Ukichunguza pande zote mbili, TRA na wafanyabiashara, wana hoja kwenye madai yao.
Itumike busara na hekima badala ya nguvu na makali ya Sheria (ambazo nyingine si za haki).
Swali: Kwa nini watu/wafanyabiashara wanakwepa au hawapendi kulipa kodi?
Jibu: Kodi ni nyingi na viwango ni vikubwa.
Solutions:
1. Serikali na TRA (kwa upande mmoja) watunge na kuweka viwango rafiki vya kodi.
•Je Kwanini VAT iwe 18% na sio 10 au 12%?
•Kwa nini corporate tax zisiwe 15%?
•Kwa nini withholding tax zisiwe 2-5%?
Kwa ufupi tu, mwishoni mwa miaka ya sitini(late 1960s) nchi za Africa, baada ya 'uhuru' zilijikuta kwenye matatizo - namna gani kukuza uchumi wao na kuongeza mapato. Nchi nyingi zikachagua njia "rahisi" na "fupi" toka kwa Wajamaa - Kodi nyingi na kubwa.
Botswana wao wakachagua njia iliyoonekana "ngumu" na "ndefu" - viwango vidogo/chini vya kodi pamoja na mazingira rafiki ya kufanya biashara.
Kufikia miaka ya themanini wale waliochagua njia 'fupi na rahisi' walikuwa HOI.
Botswana wao walikuwa wanaelekea kwa kasi uchumi wa kati kwa ile njia 'ngumu na ndefu'.
Na bado tumekuwa wazito sana wa kujifunza na kusahihisha makosa yetu; na mahali pengine hatukubali kubadilika kutokana na mahitaji na mazingira ya nyakati zetu.
2. Lazima tuifundishe jamii yetu umuhimu wa kulipa kodi na kupenda kulipa kodi. Utamaduni huo hufundishwa shuleni na majumbani tangu - toka watoto wakiwa wadogo upward.
3. Uwajibikaji na matumizi bora ya hela na mali za umma.
Hata kama tukukisanya trilioni 100 kwa mwaka, kama tabia na "Utamaduni " wa ubadhirifu, wizi, ufisadi, rushwa na matumizi mabovu na ya anasa utaeendelea kama ilivyo sasa - itakuwa ni sawa na kujaza maji kwenye gunia la sukari tu.
Tujenge mutual win-win environments.
Mkitaka, Inawezekana.