Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 417
Wadukuzi wanaodhaniwa kuhusika na shambulio la kimtandao wamedai malipo ya dola milioni 70 (sawa na Tsh. bilioni 162 na milioni 330) ili kufungulia mifumo waliyodukua.
Madai yao yaliwekwa wazi siku ya Jumapili katika mtandao wa kihalifu unaohusishwa na genge la wahalifu wa kimtandao la Urusi linalojulikana kama REvil. Wadukuzi hao walifanikiwa kuingilia mifumo ya mamia ya makampuni duniani.
Shirika la Habari la Reuters limeripoti kuwa wadukuzi hao wamepunguza dau kufikia dola milioni 50 (sawa na Tsh. bilioni 115 na milioni 950 ) baada ya kufanya mazungumzo na wataalamu wa masuala ya usalama wa mtandao.
Wataalamu hao wanasema wadukuzi hao wanaweza kuwa katika wakati mgumu kifedha kutokana na wahanga wao kutokuwa tayari kulipa fedha ili kukomboa taarifa zao, baada ya wadukuzi kuonekana kuwa tayari kuzungumza kupunguza dau. Wengine wanasema kuwa wadukuzi hao wamekusanya kiasi kikubwa cha taarifa kutoka kwa wahanga wao kiasi cha kushindwa kuhimili wingi huo wa taarifa.
Mifumo ya kielektroniki ya makampuni mbalimbali ya kibiashara, zikiwamo shule 11 nchini New Zealand na mamia ya maduka ya jumla nchini Uswidi yameathirika na shambulio hilo. Takriban nchi zingine 12 zimeathiriwa na shambulio hilo.
Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) limesema genge hilo lilihusika na shambulio lingine la kimtandao mwezi Mei lililofanikiwa kufunga mtandao wa kampuni kubwa zaidi ya uchakataji nyama duniani, JSB.
Rais wa Marekani, Joe Biden amesema Marekani itaiwajibisha Urusi ikiwa itathibitika kuwa imehusika na shambulio hilo.
Chanzo: VOA