Wafanyabiashara ni wengi kuliko waajiriwa lakini watanzania wanaoishi angalau maisha standard waajiriwa ni wengi, Tuendelee kuponda ajira?

Kuna mkinga mmoja namfahamu ni ana Bora umwambie. 😀
Kuna jamaa mmoja ni rafiki yangu, yeye ni mkinga ana hela za kutosha tu, anamiliki nyumba 3, semi 2, canter 4 na hardware 2 kushusha mifuko elfu 1 ya cement ni kawaida sana...

Lakini ana watoto wake wanaosoma st kayumba nilivyomuuliza kwa nini alicheka sana akisema "yeye anaamini kwamba hata wakisoma shule za gharama bado wataishia kugombania ajira hizo hizo za mshahara wa laki 7+... 😁😁
 
Kwa kuongezea kuna dogo mmoja tulisoma wote enzi hzo baba yake alikuwa mfanyabiashara mkubwa tu, dogo alikuwa kwenye hzi shule za st kunani ghafla mambo yakayumba akarudi kuliunga na sisi kwenye kidumu na mfagio😀.

Sisi tukawa tunamdhihaki sana tukidhani tupo sawa nae, kumbe mshua wake anamuandalia mipango ya mbeleni, Dogo kumaliza tu chuo sio mwenzetu hata kidogo alitupiga gepu kubwa sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…