Wafanyabiashara zaidi ya 100 wa maduka katikati ya jiji la Arusha wamefunga maduka yao bila kikomo wakipinga kupandishiwa mara dufu Kodi na halmashauri ya jiji la Arusha kutoka kiasi Cha sh,150,000 hadi sh,300,000 kinyume na utaratibu.
Aidha wamemwomba Rais Samia Suluhu na waziri Ummy Mwalimu kuingilia Kati ili kuondoa unyanyasaji huo unaosababisha washindwe kufanya biashara zao kwa uhuru.
Wakiongea na waandishi wa habari Jana, wafanyabiashara hao ambao ni wajenzi wa maduka hayo yaliyopo eneo la ranger safari, wamedai kuwa kitendo Cha halmashauri hiyo kupandisha Kodi ya pango kinyemela hakikuwa na makubaliano bali halmashauri hiyo imetumia ubabe wakati mwafaka ulikuwa bado haujafikiwa.
Baadhi ya Wafanyabiashara hao Godluck Alick na Amani Mollel wamedai kuwa Jana siku ya kusherehekea miaka 60 ya uhuru wa Tanzania ,baadhi ya maofisa wa jiji wakiwa na migambo kadhaa walivamia katika maduka hayo na kuwakamata viongozi wa wafanyabiashara hao na kuwapelekea polisi wakidai wanashinikiza wafanyabiashara wasilipe Kodi.
"Hili suala lilishazungumziwa na mkuu wa wilaya aliyepita Mbele ya mkurugenzi wa jiji na kufikia mwafaka kwamba wafanyabiashara hao waendeleee kulipa Kodi ya zamani ya sh,laki Moja na nusu ,lakini tumeshangaa hapo jana jambo hili limeibuka upya"alisema Mollel.
Naye mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara hao,Loken Masawe na Katibu wake,Hamidur Jamari wamemwomba Mkurugenzi wa jiji la Arusha kukaa na Wafanyabiashara hao ili kuondoa sintofahamu inayojitokez Kwa Sasa Kwa kuwa msuguano huyo umekuwa wa muda mrefu unaosababisha adha Kwa wananchi.
"Hawa Wafanyabiashara ndio waliojenga haya maduka wanamchabgi wao mkubwa Kwa Serikali,huyu mkurugenzi akutane na Wafanyabiashara na awaheshimu Kwa mchango wao kitendo Cha kuwatumia mgambo siku ya uhuru na kuwakamata viongozi wao awaombe Radhi sio Cha kiungwama"alisema Masawe.
Aidha mwenyekiti huyo amedai kuwa wafanyabiashara hao hawatafungua maduka Yao katika muda usiojulikana ili kushinikiza halmashauri hiyo kukaa kitako ili kufikia mwafaka Kwa kuwa wao ni sehemu ya wamiliki wa maduka hayo.
Katika hatua nyingine Wafanyabiashara waliopanga katika maduka mapya ya halmashauri hiyo yaliyopo eneo la Disemba nao wamegoma kufungua wakidai kiwango cha Kodi wanachotozwa na halmashauri hiyo ni kikubwa na sio rafiki na hakina usawa katika maduka hayo.
Mmoja ya wapangaji wa maduka hayo,Modester Kapinga alidai kuwa Kodi wanayolipa kwa Sasa ya sh,300,000, 400,000,500,000 na 600,000 ni kubwa na haiwalipi ukizingatia kwamba maduka hayo ni madogo na haya biashara.
Akijibu hoja za Wafanyabiashara hao mstahiki meya wa jiji la Arusha Maximilian Iranghe alisema uamuzi wa kupandisha Kodi ni uamuzi uliotolewa na baraza la madiwani baada ya kujiridhisha kuwa Wafanyabiashara hao wanalipwa kiasi kidogo Cha Kodi .
"Haya maamuzi yametolewa na baraza la madiwani halmashauri ni watekelezaji tu ,hao Wafanyabiashara wanalipwa Kodi ndogo Sana"alisema Meya Kwa kifupi.
Awali mkurugenzi wa jiji la Arusha,Dkt John Pima alidai kuwa suala la Kodi halina mjadala na asiyetaka kulipa kiasi cha sh, 300,000 Kwa mwezi aondoke .
"Hayo maduka ni Mali ya halmashauri na hakuna mjenzi aliyejenga hao ni wapangaji kama wapangaji wengine na hawawwI kutupangia Bei ya pango na asiyetaka kulipa aondoke "alisema
Aliongeza kuwa wiki ijayo halmashauri hiyo inaanza operesheni ya kuwaondoa wenye Madeni makubwa .
Ends...
View attachment 2040142View attachment 2040143View attachment 2040144View attachment 2040145