Wafanyabiashara Kariakoo wameiomba serikali iwaondoe raia kigeni (Wachina) wanaofanya umachinga

Wafanyabiashara Kariakoo wameiomba serikali iwaondoe raia kigeni (Wachina) wanaofanya umachinga

Unajua cost of loan kwa China na kwa Tanzania ni tofauti mkuu.

Mtanzania wa kawaida kukopa benki hawezi, mpaka uwe na ardhi iliyopimwa tena potential. Ardhi ikiwa ya 50M wanaikadiria 25M alafu riba, kodi ya mkopo na gharama nyingine lukuki juu. Unaanza kukatwa kabla hujazalisha. Hivyo faida kwa Mtanzania inabidi iwe kubwa kidogo kuliko mgeni mwenye government support kwao.

Meanwhile kuna raia wa kigeni anakuja na mapumbu na makatarasi anapewa mradi wa Mlimani City anakuwa financed na mabenki. Au anatokea Mwarabu anakabidhiwa mradi wa mwendokasi anaitwa mwekezaji ila hapohapo serikali inakopa NMB ikanunue mabasi 100 ambayo italipa yenyewe na mwekezaji ataweka mapumbu tu apate faida akafuge ngamia jangwani.

Bora wapate faida Wahindi na Waarabu wanaoishi bongo kina GSM na Mo Dewji kuliko wapate faida kina Meng Xian wanaotokea Wuah na hawana mpango wa kuwa hata na beki tatu hapa bongo. Kila senti wanairudisha kwao.
Benki za kibongo bila collateral ya maana kama hati ya kiwanja kilicho location nzuri na ndani yake kuna nyumba, apartment, gesti,lodge, hoteli, shule, sheli, kiwanda e.t.c, utazungushwa kama mwehu.
 
Wafanyabiashara Soko la Kariakoo, wameiomba Serikali kuwaondoa raia wa kigeni ambao wamekuwa wakiuza bidhaa rejareja kwa bei ya chini hali inayopelekea raia wa nchini kukosa wateja.

Wakiongea na EATV, wanasema kwa sasa hali imekuwa mbaya zaidi kwani wengine wamekuwa wakisimama nje ya maduka na kuchukua namba za wateja na kuwapeleka kwenye maduka yao.

Soma Pia: Dar: Raia wa China wageuka machinga, Wananchi washitushwa

Source: EATV

My Take: Wafanyabiashara wa Tanzania wana tamaa sana.....wanataka faida kubwa sana.....kitu cha 3,000/= wanaweza kukuuzia 30,000/= Mchina abakie kariakoo tupate nafuu wanunuzi.
mbona rahisi wamachinga wa kariakoo msuse muwakomoe hao wachina nendeni guangzhou
 
Siri ya wachina inabidi ujue historia yao.

China ni nchi ya watu wenye akili nyingi kitambo, kuna majengo yamejengwa miaka 3000 iliyopita mpaka leo wapo.


Kwa nini China kwa sasa ipo vizuri?
Jibu: Deng Xiaoping
Alikuwa "Rais" wa pili wa China,Huyo mzee ndio chanzo cha utajiri wa china. Yaani ni kama zali za mentali kupata kiongozi mjanja kama huyo. Kafatilie historia yake ndio utaelewa.

Ila Mchina ni mwizi wa teknolojia, mjanja sana halafu mchina anafanya kazi kwelikweli


Pia mchina anatafuta jinsi ya kuzalisha kwa bei ndogo mno ili kuvutia dunia nzima kununua vitu kwake. Nguo na viatu, mapochi ni synthetic materials za nguo, ngozi e.t.c


Mchina anapata mkopo kwa masharti nafuu ni rahisi biashara kukua kwa haraka.

Kuanzisha kiwanda china ni bei nafuuu na rahisi sana ndio maana viwanda ni vingi sana.
Kaka unaongelea kukopi technolojia huko mbali sana hata local brand zetu tunaziundermine tunazipiga vita kisa hazina ubora badala ya kuangalia namna ya kuzisuport na kuwajengea uwezo wenzetu waliothubutu kufanya hivyo, kuna siku niliona kwenye taarifa ya habari kakamatwa mwamba moja anakiwanda bubu cha kutengeneza Mafuta ya Mawese nilishangaa sana, unafikiri watengeneza bidhaa feki China serikali yao haiwaoni kuna la kujifunza hapo
 
Kaka unaongelea kukopi technolojia huko mbali sana hata local brand zetu tunaziundermine tunazipiga vita kisa hazina ubora badala ya kuangalia namna ya kuzisuport na kuwajengea uwezo wenzetu waliothubutu kufanya hivyo, kuna siku niliona kwenye taarifa ya habari kakamatwa mwamba moja anakiwanda bubu cha kutengeneza Mafuta ya Mawese nilishangaa sana, unafikiri watengeneza bidhaa feki China serikali yao haiwaoni kuna la kujifunza hapo
Ingekuwa ni nchi nyingine wangemfadhili zaidi ili awe na kiwanda complete cha kutengenezea mafuta ya kula.
 
Ingekuwa ni nchi nyingine wangemfadhili zaidi ili awe na kiwanda complete cha kutengenezea mafuta ya kula.
Ni kweli kabisa kila jambo huzaliwa utambaa, utembea kisha huanza kukimbia sasa sisi tunataka tulukie stage ya kukimbia kabla ya kutambaa, ukiangalia namna tunavyomtafasili Muwekezaji ni yule anakuja na mabilioni hawa wadogo wadogo kwetu ni kama Waharifu tu unafikili mjasiliamali mdogo atasogeaje
 
Hawa Mawinga ndio janga, Sijui kwa nini Serikali inawalea. Au hao machinga wanaouza bidhaa nje ya maduka makubwa sijui kwa nini wanashindwa kuondolewa, Serikali inalalamika walipaji Kodi directly niwatz wasiozidi mil 2 kwenye nchi yenye watu wazima zaidi ya mil 30 . Halafu wanajaza machinga Kila eneo.
Nikipengele hiki mkuu. Mawinga ni waizi kwa ufupi. Wao hawana chao ila ndio wanaharibu bei sokoni na wanajua kuterget wateja wapya ukiwa mwenyewe hawana shida na ww mgeni sasa
 
Sisi sio wachina kwa vitu vingi ila tunaweza kujifunza kwa wachina wamewezaje japo kazi nzito kweli kweli kwa sababu itahusisha mambo mengi

Nikuulize swali umewahi kufanya kazi na wachina ?
Nimefanya kazi nao kabla ya kwenda chuo. Ni wachapakazi ila pia wanapewa support na serikali na wao wenyewe wanapeana support huku.

Casino zinazomilikiwa na Wachina hapa bongo wanaenda Wachina hawaendi za Kihindi, logistics companies za Wachina wanatumia Wachina hawatumii sijui Silent Ocean. CCECC hiyo hapo ni ya serikali inakuja shindana na hawa wazawa wenye mtaji hata 50 billion hawana.

Bila ulinzi hata mabeki tatu watatoka China.
 
Waache ujinga wamachinga wa tz wamejaa tamaa sana acha wawanyooshe tu hakuna namna
 
Habari zenu ndugu

Kwa anaehitaji kutembea/kutalii Zanzibar anitafute

Zanzibar ni njema atakae aje
 
Back
Top Bottom