Wafahamu Wajumbe wa Bodi ya TCRA iliyovunjwa

Wafahamu Wajumbe wa Bodi ya TCRA iliyovunjwa


Naamini wakati wanateuliwa sifa pekee iliyoangaliwa ni utendaji na ubora katika tasnia husika na si kingine.
 
Kuwaza kubalansi kila nafasi kwa kuangalia majina ya kijihad au kigalatia NDIO UDINI wenyewe.
Mimi sioni shida kama wateuliwa wote wana majina ya kihindi tu au kiarabu tu au kizungu tu au kimatumbi tu. Muhimu ni kuwa vigezo vya dini havikuangaliwa wakati wa kuteua bali weledi, uwezo na sifa za kitaaluma pekee.

After all sio kila John Smith ni mkristo wa kweli na sio kila Shabani Masoud ni mwisiam wa kweli.
Unakosea. Umuhimu wa kuwa na watu wa dini tofauti ni kuongeza uwezo wa bodi kuangalia ishu kutoka pande zote. Ukiwa na waislamu na wakristu Bodi itaweza kuelewa namna uamuzi wao unaweza kuwagusa watu wa dini hizo. Ni kama vile uwepo wa wanawake unaleta "lived experience" ya wanawake katika bodi. Diversity ni muhimu sana katika taasisi yeyote.

Amandla...
 
Upo Uzi mwingine humu ndani unaowaongelea hao wajumbe utafute uone CV zao.
Wewe ulio uona si ungeweka link yake humu ili kila mmoja wetu azione hizo CV? Mimi nikitafuta na kuzikosa nitaona kama vile unadanganya wakati inawezekana kuwa utafutaji wangu una walakin. Tuwekee hiyo link tumalize ubishi.

Amandla...
 
This time around, wateuliwe Wagalatia tupu.

Na tusisikie kelele kama ambavyo sisi tumekaa kimya.
Tufanye hivyo kwa Baraza la mawaziri,makatibu wakuu wizara,wakuu wa mikoa,wilaya,ras,das,ded..yaani Kama wa dini Fulani ni wengi basi wapunguzww wateuliwe wa dini nyingine nao wawe wengi
 
Tukiondoa "majina" bodi ilikuwa na tija yeyote? Kwangu Allihamdulillah kutumbuliwa kwao tehteh....
 
Nasikia Rais kavunja Bodi ya TCRA. Naona hawa hapa ndio walikua Wajumbe wake

MAWASILIANO: BODI YA TCRA YAVUNJWA

Rais Samia Suluhu Hassan amevunja Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwa ni takriban mwaka mmoja tangu amteue Mwenyekiti wa Bodi hiyo

Kwa mujibu taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Rais amefanya uamuzi kuanzia Novemba 7, 2023

Waliokuwa Wajumbe wa Bodi ni Mhandisi Othman S. Khatib (Mwenyekiti), Khalfan S. Saleh (Makamu Mwenyeki), Mzee S. Mndewa (Mjumbe), Fatuma S. Ikuja (Mjumbe), Abdallah B. Katunzi (Mjumbe) na Rehema J. Khalid (Mjumbe)


View attachment 2808520

Kwani wamefanya nini? 😂 😂 😂 😂 😀 😀 😀 😀 😀 😀
 
Watu wanafungua code ngumu kweli,Utasikia ooh udini mara ooh uzanzibari n.k.
Kwenye udini tukisema tuchunguze na Mafisadi tukuka wa dini hizo utakuta wenzetu hao wanaunafuu kiasi😁😁😁😁😁
 
Rais Samia Suluhu Hassan leo 7-11-2023 akiwa Marakesh Morocco amevunja Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwa ni takriban mwaka mmoja tangu amteue Mwenyekiti wa Bodi hiyo

Kwa mujibu taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Rais amefanya uamuzi kuanzia Novemba 7, 2023
Waliokuwa Wajumbe wa Bodi hiyo ni:-​

1. Mhandisi Othman S. Khatib (Mwenyekiti),
2. Khalfan S. Saleh (Makamu Mwenyeki)
3. Mzee S. Mndewa (Mjumbe)
4. Fatuma S. Ikuja (Mjumbe)
5. Abdallah B. Katunzi (Mjumbe)
6. Rehema J. Khalid (Mjumbe

KATIBU MKUU WA WIZARA NI :- Mohamed Hamis Abdulla
Mkurugenzi wa TCRA ni. DKT JABIRI BAKARI.

Haikuwa na balance ya wajumbe. Ishmael alitoa yeye tuu akamuacha Izack mtupu. Bwana akachukizwa.

Je, ni kweli kama watu wanavyo nongona kuwa Miaka 6 kurudi nyuma mpaka Sasa nchi hii imeathiriwa sana na ukabila , udini na ujinsia?

Mungu airudishe Tanzania ile tulioijua miaka yote

Ni makosa makubwa kufikiria kila mhandisi ni mbobezi na ana msaada pale atakapowekwa. Kuna wengine wanatembelea nyota ya uhandisi. Ukiona wanayofanya unashangaa kama kweli zimo zote
 
Back
Top Bottom