Wafanyabiashara Kariakoo wameiomba serikali iwaondoe raia kigeni (Wachina) wanaofanya umachinga

Wafanyabiashara Kariakoo wameiomba serikali iwaondoe raia kigeni (Wachina) wanaofanya umachinga

Tumia akili japo kidogo, toka lini serikali haijawahi kuwa tatizo?

Serikali ya Ghaddaffi Libwa, kila kitu kilikuwa bue, mpaka mahari za kuon wanapewa na serikali, bado ikaonekana ni tatizo.

Ushindwe wewe uisingizie serikali?
Serikali ya Tanzania nitatizo hasa katika suala la ajira/biashara na uwekezaji. Ndio maana hapo juu umesema ilaumiwe TBS, na mimi nakueleza tatizo sio TBS bali Serikali. TBS uwezo wao uko chini hawana vifaa Bora vya kukagua ubora wa bidhaa ndio maana vifaa feki vimejaa.

Serikali inaruhusu vipi watu ambao work permit yao inawatambua kama wawekezaji waruhusiwe kufanya biashara ya machinga hilo ni tatizo.

Kodi Tanzania zipo nyingi za ajabu ajabu, mfano unalipia OSHA/NEMC/FIRE/TBS/WMA/TRA/WSF . Njia ya mkato nikutoa rushwa Ili ufanikiwe jambo linalokosesha Serikali mapato.
 
Wafanyabiashara Soko la Kariakoo, wameiomba Serikali kuwaondoa raia wa kigeni ambao wamekuwa wakiuza bidhaa rejareja kwa bei ya chini hali inayopelekea raia wa nchini kukosa wateja.

Wakiongea na EATV, wanasema kwa sasa hali imekuwa mbaya zaidi kwani wengine wamekuwa wakisimama nje ya maduka na kuchukua namba za wateja na kuwapeleka kwenye maduka yao.

Soma Pia: Dar: Raia wa China wageuka machinga, Wananchi washitushwa

Source: EATV

My Take: Wafanyabiashara wa Tanzania wana tamaa sana.....wanataka faida kubwa sana.....kitu cha 3,000/= wanaweza kukuuzia 30,000/= Mchina abakie kariakoo tupate nafuu wanunuzi.
Bei rahisi ndiyo vizuri, halafu nijuavyo mimi kwenye upinzani ndiyo kunakuwa na biashara pia ushindani husababisha uboreshaji wa huduma
 
Hawa wa kwetu SI wafanyabiashara hawa ni majangiri Kwa namna bei zao zilivyo.....wanataka faida mara tatu ya bei ya manunuzi ,kiufupi sisi tuna tamaa sana ya kupata kikubwa na Kwa muda mfupi na ni tofauti na misingi ya kibiashara

Hebu angalia hata kwenye usafiri wa kukodisha kabla ya ujio wa hizi taxi mtandao

Wachina wabaki na ikiwezekana waje tuu Kwa wingi Ili kutufundisha biashara na thamani halisi ya tunachokinunua
 
Wafanyabiashara Soko la Kariakoo, wameiomba Serikali kuwaondoa raia wa kigeni ambao wamekuwa wakiuza bidhaa rejareja kwa bei ya chini hali inayopelekea raia wa nchini kukosa wateja.

Wakiongea na EATV, wanasema kwa sasa hali imekuwa mbaya zaidi kwani wengine wamekuwa wakisimama nje ya maduka na kuchukua namba za wateja na kuwapeleka kwenye maduka yao.

Soma Pia: Dar: Raia wa China wageuka machinga, Wananchi washitushwa

Source: EATV

My Take: Wafanyabiashara wa Tanzania wana tamaa sana.....wanataka faida kubwa sana.....kitu cha 3,000/= wanaweza kukuuzia 30,000/= Mchina abakie kariakoo tupate nafuu wanunuzi.
 
Wafanyabiashara Soko la Kariakoo, wameiomba Serikali kuwaondoa raia wa kigeni ambao wamekuwa wakiuza bidhaa rejareja kwa bei ya chini hali inayopelekea raia wa nchini kukosa wateja.

Wakiongea na EATV, wanasema kwa sasa hali imekuwa mbaya zaidi kwani wengine wamekuwa wakisimama nje ya maduka na kuchukua namba za wateja na kuwapeleka kwenye maduka yao.

Soma Pia: Dar: Raia wa China wageuka machinga, Wananchi washitushwa

Source: EATV

My Take: Wafanyabiashara wa Tanzania wana tamaa sana.....wanataka faida kubwa sana.....kitu cha 3,000/= wanaweza kukuuzia 30,000/= Mchina abakie kariakoo tupate nafuu wanunuzi.
Tusipowekeza, kwenye utafiti, uundaji, utengenezaji na kusomesha wataalam wa viwanda, tutakuwa dampo na soko kwa wote duniani. Ataondoka mchina, bado hatuna viwanda vyetu lazima tuende nchi zingine kukusanya kuja kutupia kwetu. Wakati wa Nyerere tulikuwa na viwanda zaidi ya 400 tukaviuwa tukavifanya maghala ya kuhifadhia takataka za nchi zingine.
 
