Countrywide
JF-Expert Member
- Mar 2, 2015
- 20,694
- 32,527
Wewe unataka kutuchota na uongo.Kiuchumi ni bora wazawa wauze kwa bei kubwa wananchi wa kawaida wataumia ila mwisho wa siku mzunguko wa biashara na hela utabaki nchini na ile faida ya wafanyabiashara itatumika kwenye shughuli nyingine za kiuchumi ndani ya nchi. Haohao wakipata faida kubwa ndio watasaidia wengine, wataajiri, watahonga, watalipa ada, watanunua nyama, watafuga na kulima, watanunua simenti na mbao wajenge.
Ni bora hivyo kuliko Wachina waje na bei ndogo zaidi, waue soko la wazawa na viwanda vya ndani kisha faida yote waipeleke kwao huku wazawa ndani wakibaki vibarua. Singapore ina gharama kubwa za kuishi na sio nchi maskini, Burundi ina gharama ndogo sana za kuishi na biashara zao zinapata faida kidogo mno ila bado ni maskini wa kutupwa.
Namibia wana biashara zina faida na zina bei kuliko sisi ila wana maisha mazuri kutuzidi.
Ni bora mchina auze bei ndogo kuliko mzawa auze Bei juu. Bei juu inachochea inflation, inaangusha sarafu
Uchumi wetu sio wa bei juu, pia hata hao wazawa wakiuza bei juu bado atayefaidika sana ni hao hao wachina na wengine wa nje sababu sisi ni waagizaji wakubwa mno kuliko kuzalisha. Atanunua range ambalo atapeleka pesa nje, atanunua mafuta kila siku ambayo nayo tunatoa nje
Mchina akiuza bei ndogo ni faida kwetu sababu pesa nyingi tutabaki nayo mfukoni hapahapa na pia atasaidia kucontrol inflation