Waendesha bodaboda, tabia hii inakera sana

Shamkware

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2013
Posts
1,750
Reaction score
2,283
Habari wakuu,

Niende moja kwa moja kwenye maada.

Hivi sasa tunatambua bodaboda imekuwa ni kazi inayowasaidia vijana wengi sana kujikwamua kiuchumi katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu kitu ambacho ni kizuri sana.

Lakini kazi hii baadhi ya maeneo inafanywa kwa kukosa weledi na maarifa ya kibiashara, sijui ni kwa sababu wamekuwa wengi sana au tatizo nini?

Nakereka na tabia ya vijiwe vya bodaboda yaani mtu ukitokeza tu kwenye kona wanaza kukupigia honi na miluzi utafikiri mbuzi au mbwa kaiba mboga wengine kukukimbilia hovyo hovyo. Hivi kwanini msitulie tu kijiweni abiria si tunajua mnapopatikana.

Saa nyingine maeneo ya usafiri ukishuka tu kwenye gari kelele kibao za bodaboda na ukizubaa tu mara huyu kasha chukua na begi yaani tabu tupu.

Kwanini msitulie kijiweni mkawa mnabeba abiria wenu vizuri kwa zamu, akija abiria anaenda na huyu, akija mwingine anaenda na huyu mnakuwa na rotation nzuri kwa ustaarabu ili kila mtu apate mkate wa kila siku hizi papara zenu zina boa bana.

Nawapongeza bodaboda wa Mwanza na Tabora kidogo watulivu na hizi tabia ni chache kwao kama sio hawana kabisa.

Lakini baadhi yenu badilikeni, Pia vaeni vizuri hiyo ni kazi kama kazi nyingine mnajirundika makoti machafu na kofia za hovyo na hiyo miziki ya ajabu ajabu tena kwa sauti ya juu plus kuendesho hovyo.
 
Mi wenye kelele na wanaofata hadi miguuni huwa sishuhuliki nao kabisa nashuka kwenye gari
naenda kijiweni,nachagua boda aliyekaa katulia napanda

Hio pia kwa wapiga debe stand wanatabia ya kuuliza unaenda wapi?,haujakaa Sawa wanaanza vuta begi lako

Hahaha kuna Dada alivutiwa begi mpaka likachanika jamani!!!!

Mm hadi kufika stand Ina maana najua wapi naenda,magari yameandikwa najua ninalo panda,yaniiii

Inakera sana hiyo tabia yao,ina haribu mood kabisa
 
Mbona unataka kubadili thread kutoka bida boda mpaka wapiga debe?
 

Boda boda watakuwa humu?
 
"Honi kama mbwa kaiba mboga"
 
Tumesikia tutabadilika taratibu Ndugu.
 
Hasa msamvu kuna ushenzi huo sana lol.
 
Tangu lini wavuta bangi wakawa organised , hawana akili hata chembe hao ndiomaana wanasiasa wanawageuza kuwa mitaji yao ya kisisasa
 
Kuna tabia nyingine imezuka kwa hao Boda boda kuweka exhaust pipe kupiga mlio kama baruti tene wanategea usiku wakiwa karibu na watu wanapiga na kama ukiwa na ugonjwa wa moyo unaanguka na kufa..hi tabia iko sana Dodoma maeneo ya Nzuguni,NaneNane,Dar es Salaam road hadi Ilazo..inahatarisha maisha ya wasafiri kwa miguu barabarani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…