DOKEZO Wafanyabiashara Kariakoo kugoma Mei 15, 2023

DOKEZO Wafanyabiashara Kariakoo kugoma Mei 15, 2023

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Twin Tower

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2023
Posts
2,170
Reaction score
3,067
Kuna tetesi ya mgomo wa wafanyabiashara eneo la Kariakoo.

mgomo 2.jpg

Sababu za kuitisha mgomo;
1. Urasimu bandarini
2. Usajili wa stoo
3. Kamata kamata hovyo ya wateja kwa ukuguzi wa risiti

Wao wapo tayari kufanya biashara kwa uhuru na kulipa kodi bila mambo ya rushwa rushwa na maonezi.

mgomo 1.jpg

Rai kwa mamlaka zinazohusika kuchukua hatua za haraka hili jambo lisitokee. Pale ni kitovu cha biashara ukanda huu. Makosa kidogo tunaweza hamisha hii biashara kwa jirani zetu.

mgomo.jpg
 
Tanzania tunaagiza mno kuliko tunachozalisha. Hiyo inasababisha biashara kuwa nyingi kuliko wateja. Hapo kitakachotokea biashara kuwa ngumu, utokaji mgumu, fitina na hujuma Zitakuwa nyingi. Vita za kibiashara pia zinasababisha watu kufanyiana hujuma kwa kupandishiana kodi na tozo na fitina bandarini.

Hata kodi zikipunguzwa itapunguza makali kwa muda tu, baadae yatarudi yaleyale

Bandari inatakiwa iexport vitu toka tz kwenda nchi zingine duniani. Sio kuagiza tu.
 
Karia koo ni soko kubwa sana hapa Afrika mashariki na kati pamoja na kusini. Kariakoo ukienda kununua vitu jumla namanisha nguo, viatu mashine mbalimbali pamoja na vifaa vyote vya msingi nyumbani . Utakutana na wakongo, wazambia, wamalawai wa nyasa, wakenya, waganda nk

Watu wanataka kujenga nchi yetu lakini kuna croocks wapo hapo katikati wanaweka vizuizi wale rushwa.
 
Tanzania tunaagiza mno kuliko tunachozalisha. Hiyo inasababisha biashara kuwa nyingi kuliko wateja. Hapo kitakachotokea biashara kuwa ngumu, utokaji mgumu, fitina na hujuma Zitakuwa nyingi.

Hata kodi zikipunguzwa itapunguza makali kwa muda tu, baadae yatarudi yaleyale

Bandari inatakiwa iexport vitu toka tz kwenda nchi zingine duniani. Sio kuagiza tu.
Hatari Sana , viwanda vyetu vinahujumiwa na mapinduz ya kilimo ya bashe hatuyataki mwisho tumebak kuexport drugs na kujiuza
 
Kuna tetesi ya mgomo wa wafanyabiashara eneo la kariakoo.
Sababu za kuitisha mgomo
1. Urasimu bandarini
2. Usajili wa stoo
3. Kamata kamata hovyo ya wateja kwa ukuaguzi wa risiti

Wao wapo tayari kufanya biashara kwa uhuru na kulipa kodi bila mambo ya rushwa rushwa na maonezi.

Rai kwa mamlaka zinazohusika kuchukua hatua za haraka hili jambo lisitokee. Pale ni kitovu cha biashara ukanda huu. Makosa kidogo tunaweza hamisha hii biashara kwa jirani zetu.
Yani wanagoma wakati kuna msiba wa taifa?
 
Waachane Ni migomo ni njia ya kizamani Sana yakutatua migogoro...wakae meza moja nawahusika wayamalize.
"Ila stakabadhi za kielectronic watoe waache janja janja "
 
Tanzania tunaagiza mno kuliko tunachozalisha. Hiyo inasababisha biashara kuwa nyingi kuliko wateja. Hapo kitakachotokea biashara kuwa ngumu, utokaji mgumu, fitina na hujuma Zitakuwa nyingi. Vita za kibiashara pia zinasababisha watu kufanyiana hujuma kwa kupandishiana kodi na tozo na fitina bandarini.

