Wafanyabiashara mnaolipa media kuwachafua wachina mnapoteza muda, Wateja tunawataka wachina

Mchina katumwa hela.., hana mambo mengi
 
Kodi inalipwa na wote
Angalia mizigo wanayouza kama inapitia kwenye EFD
Nionyeshe mmoja tu
 
Hili suala kwa bahati mbaya limebebwa kwa ushabiki, jazba na ujuaji kama ilivyo kawaida ya wabongo.....lakini kiuhalisia hili suala linataka upembuzi yakinifu kutoka kwa wabobezi wa masuala ya kiuchumi ili tupate faida na hasara zake mbele za safari.......

Tunaweza kuona urahisi WA bidhaa lakini ikatugharimu kama nchi mbele ya safari......pamoja na kuwa wafanyabiashara wetu Wana changamoto za tamaa.....lakini suala hili sio la kulibeba kimihemko.....

Ningependa wajuvi wa kiuchumi waje jukwaani watutoe gizani kwenye hili....
 
sasa suala la discount mbona kawaida mzee, Negotiation kwenye biashara ipo me naweza nikawa nauza bidhaa 100000 fixed lakini akaja mteja anaejua kujitetea na na maneno mengi nikamuuzia kwa 70000…. Sio hivyo hata akaja ndugu nikamuuzia kwa hiyohiyo kuna wakati naweza kukubali kumuuzia mtu kwa bei ya hasara kwa kuwa nataka kuingiza mzigo mpya au kwa faida ndogo kwa kuwa amenishawishi au kwa kuwa hali sio rafiki

Faida zinaenda na percent ya mtaji wa mzigo, Mtu hawezi akaimport mzigo kwa mtaji wa milioni alafu akaja kuuza kwa milioni na laki moja lazima auze kwa faida ya kufidia gharama zote pamoja muda

Ningekuelewa kama ungetengeneza hoja ya ziwekwe njia zenye unafuu za kufanya mtanzania asiumizwe katika kuimport bidhaa ili kupunguza gharama kuwa juu.

Wachina wanauza kwa bei nafuu sana kwa kuwa wao ndo wazalishaji wenyewe na wana uzoefu na uwezo wa kuingia ubia na viwanda vya kwao wakatengeneza mzigo mwingi kwa kujua hata kama watapata faida ndogo kwenye kila bidhaa ila zitatoka kwa wingi ila mbongo yeye anaingiza mzigo mdogo kwa kunasia kwa kuwa mtaji na uwezo wa kufanya kwa ukubwa haupo
 
Kwa ufupi ni kwamba mchina anapunguza ukali wa maisha ?
 
Kwa ufupi ni kwamba mchina anapunguza ukali wa maisha ?
Maisha hayapungui ukali maana asilimia kubwa cheap is expensive… Hamna filter watu wanauziwa vitu vyenye ubora chini ya viwango vinavyofanana na uhalisia kwa sababu ubora kwao sio issue bali gharama
 
Watanzania tunauana. Jana nilinunua Drum ya wino kwa Tsh 1.1M wakati leo nikiangalia Alibaba ni USD 53 ambayo ni TSh
53×2,730
=144,690
Hivi hii ni sawa? Tunauana tu! Set nzima ni $212 ambayo ni
212×2,730
=578,760 yeye ananiuzia piece moja 1.1m

Ushahidi
DR711
use for bizhub C654/C654E/C754/C754E/754E
K $53/PCS
C $53/PCS
M $53/PCS
Y $53/PCS
 
Watz tatizo letu kubwa ni ujinga...hujaelewa mantiki ya kinachoongelewa itakuwa.
Yan tunaua uchumi wetu kisa ww uuziwe Radio bei chee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…