Wadudu wa Arusha ni uchafu wa kijamii, sio sifa njema kwa Arusha. Ududu upigwe vita!

Wadudu wa Arusha ni uchafu wa kijamii, sio sifa njema kwa Arusha. Ududu upigwe vita!

Kuna kundi la vijana mchanganyiko wa Arusha ambao hawana kazi rasmi, wengi miongoni mwao wakijihusisha na ulevi uliopindukia, uvutaji wa bangi, matumizi ya unga, uporaji, ukabaji, ubakaji na uharifu mwingine mdogo mdogo wa mtaani huku wajitengenezea swaga, mikwara na miondoko fulani yakuweza kutrend mitandaoni, wakiitwa na kujiita wadudu. Ni rahisi kuwajua kutokana na mavazi ya ajabu ajabu, lugha ya ajabu ajabu na kutembea kiajabu ajabu.

Hili sio kundi jema kimaadili kwa jamii iliyostaarabika hususani katika jiji lenye mtazamo wa kimataifa na kitalii zaidi hapa Tanzania, yaani jiji la Arusha.

Ni kiwango cha juu sana cha ujinga na upumbavu kwa taifa kutafuta sifa za kujivunia kupitia wadudu wa Arusha. Watanzania hatuwezi kujivunia tabia za wadudu.

Ule ni uchafu wa kijamii na kimaadili. Arusha haihitaji 'wadudu' ili kuvuma. Arusha inahitaji sana usafi, usalama, ustaarabu, utaratibu, usomi, uungwana, uchapakazi na uwajibikaji.

Tukatae na kupinga kabisa harakati zozote za kuukuza na kuuvumisha huo mtindo wa harakati za wadudu katika jiji la Arusha.

Hivi tulishawaza haya;
1. Mtoto wako au ndugu yako awe ni sehemu ya hao wadudu.
2. Umuone dada yako au binti yako akiwa ana trend na wadudu wa Arusha.
3. Umeone shemeji yako naye ni miongoni mwa wadudu.
4. Hivi waandaji wa mikutano ya kimataifa au watalii wanaweza kutamani kuja Arusha ikiwa jiji litakuwa limetakapaa magenge ya wadudu.

Jamani, hivi tunawajua vizuri wale wadudu?
Yaani kama taifa tunaamua kuhalalisha magenge ya uhalifu, halafu tunategemea usalama utakuwepo?

#KATAAwadudu
#FUTAwadudu
#ARUSHAsafi

Wadudu Arusha hawazidi 50, si chochote na hawana mazara yeyote popote.
 
Hapana.
Chawa ni watu wazima wanaojitoa ufahamu, akili na utu ili kuweza kukaa kumpamba na kumsifia mtu kwa lolote lile mwisho wa siku walipwe chochote au kuvuna chochote kutoka kwa mhusika.

Wadudu ni trend style ya baadhi ya vijana wa Arusha katika kuonekana, kuvaa, kutembea, kuendesha na kuongea lakini ndani yake ikiwa imebeba tabia za kijamii zizoweza kueleweka au kuelezeka vyema.

Zote hizo ni illogical kind of bad social behaviours.
Kumbe CHAWA siyo WADUDU.
Nilidhani CHAWA ni WADUDU.
 
Jipange kisaikolojia kama Mwijaku na wazee wa mikoti wa miso misondo, wadudu nao watatinga bungeni!
 
Back
Top Bottom