Hata kodi zikipunguzwa itapunguza makali kwa muda tu, baadae yatarudi yaleyale

Bandari inatakiwa iexport vitu toka tz kwenda nchi zingine duniani. Sio kuagiza tu.
Mkuu heshima kwako.

Unadhan nin kifanyike?, Kumbuka serikali haina uwezo wa kufanya biashara wala kuendesha viwanda.
 
Kariakoo hawawezi goma hataa siku Moja, maana hawana ushirikiano hata kidogo TRA kila siku wanawanyanyasa na hawawez hata kujitetea mfano wanaofanya biashara ya viatu TRA wanajua namna ya kula hela zao

Kama ni mizigo inayoenda nje labda Congo, Zambia, Malawi n.k TRA wanabana jiran na road ya kuingilia Transporter husika, na transporter za zilizopo huku ilala kama zinazoenda Lubumbashi na Lusaka TRA wanasimamamisha gari lao ile mitaa ya karume 😁😁 wanasubiri gari lenye turubai

Kama ni huku mjini bas kila transporter panakua na agent wa TRA anazuia mizigo isiandikishwe anasubir jioni ifike mwisho wa siku anawachaji 200k anasepa zake

Wafanyabiashara wengi wanaonewa lkn hawana umoja

Kuna siku walikamata mzigo wa mchina thamani ya mzigo ilikua 40M ila mchina kwenye risiti aliandika 27M kwenye thamani TRA hawakua na shida ila changamoto ilikua majina yaliyo kwenye risiti mchina aliandika jina Moja tu, TRA walinambia kusawazisha mambo niwape 3M ili yaishe kimya kimya nikakaza wakanipa form yao mzigo ukalala ofisini kwao pale stesheni siku ya pili nlipamabania hadi nkautoa bila kulipa hata mia

Nlimwambia mchina wanataka 800k akanipa 🤣🤣
 
Kuna tetesi ya mgomo wa wafanyabiashara eneo la kariakoo.
Sababu za kuitisha mgomo
1. Urasimu bandarini
2. Usajili wa stoo
3. Kamata kamata hovyo ya wateja kwa ukuaguzi wa risiti

Wao wapo tayari kufanya biashara kwa uhuru na kulipa kodi bila mambo ya rushwa rushwa na maonezi.

Rai kwa mamlaka zinazohusika kuchukua hatua za haraka hili jambo lisitokee. Pale ni kitovu cha biashara ukanda huu. Makosa kidogo tunaweza hamisha hii biashara kwa jirani zetu.
Wakinga na wachaga wamezoea wizi sasa wamebanwa na serkali huku china ikifanya yake kwa kunyooka wanalialia tu

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatari Sana , viwanda vyetu vinahujumiwa na mapinduz ya kilimo ya bashe hatuyataki mwisho tumebak kuexport drugs na kujiuza
😂😂😂
Inahitajika akili ya ziada ili kuelewa mambo hayo. Hii akili ya kuagiza (import) yaani kila kitu tunaagiza ndio imelemaza akili. Kila mtu ni kuagiza tu, china,dubai, uturuki, dubai. Hapo kiufupi wafanyabiashara wanaona wanafaidika. Ila kiukweli wanafaidika wachina. Maana bidhaa nyingi mno za kariakoo ni za china.
Huu mgogoro wa sasa hivi chanzo ni wafanyabiashara wa vitenge, nasikia kuna kodi imeletwa kwa vitenge toka nje.
Ila yote kwa yote soko la kariakoo linamfaidisha sana mchina.

NB: Bashe ana hoja ila sio kila mtu atamuelewa. Tunatofautiana akili. Siku bashe akikomaa na pamba. Na viwanda vya kutengeneza nguo na pamba, pia nguo ambazo zina mchanganyiko wa pamba na synthetic fibers nitamuelewa zaidi. Ila ni aibu sana, nchi za jangwa wanalima kuliko sisi na tunaagiza toka nchi zenye jangwa, pia mpaka leo tunaagiza ngano 😂😂😂
 
Back
Top Bottom