Katika uongozi wa Hayati John Pombe Magufuli tuliona utendaji wa kuacha alama katika awamu hiyo ya tano, tuliona uwajibikaji uliotukuka na kwa hakika Mabadiliko ya kimaendeleo yaligusa kila mmoja wetu, kama uhukuona basi ulishika uligundua Kweli kuna mabadiliko, kama hukushika basi ulikanyaga na uligundua mabadiliko makubwa ya kimaendeleo, ukitoka kibaha kuja Mbezi hadi Kimara uliona kazi kubwa iiliyofanyika ya ujenzi wa Barabara ya Morogoro, utajua kweli Serikali ya Rais Magufuli ilifanya kazi.
Awamu ya tano ilivyoingia Madarakani tumeona utendaji huu,
-Ujenzi wa Hostel za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (udsm).
-Ujenzi wa Hostel za Askari Magereza.
-Ununuzi wa Ndege 6 (Nyingine 2 ziko mbioni kuja).
-Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo,
-Upanuzi wa Airport Mwanza,Bukoba,Mbeya,Songea,Dodoma na Musoma.
-Upanuzi barabara ya Moroco Dsm,Mwanza na Arusha.
-Upanuzi wa Kisasa Airport Dar ,terminal 3.
-Kusimamia misingi ya kimaadili ya Utumishi wa Umma, Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
-Ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme (Standard Gauge)
-Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba.
-Ujenzi wa kota za Magomeni.
-Ununuzi na Ujenzi wa Rada Mpya ya kuongozea ndege katika anga lote la Tanzania.
-Elimu bure na Mafunzo ya kujitegemea katika Veta na Jkt kwa wahitimu wa Elimu ya Sekondari.
-Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.
-Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.
-Miradi Mikubwa ya Maji,Ujenzi wa Matenki makubwa Dar es Salaam na mradi mkubwa wa Maji toka Ziwa Victoria kuja Tabora hadi Dodoma.
-Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Jijini Tanga,Tanzania.
-Usimamizi wa Mazao Mfano Korosho,Pamba,Katani,Alizeti,kahawa,Chai,Maharage,Kilimo cha Mpunga na kutafuta masoko nje ya Nchi kwa ajili ya kupata fedha za kigeni kuinua uchumi wetu.
-Kuboresha Sekta ya Utalii kwa kununua ndege kurahisisha usafiri wa Watalii toka Mabara yote kuja Tanzania.
-Usimamizi wa Mapato ya Mali asili zetu,mfano Madini ya Dhahabu, Tanzanite na Almasi.
-Ukusanyaji Mapato baada ya kuziba nianya ya ufisadi na wizi wa mapato na mali ya Umma.
-Kujenga Utaifa na Uzalendo.
-Ujenzi wa Bwawa la Umeme katika Mto Rufiji "Stigglers Gorge".
Kwa hakika katika awamu hii ya 5,Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Magufuli iliifanya CCM kuwa Mpya katika utendaji wa kasi na wa uhakika pasipo porojo wala propaganda, Mwenye macho aliona utendaji katika sekta mbali mbali kuijenga Tanzania Mpya ambayo ilikuwa inawenda kuwa Baba la Uchumi barani Africa.