Wafahamu hawa aina mpya ya panya

Wafahamu hawa aina mpya ya panya

complex31

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2016
Posts
421
Reaction score
1,289
Habari wanajamvi,

Nimevamiwa na aina mpya ya Panya ambayo wanaitwa “Asia House Shrew” nimeambatanisha na picha hapo chini.
PHOTO-2024-08-22-20-18-55.jpg

Hawa Panya nimegundua baadhi ya mambo kwao:

1. Wanasauti kama ndege

2. Wanatembea kwa Makundi

3. Wanazaliana kwa kiwango cha juu sana

4. Hawakai ndani ya nyumba (wanapendelea kuishi maeneo ya nje kwenye Garage au majani makubwa).

5. Sio waoga kabisa

6. Hawali Sumu ukiwategea

7. Wana pua ndefu, wanene na mikia yao ni mifupi minene


Kwa muda wa miezi miwili nimehangaika kuwatokomeza kwa kutumia mitego ya Panya kuna kipindi nilikua nawaangamiza mpaka 8 kwa siku moja, nimefanikiwa kuwamaliza.

Hawa viumbe sio wa kawaida kabisa nimejaribu kusoma kwenye mitandao nimegundua wanapatikana bara la Asia na huku walikuja kwa mizigo ya kwenye Container kutoka China/ India.

Ukiwaona chukua tahadhari na jitahidi kuwaangamiza mapema kabla hawajawa mamia kwa mamia,

Nimeweka pia Picha ya mitego niliyoitumia.

IMG_7970.jpeg
IMG_7969.jpeg
IMG_7968.jpeg
PHOTO-2024-08-22-20-18-55.jpg
PHOTO-2024-08-24-23-04-13.jpg
PHOTO-2024-07-09-06-20-05.jpg
PHOTO-2024-08-24-23-16-55.jpg
PHOTO-2024-06-29-10-20-18.jpg
PHOTO-2024-09-03-21-30-01.jpg
 
Wakishaitana kikao kimoja tu kwa ajili ya kufanya evaluation, hapo ujue hauwakamati tena kwa hiyo mitego yako.

Watakuwa wanakuja ndani kwako wakiwa wameshashiba au wanabeba kabisa 'Take Away'.

Kwako wanakuwa wanakuja kutoboa na kula masofa na kukata nyaya za vifaa vya umeme kisha wanasepa.
 
Kweli mkuu upo sahihi kabisa hawa panya ni balaa zito hawaogopi mtu afu hawana haraka kabisa lakini pia Wana roho ngumu sana kufa, wanasauti Kali sana tofauti na panya hawa wa kawaida tuliowazoea kilichonishangaza sana hawafi kizembe Kuna mmoja nilikutana nae nimepiga sana panya anapiga kelele tu hadi kufa nimefyatua buti Karibu Tano ndio kazima lakini bado anapiga kelele sana
 
Back
Top Bottom