Kila Mhindi bilionea unayemuona bongo ana uraia Canada au UK huku Tanzania ananyonya tu.
Iddi Amin alipowapa masharti ya kupokea uraia wa Uganda walikataa sababu ni shithole country, ila muda huohuo walikuwa mitaa ya Kampala na Entebbe wanafanya biashara. Akawapa miezi mitatu wahame bila kitu, Wahindi 80,000 wakakimbilia Uingereza chanzo kidogo tu ni mgogoro wa kukataa uraia.
Mchina akiuza mitumba yake anapeleka faida China, huku anabaki na hela ya kula tu. Thamani ya shilingi inaporomoka kila siku, hela inatoka kwenye mzunguko wa bongo inaenda nje.
Ukitoa shilingi 10,000 kununua tshirt ya Mchina, ile tshirt kaichukua kwa 2,000 kwao akaongeza usafiri na kodi maybe 2,000 nyingine faida anakuwa na 6,000. Mbongo akiuza tshirt ileile kwa 12,000 kainunua kwa 3,000 sababu Wachina wanauziana kwa bei ndogo mbongo hawezi nunua kwa 2,000. Na akiongeza 2,000 gharama. Anapata faida ya 7,000.
6,000 faida ya Mchina atatoa kama 1,000 ya matumizi ile 5,000 arudishe China kujenga kiwanda, kuajiri, kujenga makazi, kununua hisa, etc. Wakati ile faida ya 7,000 ya mbongo akitoa matumizi yote na uwekezaji wote ni hapahapa bongo. Ukitoa 10,000 kwa Mchina unajikuta umeondoa 5,000 kwenye mzunguko wa fedha nchini na umeua thamani ya TZS.