Mkuu punguza ukali wa maneno halafu usipende kujumuisha makosa ya wachache kwa wote kwani wapo watu wanasomesha,kujenga,kupata mitaji ya biashara na hata kuendesha maisha in general sasa ww unaposema ndo mana wanasiasa wanawageuza mitaji ya kisiasa jee unawazungumzia vipi mama,baba lishe pamoja na wamachinga kiasi kwamba mjini kote wametawala wao jee sio mitaji kwa wanasiasa?Tangu lini wavuta bangi wakawa organised , hawana akili hata chembe hao ndiomaana wanasiasa wanawageuza kuwa mitaji yao ya kisisasa
Ile Prado yako uliuza?Sina hata hamu na boda boda, ila bas tyuuh hakna namna lol.
Aisee huwa inanikera sana yaani dahHabari wakuu,
Niende moja kwa moja kwenye maada.
Hivi sasa tunatambua bodaboda imekuwa ni kazi inayowasaidia vijana wengi sana kujikwamua kiuchumi katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu kitu ambacho ni kizuri sana.
Lakini kazi hii baadhi ya maeneo inafanywa kwa kukosa weledi na maarifa ya kibiashara, sijui ni kwa sababu wamekuwa wengi sana au tatizo nini?
Nakereka na tabia ya vijiwe vya bodaboda yaani mtu ukitokeza tu kwenye kona wanaza kukupigia honi na miluzi utafikiri mbuzi au mbwa kaiba mboga wengine kukukimbilia hovyo hovyo. Hivi kwanini msitulie tu kijiweni abiria si tunajua mnapopatikana.
Saa nyingine maeneo ya usafiri ukishuka tu kwenye gari kelele kibao za bodaboda na ukizubaa tu mara huyu kasha chukua na begi yaani tabu tupu.
Kwanini msitulie kijiweni mkawa mnabeba abiria wenu vizuri kwa zamu, akija abiria anaenda na huyu, akija mwingine anaenda na huyu mnakuwa na rotation nzuri kwa ustaarabu ili kila mtu apate mkate wa kila siku hizi papara zenu zina boa bana.
Nawapongeza bodaboda wa Mwanza na Tabora kidogo watulivu na hizi tabia ni chache kwao kama sio hawana kabisa.
Lakini baadhi yenu badilikeni, Pia vaeni vizuri hiyo ni kazi kama kazi nyingine mnajirundika makoti machafu na kofia za hovyo na hiyo miziki ya ajabu ajabu tena kwa sauti ya juu plus kuendesho hovyo.
Yan unakuta umetokezea sehemu walipo unasikia tu honi unajua kabisa wamekuona tayari, sasa inua kichwa tu kuwaangalia chuma ishawaka, na ndo mana siku izi hukuti boda ambayo haipigi starter, manake kama hana stater atapata hadi apige kick atapata tabu sana kijiweni anakopaki[emoji23][emoji23]
Utakuwa Ni Dada Poa Mtulivu na sio sister DuMi wenye kelele na wanaofata hadi miguuni huwa sishuhuliki nao kabisa nashuka kwenye gari
naenda kijiweni,nachagua boda aliyekaa katulia napanda
Hio pia kwa wapiga debe stand wanatabia ya kuuliza unaenda wapi?,haujakaa Sawa wanaanza vuta begi lako
Hahaha kuna Dada alivutiwa begi mpaka likachanika jamani!!!!
Mm hadi kufika stand Ina maana najua wapi naenda,magari yameandikwa najua ninalo panda,yaniiii
Inakera sana hiyo tabia yao,ina haribu mood kabisa
Ht Kama mkuu wanahustle wakamilishe ya Boss usafi Ni Jambo la Lazima.Kwamba boda apaki piki piki nyumbani ili afue jaketi lake?
Hujui hii kazi jamaa
So yeye hapumziki ama?Kwamba boda apaki piki piki nyumbani ili afue jaketi lake?
Hujui hii kazi jamaa
Wengine hata boksa na chupi zao zinanuka halikadhalika midomo na meno ndio usiseme ni shiidaaa kubwa.Hapo kwenye makoti machafu kiukweli wabadilike wawe wanafua.
Mimi nikishuka kwenye daladala hawa hapa, wanasahau natembea tu kuingia kazini kwangu....au nikiwa na gari yangu nikishuka kwenda kununua vocha hawa hapa, tayari wameshasahau nimeshuka kwenye ndinga yangu.Vita ni vita muraaaa[emoji23][emoji23][emoji23]umenikumbusha boda wa mbezi yaani unashuka na wenyewe wanakufungia breki miguuni
Kingsmann
ππππMimi nikishuka kwenye daladala hawa hapa, wanasahau natembea tu kuingia kazini kwangu....au nikiwa na gari yangu nikishuka kwenda kununua vocha hawa hapa, tayari wameshasahau nimeshuka kwenye ndinga yangu.
Kwl kabisa mkuuYaAni ukimwangalia mkagongana tu macho ashawasha pikipiki, sijui kwenye vikao vyao ndo ajenda zao manake ni kama wote wana tabia moja.