HIMARS
JF-Expert Member
- Jan 23, 2012
- 70,791
- 98,334
Kuna wengine nimeona wanafunguaTRA wanapigwa mapema na Kariakoo Dabi!! Utakuja niambia!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna wengine nimeona wanafunguaTRA wanapigwa mapema na Kariakoo Dabi!! Utakuja niambia!!
Wapi hapo tuwafate hao wasaliti?Kuna wengine nimeona wanafungua
Mtaa wapouza pikipiki kuna Mhindi kafungua duka lake, yuko karibu na Cate hotelWapi hapo tuwafate hao wasaliti?
Ni kweli huu mgomo hauna kikomo?Mpaka Abdul mtoto wa rais nae hajafungua duka
Umoja ni kitu kizuri sana, bora watu wakubali hasara hata ya siku 3 ila ujumbe uwe umewafikia.Mpaka Abdul mtoto wa rais nae hajafungua duka
Huu mgomo una watu wakubwa hivyo watu itabidi wakomae tu, Serikali itawasikilizaNi kweli huu mgomo hauna kikomo?
kama vile namwona Omolo Odinga katia mguu bongoKuna tetesi ya mgomo wa wafanyabiashara eneo la Kariakoo.
View attachment 2622388
Sababu za kuitisha mgomo;
1. Urasimu bandarini
2. Usajili wa stoo
3. Kamata kamata hovyo ya wateja kwa ukuguzi wa risiti
Wao wapo tayari kufanya biashara kwa uhuru na kulipa kodi bila mambo ya rushwa rushwa na maonezi.
View attachment 2622389
Rai kwa mamlaka zinazohusika kuchukua hatua za haraka hili jambo lisitokee. Pale ni kitovu cha biashara ukanda huu. Makosa kidogo tunaweza hamisha hii biashara kwa jirani zetu.
Acha kujitoa akili Ndg.....inamana huoni huu ukiritimba unaoendelea kila sekta....?!sasa bro, wewe na we si mtanzania? hebu tuonyeshe shamba la ngano au la mahindi unalolima? sisi wananchi tunatakiwa kuchukua hatua kufanya kilimo biashara, sidhani kama serikali haijaweka mazingira rafiki ya kilimo. ukisafiri kwa basi unakutana na mapori kila sehemu yapo tu, hakuna watu wa kulima ila tunalaumu serikali kwamba inafanya watu waagize chakula nje? hizo akili au matope? wewe umefanya nini walau ili kutuhakikishia kuwa ukishika nchi utakuwa na pa kuanzia.
Ukichunguza pande zote mbili, TRA na wafanyabiashara, wana hoja kwenye madai yao.
Itumike busara na hekima badala ya nguvu na makali ya Sheria (ambazo nyingine si za haki).
Swali: Kwa nini watu/wafanyabiashara wanakwepa au hawapendi kulipa kodi?
Jibu: Kodi ni nyingi na viwango ni vikubwa.
Solutions:
1. Serikali na TRA (kwa upande mmoja) watunge na kuweka viwango rafiki vya kodi.
•Je Kwanini VAT iwe 18% na sio 10 au 12%?
•Kwa nini corporate tax zisiwe 15%?
•Kwa nini withholding tax zisiwe 2-5%?
Kwa ufupi tu, mwishoni mwa miaka ya sitini(late 1960s) nchi za Africa, baada ya 'uhuru' zilijikuta kwenye matatizo - namna gani kukuza uchumi wao na kuongeza mapato. Nchi nyingi zikachagua njia "rahisi" na "fupi" toka kwa Wajamaa - Kodi nyingi na kubwa.
Botswana wao wakachagua njia iliyoonekana "ngumu" na "ndefu" - viwango vidogo/chini vya kodi pamoja na mazingira rafiki ya kufanya biashara.
Kufikia miaka ya themanini wale waliochagua njia 'fupi na rahisi' walikuwa HOI.
Botswana wao walikuwa wanaelekea kwa kasi uchumi wa kati kwa ile njia 'ngumu na ndefu'.
Na bado tumekuwa wazito sana wa kujifunza na kusahihisha makosa yetu; na mahali pengine hatukubali kubadilika kutokana na mahitaji na mazingira ya nyakati zetu.
2. Lazima tuifundishe jamii yetu umuhimu wa kulipa kodi na kupenda kulipa kodi. Utamaduni huo hufundishwa shuleni na majumbani tangu - toka watoto wakiwa wadogo upward.
3. Uwajibikaji na matumizi bora ya hela na mali za umma.
Hata kama tukukisanya trilioni 100 kwa mwaka, kama tabia na "Utamaduni " wa ubadhirifu, wizi, ufisadi, rushwa na matumizi mabovu na ya anasa utaeendelea kama ilivyo sasa - itakuwa ni sawa na kujaza maji kwenye gunia la sukari tu.
Tujenge mutual win-win environments.
Mkitaka, Inawezekana.