Wafanyabiashara Halali wa Mbagala wanawezaje kulipa kodi ikiwa Wamezibwa 100% na Wamachinga?

I have been there once, I spent 15 mins kichwa kiliuma aiseee vile vispika Sasa Kila mtu anacho kinapiga kelele, mama lishe wanamisufuria imejaa mapilau wanauza barabarani uani ni tafrani in short wapaite Mbagala Republic
 
hii nchi ni ya kishenzi na kishamba sana, yani mtu anaekeka biashara mbele ya mlango wako halafu yeye ndie anakuvimbia na hata serikali inamlinda yeye
 
Usichojua wale MACHINGA wengi wao pale wanachukua mzigo kutoka kwenye maduka makubwa hapohapo ndiyo wanaenda kuuza kwa makubaliano kifupi zile biashara ni zawenye maduka makubwa palepale wale MACHINGA ni wauzaji tu wakiuza pesa wanapeleka kwa wenye maduka wao wanapewa chochote kitu
 
Halafu wenye maduka ya Nafaka wana utaratibu wa kishebzi na wizi. Iko hivi Unapo nunua mchele mfano kilo moja ni sh 2000 na umenunua kilo 10, badala ya kulipa sh 20,000 tu utadaiwa sh 20200. Hiyo sh 200 inayozidi ni service charge ( gharama ya kuhudumiwa). Hiyo Ndiyo Mbagala Republic.
 
tatizo sio hao wamachinga tatizo ni serikali yetu haijui kutumia rasilimali watu. Baadae nitafafanua vizuri
 
umeandika baadhi ya yale niliyotaka kusema. Na hiyo ndio njia wanayotumia hao wenye maduka makubwa kukwepa kodi maana wanasingizia wamachinga wakati wamachinga ndo wateja na wauzaji wa biashara zao
 
Sijawah kusifia uongozi wa samia isipokuwa katika suala la wamachinga japo lilikuwa na mapungufu lakin afadhali alivowaondoa barabaran japo kuna baadhi ya maeneo kama kariakoo wameshindikana kuondoka
 
umeandika baadhi ya yale niliyotaka kusema. Na hiyo ndio njia wanayotumia hao wenye maduka makubwa kukwepa kodi maana wanasingizia wamachinga wakati wamachinga ndo wateja na wauzaji wa biashara zao
Hii hoja haina Mashiko, unawezaje kuwapa mali yako ya thamani watu usiowajua?
 
Sasa hivi serikali haiwezi kufanya lolote! Mwaka huu na mwaka kesho ni kura mkuu!
 
Mbagala ipi hiyo yenye maduka ya wahindi? Barabara ya kuelekea wapi hiyo inayozibwa na mama ntilienwasonga ugali?
Meya yupi huyo mwenye mamlaka ya kuzuia vyombo vya Dola kutekeleza Sheria za nchi?

Fika kariakoo uone machiga wa pale ndio urudintena
 
Mada ya leo ni Mbagala, kariakoo tutakuja.

Kingine ulichokisahau ni hiki, Vyombo vya Dola vya Tanzania havijawahi kufanya kazi bila kutumwa na ccm
 
Mkuu wa mkoa washirikiane na meya kuhakikisha watu wote tunalipa kodi,si TRA kutupigia simu sisi tu Tena kila baada ya miez3.
Bado leseni,ada ya taka,ulinzi.daah
Waeke mazingira mazuri ya kibiashara kwa wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…