Wafahamu hawa aina mpya ya panya

Wafahamu hawa aina mpya ya panya

Habari wanajamvi,

Nimevamiwa na aina mpya ya Panya ambayo wanaitwa “Asia House Shrew” nimeambatanisha na picha hapo chini,

Hawa Panya nimegundua baadhi ya mambo kwao,
1. Wanasauti kama ndege

2. Wanatembea kwa Makundi

3. Wanazaliana kwa kiwango cha juu sana

4. Hawakai ndani ya nyumba (wanapendelea kuishi maeneo ya nje kwenye Garage au majani makubwa).

5. Sio waoga kabisa

6. Hawali Sumu ukiwategea

7. Wana pua ndefu, wanene na mikia yao ni mifupi minene

Kwa muda wa miezi miwili nimehangaika kuwatokomeza kwa kutumia mitego ya Panya kuna kipindi nilikua nawaangamiza mpaka 8 kwa siku moja, nimefanikiwa kuwamaliza.

Hawa viumbe sio wa kawaida kabisa nimejaribu kusoma kwenye mitandao nimegundua wanapatikana bara la Asia na huku walikuja kwa mizigo ya kwenye Container kutoka China/ India.

Ukiwaona chukua tahadhari na jitahidi kuwaangamiza mapema kabla hawajawa mamia kwa mamia,

Nimeweka pia Picha ya mitego niliyoitumia

View attachment 3086270View attachment 3086271View attachment 3086272View attachment 3086275View attachment 3086276View attachment 3086277View attachment 3086278View attachment 3086279View attachment 3086280
Naona umeweka picha kwa hasira kinoma 😂😂😂😂 sema umeeleweka mkuu
 
Habari wanajamvi,

Nimevamiwa na aina mpya ya Panya ambayo wanaitwa “Asia House Shrew” nimeambatanisha na picha hapo chini,

Hawa Panya nimegundua baadhi ya mambo kwao,
1. Wanasauti kama ndege

2. Wanatembea kwa Makundi

3. Wanazaliana kwa kiwango cha juu sana

4. Hawakai ndani ya nyumba (wanapendelea kuishi maeneo ya nje kwenye Garage au majani makubwa).

5. Sio waoga kabisa

6. Hawali Sumu ukiwategea

7. Wana pua ndefu, wanene na mikia yao ni mifupi minene

Kwa muda wa miezi miwili nimehangaika kuwatokomeza kwa kutumia mitego ya Panya kuna kipindi nilikua nawaangamiza mpaka 8 kwa siku moja, nimefanikiwa kuwamaliza.

Hawa viumbe sio wa kawaida kabisa nimejaribu kusoma kwenye mitandao nimegundua wanapatikana bara la Asia na huku walikuja kwa mizigo ya kwenye Container kutoka China/ India.

Ukiwaona chukua tahadhari na jitahidi kuwaangamiza mapema kabla hawajawa mamia kwa mamia,

Nimeweka pia Picha ya mitego niliyoitumia

Wananchi turuhusiwe kununua bastola ili tuwaangamize kirahisi. Hata hivyo ukatili uliomfanyia panya huyo kwa kumuua kwa kumbana na mtego haukubaliki, naomba watetezi wa haki za wanyama wakuchukulie hatua kali, Mods wa JF hakikisheni mtuhumiwa anatambulika ili akamatwe, na TSPCA mpo?
 
Kweli mkuu upo sahihi kabisa hawa panya ni balaa zito hawaogopi mtu afu hawana haraka kabisa lakini pia Wana roho ngumu sana kufa, wanasauti Kali sana tofauti na panya hawa wa kawaida tuliowazoea kilichonishangaza sana hawafi kizembe Kuna mmoja nilikutana nae nimepiga sana panya anapiga kelele tu hadi kufa nimefyatua buti Karibu Tano ndio kazima lakini bado anapiga kelele sana
"Wana roho ngumu sana kufa", hawana tofauti na wajomba zao CCM, pamoja na kusemana juu ya wizi wa kura lakini bado wamo tu!
 
Wakishaitana kikao kimoja tu kwa ajili ya kufanya evaluation, hapo ujue hauwakamati tena kwa hiyo mitego yako.

Watakuwa wanakuja ndani kwako wakiwa wameshashiba au wanabeba kabisa 'Take Away'.

Kwako wanakuwa wanakuja kutoboa na kula masofa na kukata nyaya za vifaa vya umeme kisha wanasepa.
umesahau kula document za muhimu
 
Mkuu hao hawana shida kabisa ndo maana huwa wanakata nje kwenye taka, huwa wanasaidia Sana kuua wadudu hatari eg tandu, nge na nyoka wadogo, wasio hatari kama mende na Panya wadogo(mice) na ndani huwa hawaingii...na ukiona ameingia ndani ujue alikiwa anakimbiza mdudu ili amle or else haingii ndani.
Sumu wanayo Kwa ajili ya kuua wadudu akikuuma binadamu ujue ulishika vibaya au anajilinda dhidi ya kipigo chako.

Kwa Nini haliwi na paka sababu huwa akifa mwili wake hutoa harufu na mbaya so make unfavourable to be eaten 😂

Home wapo na wamesaidia sana kwenye garden 😊

I attach their boss photo 😂
 
Attachments

  • Mr._Big_Render.png
    Mr._Big_Render.png
    1,021.4 KB · Views: 3
Back
Top Bottom