Kuna watu wengi kama Mbowe,Zitto,Lissu,Mnyika,Kinana, Mama na machawa wake wanamsema sana Hayati Rais John Pombe Magufuli kwa kuharibu nchi,ebu tuone hayo wanayosema kayaharibu Hayati Rais John Pombe Magufuli,RIP.
Jpm kaharibu kujenga mradi wa umeme mkubwa,Bwawa la Rufiji (Bwawa la Mwalimu Nyerere) unaozidi uwezo wa umeme wote unaozalishwa tangu mkoloni,Nyerere,Mwinyi,Mkapa na Kikwete na Sasa hakuna tena mgao wa Umeme,tutapata Umeme na kusaza,tutasahau habari ya iptl,dowans,Richmond na Escrow!.
Jpm kaharibu kujenga Reli ya Umeme,Reli ya kisasa yenye uwezo mkubwa wa kwenda kwa haraka na kubeba mzigo mkubwa kuliko Reli zote nchini,Treni ambayo itatumia saa moja na nusu toka Dar hadi Morogoro,na Massa matano tu toka Dar hadi Mwanza,hii itafanya kuharakisha Maendeleo,badala ya kusafiri Masaa 17 toka Dar hadi Mwanza.
Jpm kaharibu kujenga maghala ya kutunzia vyakula kwa mikoa yote inayozalisha vyakula kwa hifadhi za taifa letu,Sasa Taifa litakuwa na hifadhi ya kutosha ya Mazao ya Chakula.!.
Jpm kaharibu kwa kufufua shirika la ndege la atcl na ununuzi wa ndege zake kumi na moja kwa ajili ya kukuza na kuboresha sekta ya Utalii,hivi sasa tunashuhudia Watalii zaidi ya 1,000 wakitua nchini.
Jpm kaharibu kwa kutoa ruzuku ya kielimu ( elimu bure) kwa shule za misingi na sekondari,hivi sasa hakuna mtoto asiyejua kusoma wala kuandika.!.
Jpm kaharibu kwa kujenga hospitali kwa wilaya zote ambazo hazikuwa na hospitali za wilaya na vituo vya Afya zaidi ya 300 nchini baada ya kuvikuta vituo 67 tu!
Jpm kaharibu kwa kumalizia miradi iliyoanzishwa na watangulizi wake ambayo ilikwama kuendelea baada ya pesa kupigwa ama ujenzi usioridhisha kama barabara,Madaraja,Viwanja vya ndege vya zamani na Vipya,Kujenga barabara za juu na zile za kukatisha bahari ya hindi na kule ziwa Victoria na vivuko mbalimbali.
Jpm kaharibu kwa kuendelea kujenga miundombinu ya bandari na ujenzi wa meli mpya kwa maziwa ya Nyasa,Victoria na Tanganyika!.
JPM kaharibu kwa kuijenga Ikulu ya Dodoma ambayo ilishindikana kujengwa kwa miaka 50.Jpm yeye kaijenga na kahamisha makao makuu ya nchi toka Dar es Salaam hadi Dodoma,kuna watu wameumia sana wanasema kaharibu,!!?
Haya ndio ambayo kaharibu JPM,sasa kwa akili ya kawaida watu wanaomsema wana akili timamu!?