Wafahamu macelebrity wa JF na sifa zao

Wafahamu macelebrity wa JF na sifa zao

Niko JF tangu kitambo na wengi sana humu mmenikuta nishaijua hii mitaa sema sikua active sana kwenye huu mtandao pendwa ila ktk kuishi humu nimegundua kuna watu wenye ushawishi sana humu JF sijui tuwaite JELEBRITY au sio

Unakuta kuna raia umu hata wakicomment nukta watu wanamiminika kureply likes kibao..

Kuna haja JF iwatambue hawa watu wapate verification ya account zao...

Kuna watu ambao nyuz zao ndo zinaongoza kwa kupata engagement achana na umaarufu wa uzi wa kula kimasihara..

Naomba niwatambue wafuatao km watu wa nguvu sana humu jukwaani kutokana na mchango wao kupitia post zao na ikiwezekana wajipost siku moja moja tuwajue siku tukikutana nao mtaani tuwabless mbili tatu moyo uelee

1;MSHANA JR;namuonaga km mtu fulani mwny hekima sana kupitia thread zake,usipite thread za huyu mwamba km unataka kupata madini mbalimbali

2;mzabzab; huyu mwamba matusi sana yuko sana mitaa ya jukwaa la mahusiano kule,uzi wa jukwaa la MMU bila comment ya huyu mwamba bado sana uo haujaenda mjini

3;Gentamicine;kama shabiki wa Chelsea na Simba huwa lazma nipitiw jukwaaa la Sports na huyu jamaa anakiwasha sana uko na kutoa za ndaaaani though anaonekana raia hawamuelewi mpikaji sana wa data

4;Robert Heriel; Mzee wakuitwa Taikon wa Fasihi mwamba anatoa zile ngumu kumeza yaani kupitia misimamo yake so huwa siwez kupita uzi alouanzisha huyu jamaa

5;Rikiboy;Mzee wa uzi wa kula kimasihara yaan jamaa katoa hit song moja ya kudumu mpk mwisho wa hii app moja ya uzi ambao uko active mda wote washatokea watumishi na wahubiri wakashindwa kuuzuia

6;Sky Eclat;yuko JF since 2012 namuona km Lady Jay Dee wa humu JF huyu madam,nawish nimuone yukoje

TOA APPRECIATION ZAKO KWA WANA JF wengne unaowakubali ambao wanafanya vizuri[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji115][emoji115]
Nikajua utanisahau mkuu... much love 😀 😀 😀 😀 uzi wetu pendwa udumu
 
Unaweza kumponda mtu hivyo kuwa si mkongwe kwa kuangalia mwaka aliojiunga.

Lakini nikupe mfano mimi sikuwa registered member ila nimekuwa msomaji mzuri sana wa nyuzi na forums mbalimali tangu mwaka 2007 lakini nikaja kutengeneza akaunti yangu rasmi mwaka huu 2022

Kwa mfano kuna forums ya mambo ya historia. Huenda watu wa kule wasiwe maarufu kama wa kwenye MMU na siasa.

Ila kwa heshima kule kuna mzee wetu Mohamed Said yule mzee ana madini mengi sana ya historia ya Tanganyika pia kuna Nyani Ngabu heshima kwao watu hao pia.
Wewe sasa mkongwe nimependa ulivyo insight ukweli kuwa wanaoona maarufu ni hawa wachangia mapenzi, uchawi na vichekesho.
Ila miamba kama Kiranga hawaijui
 
Kuna Kiranga huyu jamaa alinivutia sana kuipenda jamiiforums na kunisanua kuhusu hizi dini, kikubwa critical and logical reasoning nimejifunza kwa huyu mwamba, nakumbuka mtaa wangu ulikua jamii intelligence naanzia uko uko namalizia uko uko huyu jamaa bhana hoja zake kama haupo neutral hauwezi kumwelewa., kuna siku moja Mshana Jr aliingia kichwa kichwa akamuuliza "kiranga una akili?" Kiranga nae kabla ya kujibu akataka kujua akili ni nini kwaiyo akauliza "akili ni nini". Mjadala ukaishia hapo kila moja anahisi akijibu tu anapigwa knock-out mpaka thread ya 10 mshana hataki kufafanua akili ni nini ili ajibiwe na kiranga anataka afafanuliwe kwanza akili ni nini ili ajibu kama anayo au hana
Hahahaa,

NaonauUnaukumbuka ule mjadala bado.

Asante kwa kunitaja kwa kumbukumbu nzuri.
 
Mchawi Mstaafu Mshana Jr ni kiboko jamaa anajua mambo mengi kwenye angle mbalimbali. JF walikosea sana kutomrecognize Mshana wakampa tuzo yule mzanzibari na maamuma Mohammedi.
natamani siku 1 ID zetu fame ziwe wazi ili nimjue Kiranga ni nani maana sio kwa ubishi ule.
Mwamba sana huyu sijawah kuukosa uzi wake hata mmoja,madini sana, appreciation kwake Mshana Jr

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom