilo eneo. Ni eneo dogo huenda kuliko sawa na kata ya Kivukoni ambayo imebeba maeneo ya Posta hapo Dar. Ni kama vile waarusha wanaposema mjini kati.
 
sasa unataka kila upuuzi atakao uona aufungulie uzi?
 
Arusha haijawahi kujivunia mashoga bali kwa sasa inajivunia wadudu!
Ni upumbavu mkubwa watu wenye akili timamu na upeo kama Arusha kujivunia wale vijana wa ovyo ovyo wanaoitwa wadudu.

#KATAAwadudu
#FUTAwadudu
#ARUSHAsafi
Umenena ukweli. Makonda & co (maccm) ndio wanawatumia hao wadudu kwa manufaa ya kisasa. Tukisema mtaji mkubwa wa ccm ni ujinga wa mtanzania ieleweke. Huku chawa, huku wadudu.
 
Ujue mimi sipendi shobo sio mzenji ningesema niogope nn sasa? ukiniuliza huku zenji sipajua sasa nitajibu nn ? 😀 😀 Fuatilia wapi nimesema mimi ni mzenji .
Sasa uzanzibar wangu unakuuzi nini wewe?
Ama uarusha wangu unakuuma nini wewe?

Mimi nimeleta mada kuhusu athari mbaya ya uwepo wa wadudu Arusha, wewe unakuja kuhoji asili yangu ya ubara au uzanzibar, ili iweje?
 
Sasa uzanzibar wangu unakuuzi nini wewe?
Ama uarusha wangu unakuuma nini wewe?

Mimi nimeleta mada kuhusu athari mbaya ya uwepo wa wadudu Arusha, wewe unakuja kuhoji asili yangu ya ubara au uzanzibar, ili iweje?
Mamluki acha shobo , wewe ni mdudu mvaa mitumba.
 
Hivi CHAWA ni WADUDU?
 
Shida ni fulsa za ajira hakuna, unataka wapateje ugari wao?wakukabe?
We kama unashiba msosi wa baba, wenzako wanatafuta wenyewe
 
Kuna aina mbili za wadudu

Wadudu wasanii (feki) na ndio unawaona wakiwa mara na RC mara wapo kwenye mziki. Hao sio wadudu wenyewe bali wasanii tu hao.

Alafu sasa kuna,

Wadudu Og, hawa ndio watu hatari. Kwanza hawana shobo na serikali sababu ni adui wao namba moja, why? Sababu ni wahalifu wengi wanasafirisha vitu haramu kwa piki piki. Hawa utawajuaje sasa. Kwanza ni wachache sana kwa idadi. Pili wana piki piki mpya zisizo na plate namba ila sio boda boda. Tatu ni wasafi kimavazi na wanavaa mazazi ya gharama ila kazi hutawaona wakifanya.

Alafu kuna hawa wengine

Wadudu fuata mkumbo, kwa wale waliowahi kuishi Arusha watakubaliana na mimi kuwa watu wengi wa Arusha ni fuata mkumbo na ushamba mwingi sana. Sasa hapa ndio wanaibuka walevi, wavuta bangi na wajinga wengine wanaufuata mkumbo wa wadudu bila kujua wanafuata nini.

Hawq ndio utaona msibani mara wanazika kwa mikono, mara wanapenda kuhojiwa hojiwa na hizi online Tv. Ukiona hao wewe jua huyu sio mdudu huyu ni mfuata mkumbo tu hajui anachokifanya. Machalii wengi wa Arusha wanapenda kuonekana wakorofi hata kama sio wakorofi ndio maana wanakuwa wafuata mkumbo.


Tofauti na Wadudu kuna makundi mengine ambayo ukifuata mkumbo lazima upotee au hata kufariki kabisa. Mfano ni wale wa Rally watu kama Miami Gang wale ukitoka na toyo yako uliyojifunzia uchochoroni ukasema uende Rally ndio utasikia Bodo boda 6 wamekufa kwa ajali wakienda Rally Moshi/Kisongo.

Hawa Wadudu Og sio wakufanya nao masihara hata kidogo. Lazima tujue tunapoelekea ni wapi.

Nakubaliana na mleta uzi.
 
Hivi CHAWA ni WADUDU?
Hapana.
Chawa ni watu wazima wanaojitoa ufahamu, akili na utu ili kuweza kukaa kumpamba na kumsifia mtu kwa lolote lile mwisho wa siku walipwe chochote au kuvuna chochote kutoka kwa mhusika.

Wadudu ni trend style ya baadhi ya vijana wa Arusha katika kuonekana, kuvaa, kutembea, kuendesha na kuongea lakini ndani yake ikiwa imebeba tabia za kijamii zizoweza kueleweka au kuelezeka vyema.

Zote hizo ni illogical kind of bad social behaviours.
 
Umeandika vyema kabisa.
Trend ya wadudu wa Arusha imebeba na kuficha vitu vingi sana nyuma yake, na sio rahisi vyote kuvielewa au kuviweka pamoja. Mwisho sio kitu cha ku entertaining kijamii maana ni rahisi mnoo vijana wa Arusha kufuata mkumbo (mob psychology) wakati mwisho huelekea shimoni.
 
Kabisa Mkuu.
RC naona mwanzo hakujua kuwa anaingia chaka. Sahivi naona ameanza wakataa kimtindo japo kachelewa.
 
Kutetea vitu vya kijinga ni ujinga maradufu. Wewe unaona ule uvaaji wa wadudu unakufurahisha?
Ungetamani ndugu yako, rafiki yako, mtoto wako, shemeji yako avae vile halafu mtembee wote barabarani?
Ule ni utamaduni wa watu waachie hata kama huupendi hata sisi tunaona kanzu na baraghashia ni uchafu kama hupendo wadudu anza kuwakataa chawa maana wote ni wadudu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…