Mnavyoona wateja wamewakimbia wanaenda kwa wachina wala hakuna ndumba bali ni bei zao zinavutia, Ili mpambane na wachina punguzeni tamaa ya ganji (faida) kubwa.
Kila leo wachina wanazungumziwa kwenye vyombo vya habari, TUMESHAWASTUKIA !! acheni kuwalipa watangazaji kuwasagia kunguni wachina, mnapoteza muda na pesa.
Yaani mfanyabiashara wa bongo anataka aende China kununua radio elf 10 aje bongo kutupiga elf 50, Tumechoka !! Ukienda kwa mchina sasa, Ahhhhh!! wala hana tamaa, ana subira, atakuuzia maybe elf 15, hata nguvu za kuomba punguzo zinakuisha zaidi ya kutoa shukrani.
Propaganda za wafanyabiashara wa bongo zinashangaza, zimejaa chuki na ubaguzi, Uchumi wa nchi nyingi duniani ni soko huru, wabongo wengi tu wapo China wala hawafanyiwi haya mambo, wakiamua kufungua maduka au viwanda ni ruksa ila ni kujipanga tu kwenye ushindani, wengi wamekuwa mawinga wala hawasemwi lakini kinachoendelea huku ni ubaguzi (Xenophobia)
Uzuri ni kwamba wateja tupo upande wa wachina 😀😀 nchi yetu ni 3rd world country tunawahitaji kutupunguzia ukali wa maisha, Tumechoka kupigwa !!