Wafahamu hawa aina mpya ya panya

Wafahamu hawa aina mpya ya panya

Mimi hao shughuli yao naijua vzr sana Yani mpka dam kabisa lakin utastukia tu asubuhi unaumia ila wakat wanakutafuna hauskii wala kuhisi chochote
Kule Hanang' ilifikia hatua watu wakawa wanalala na buti na kuvaa helmet ili panya wasimalize miguu au wasidhuru sehemu za kichwa.
 
Wameletwa na watu wanaoagiza vitu used kutoka China, Japan na India
Hapana. Wapo enzi na enzi. Huku kwetu Umasaini ndani ndani huku tunawaita "endorkony' " kule uchangani wanaitwa "Mbeva".
Vitu used a.k.a mitumba inapitia mchakato ambao panya hawezi kuuhimili atakufa - chemicals na joto kali.
 
Hawapatani na zile panya zetu na ni watata Sana hao.
 
View attachment 3086758
Hiyo gundi hakuna panya anachomoka, asubuhi unamkuta mzima anakutolea macho unaamua umpe adhabu gani
Ni Kweli. Lakini hiyo gundi ubora wake unaisha kama itaingia vumbi na wakati mwingine itanasa nzi wengi mno kiasi kwamba panya anapita juu ya nzi waliofia hapo. Gundi haisafishiki i.e.huwezi kuikarabati ikishachafuliwa na nzi, mende,vipepeo na wadudu wengineo kwa kunasa hapo. Ukijisahau, panya aliyenasa hapo atakufa kwa njaa na ataozea hapohapo.
 
Kiboko hao kelele hatari wakachukua 20,000 juu ya dressing table yangu kwakua nilikua pekeangu nikajua ni hao tu
Baada ya siku kadhaa kupita nikaziona maajabu hazikuliwa
 
Hao panya wengine n wakutengeneza pia wengine wanaletwa na watu kutoka china hawa wa bidhaa used
 
Niliwahi kuwaona Zanzibar kwenye moja ya hoteli
Wakazi wa Zanzibar pia wanasema huko wako wengi hivo ukiangalia sehem ambazo wakazi wanasema wamewaona ni maeneo yenye muingiliano wa mizigo kutoka bara la Asia na Tanzania kama Zanzibar, Kariakoo, Kigamboni
 
Wakazi wa Zanzibar pia wanasema huko wako wengi hivo ukiangalia sehem ambazo wakazi wanasema wamewaona ni maeneo yenye muingiliano wa mizigo kutoka bara la Asia na Tanzania kama Zanzibar, Kariakoo, Kigamboni
Zanzibar tunawaita viruka njia.

Kwangu walikuwa wanaingia kupitia tundu la maji chooni wanakula sabuni na soap dish yake. Kuna siku nikawacha night dress yangu nimeitundika kwenye hanger ya bafuni waliitafuna tafuna night yangu mpya 😡
Dawa yao ikawa usiku wakati kabla kulala naweka chupa kwenye tundu ili wasiingie
 
Wanaitwa panya mkembe hao mbona wapo toka zama za mkwere,nimewaona kwa mara ya kwanza miaka ya 2000.
 
Back
Top Bottom