Waendesha bodaboda, tabia hii inakera sana

Waendesha bodaboda, tabia hii inakera sana

M
Tangu lini wavuta bangi wakawa organised , hawana akili hata chembe hao ndiomaana wanasiasa wanawageuza kuwa mitaji yao ya kisisasa
Mkuu punguza ukali wa maneno halafu usipende kujumuisha makosa ya wachache kwa wote kwani wapo watu wanasomesha,kujenga,kupata mitaji ya biashara na hata kuendesha maisha in general sasa ww unaposema ndo mana wanasiasa wanawageuza mitaji ya kisiasa jee unawazungumzia vipi mama,baba lishe pamoja na wamachinga kiasi kwamba mjini kote wametawala wao jee sio mitaji kwa wanasiasa?
 
Habari wakuu,

Niende moja kwa moja kwenye maada.

Hivi sasa tunatambua bodaboda imekuwa ni kazi inayowasaidia vijana wengi sana kujikwamua kiuchumi katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu kitu ambacho ni kizuri sana.

Lakini kazi hii baadhi ya maeneo inafanywa kwa kukosa weledi na maarifa ya kibiashara, sijui ni kwa sababu wamekuwa wengi sana au tatizo nini?

Nakereka na tabia ya vijiwe vya bodaboda yaani mtu ukitokeza tu kwenye kona wanaza kukupigia honi na miluzi utafikiri mbuzi au mbwa kaiba mboga wengine kukukimbilia hovyo hovyo. Hivi kwanini msitulie tu kijiweni abiria si tunajua mnapopatikana.

Saa nyingine maeneo ya usafiri ukishuka tu kwenye gari kelele kibao za bodaboda na ukizubaa tu mara huyu kasha chukua na begi yaani tabu tupu.

Kwanini msitulie kijiweni mkawa mnabeba abiria wenu vizuri kwa zamu, akija abiria anaenda na huyu, akija mwingine anaenda na huyu mnakuwa na rotation nzuri kwa ustaarabu ili kila mtu apate mkate wa kila siku hizi papara zenu zina boa bana.

Nawapongeza bodaboda wa Mwanza na Tabora kidogo watulivu na hizi tabia ni chache kwao kama sio hawana kabisa.

Lakini baadhi yenu badilikeni, Pia vaeni vizuri hiyo ni kazi kama kazi nyingine mnajirundika makoti machafu na kofia za hovyo na hiyo miziki ya ajabu ajabu tena kwa sauti ya juu plus kuendesho hovyo.
Aisee huwa inanikera sana yaani dah
 
[emoji23][emoji23]
Yan unakuta umetokezea sehemu walipo unasikia tu honi unajua kabisa wamekuona tayari, sasa inua kichwa tu kuwaangalia chuma ishawaka, na ndo mana siku izi hukuti boda ambayo haipigi starter, manake kama hana stater atapata hadi apige kick atapata tabu sana kijiweni anakopaki
 
Mi wenye kelele na wanaofata hadi miguuni huwa sishuhuliki nao kabisa nashuka kwenye gari
naenda kijiweni,nachagua boda aliyekaa katulia napanda

Hio pia kwa wapiga debe stand wanatabia ya kuuliza unaenda wapi?,haujakaa Sawa wanaanza vuta begi lako

Hahaha kuna Dada alivutiwa begi mpaka likachanika jamani!!!!

Mm hadi kufika stand Ina maana najua wapi naenda,magari yameandikwa najua ninalo panda,yaniiii

Inakera sana hiyo tabia yao,ina haribu mood kabisa
Utakuwa Ni Dada Poa Mtulivu na sio sister Du
 
"Ifuate hela,, hela haina tabia ya kumfuata mtu". Ukikaa na hela hukaa pia ndivyo hivyo ukisimama pia.
 
Nachukizwa sana pale bodaboda anapopakia abiria halafu mziki sauti mpaka mwisho...wanafikiri abiria wote wapenda heka heka.

Hii tabia ya kudaka daka watu hovyo imeibuka pia pale Makumbusho (Dsm)stand...ile migahawa pale around.
 
Vita ni vita muraaaa[emoji23][emoji23][emoji23]umenikumbusha boda wa mbezi yaani unashuka na wenyewe wanakufungia breki miguuni


Kingsmann
 
Ndo kula yao wacha watafute pesa aisee!! Akizubaa zubaa tu atapata wapi ya kurejesha kwa bosi?? Haya Maisha tu
 
Vita ni vita muraaaa[emoji23][emoji23][emoji23]umenikumbusha boda wa mbezi yaani unashuka na wenyewe wanakufungia breki miguuni


Kingsmann
Mimi nikishuka kwenye daladala hawa hapa, wanasahau natembea tu kuingia kazini kwangu....au nikiwa na gari yangu nikishuka kwenda kununua vocha hawa hapa, tayari wameshasahau nimeshuka kwenye ndinga yangu.
 
Mimi nikishuka kwenye daladala hawa hapa, wanasahau natembea tu kuingia kazini kwangu....au nikiwa na gari yangu nikishuka kwenda kununua vocha hawa hapa, tayari wameshasahau nimeshuka kwenye ndinga yangu.
😂😂😂😂
 
Alafu kwenye suala la speed ni niii!! mimi nilimwambia mmoja sitaki ukanichubue magoti nipe niendeshe mwenyewe
 
Back
Top Bottom