Kiuchumi ni bora wazawa wauze kwa bei kubwa wananchi wa kawaida wataumia ila mwisho wa siku mzunguko wa biashara na hela utabaki nchini na ile faida ya wafanyabiashara itatumika kwenye shughuli nyingine za kiuchumi ndani ya nchi. Haohao wakipata faida kubwa ndio watasaidia wengine, wataajiri, watahonga, watalipa ada, watanunua nyama, watafuga na kulima, watanunua simenti na mbao wajenge.

Ni bora hivyo kuliko Wachina waje na bei ndogo zaidi, waue soko la wazawa na viwanda vya ndani kisha faida yote waipeleke kwao huku wazawa ndani wakibaki vibarua. Singapore ina gharama kubwa za kuishi na sio nchi maskini, Burundi ina gharama ndogo sana za kuishi na biashara zao zinapata faida kidogo mno ila bado ni maskini wa kutupwa.

Namibia wana biashara zina faida na zina bei kuliko sisi ila wana maisha mazuri kutuzidi.
 
Mkiwatimua Kkoo, jiandaeni nanyi kutimuliwa watanzania wanaobangaiza Guangzhou au Yiwu...
 
Kiuchumi ni bora wazawa wauze kwa bei kubwa wananchi wa kawaida wataumia ila mwisho wa siku mzunguko wa biashara na hela utabaki nchini na ile faida ya wafanyabiashara itatumika kwenye shughuli nyingine za kiuchumi ndani ya nchi. Haohao wakipata faida kubwa ndio watasaidia wengine, wataajiri, watahonga, watalipa ada, watanunua nyama, watafuga na kulima, watanunua simenti na mbao wajenge.

Ni bora hivyo kuliko Wachina waje na bei ndogo zaidi, waue soko la wazawa na viwanda vya ndani kisha faida yote waipeleke kwao huku wazawa ndani wakibaki vibarua. Singapore ina gharama kubwa za kuishi na sio nchi maskini, Burundi ina gharama ndogo sana za kuishi na biashara zao zinapata faida kidogo mno ila bado ni maskini wa kutupwa.

Namibia wana biashara zina faida na zina bei kuliko sisi ila wana maisha mazuri kutuzidi.
Kwanini tusiwe na viwanda vyetu tena pamba tunayo bora iwe hivyo ndipo tutapata akili
 
nafurahi sana tena sana kumuona mchina KARIAKOO, kwasababu wafanyabiashara wa kibongo wamezidi UHUNI kwa kupandisha bidhaa BEI kupita kiasi na UWINGA wa hovyo, acha wanyooshwe ili wajifunze kuendana na bei elekezi na nafuu kwa mwananchi wa kawaida.
 
Malighafi ni shida, mfano hebu jaribu kutengeneza sabuni au sukari mwenyewe uone gharama utakayoingia halafu uone mche mmoja au kilo ya sukari utaiuza sh? Lazima bei itakuwa juu.
Upo sahihi mkuu,shida ni gharama za uzalishaji,baada ya kutengeneza bidhaa unakutana na Kodi.
 
Tatizo la Watanzania walio wengi tumezoea kuishi maisha ya kulalamika, kupenda kubebwa bebwa kila mahali, kuishi maisha ya kutaka kujuana sana. Miaka , karne na nyakati imekwenda jamani tuishi maisha ya wakati uliopo. Maisha ya kutaka Monopoly ya kila kitu ufanye mwenyewe yata baki kwako na familia yako huku nje dunia ilisha kuwa ya juhudi zako na uchacharikaji wako kikubwa usivunje sheria.
Leo wafanyabiashara wa kariakoo walisha zoea kuuza vitu bei mara mbili mpaka tatu ya bei halisi wanapo kutana na watu wanao taka kufanya biashara kiuhalisia kulingana na bei halisi wanaona wanaonewa. Maisha ya kuona wao tu wanaweza kufika China etc nakufanya manunuzi ilikuwa zamani, maisha ya kuona wao tu wanaweza panda ndege ni zamani, sasahivi ulimwengu ni kama kijiji mambo ni Digital, business across borders has been made available and easy, biashara janja janja hakuna tena, wafanyabiashara wa Kariakoo wanataka tuaminisha ni wao tu wanafahamu bidhaa zinapo patikana na kuuzwa.
Sasa kwenye Digital Free World biashara imekuwa haina mwenyewe wateja na huduma zimesogezwa kiganjani, pay on delivery imekuwa njia mpya mauzo na biashara, mzigo una nunuliwa China rejareja una uwezo wa kukufikia wewe wa Kigoma. Je ni lini wafanya biashara wa Kariakoo wata acha kulalamika? Je ni lini wafanya biashara wa Kariakoo walidhania wata endelea kutu kandamiza na bidhaa bei juu? Je ni lini wafanya biashara wa Kariakoo wata gundua watu sio wanao weza kuleta mizigo? Je ni lini wafanya biashara wa Kariakoo wata gundua nyakati zimebadilika? Je wafanya biashara wa Kariakoo wanataka kusema bidhaa za hao wa China na wao zina pita bandari na kulipa ushuru tofauti? Wafanya biashara wa Kariakoo bei zao za bidhaa wanatoa wapi?
Asante Mama Samia kwa Kufungua mipaka wacha tule wote tunu ya Taifa hii nchi niya wote hao wa chache wanao sema wanaone kisa wanataka Monopoly the era is long gone, wake up things are no longer at ease. Viwanda ni vingi karne hii na bidhaa ni rahisi acheni kutu nyanyasa wachina pige kazi
 
Back
Top Bottom