Wafanyabiashara Soko la Ndizi Mabibo: Rais Samia tunaomba tusaidie tupate hati ili soko lijengwe

Wafanyabiashara Soko la Ndizi Mabibo: Rais Samia tunaomba tusaidie tupate hati ili soko lijengwe

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Akielezea hali ya mazingira yalivyo katika Juma Idris Chombo ambaye ni Makamu Mwenyekiti Soko la Mabibo Dar es Salaam anaelezea:

Makusanyo ya Tozo tunayokusanya hapa ni shilingi miamia, tunakusanya kwa ajili ya huduma tu kama vile usafi na ulinzi, kwa kiwango hicho hatuwezi kujenga soko la bilioni 30.

Mabanda yetu mengi yamekufa, mifereji imeziba na fedha nyingine tunajikusanya wenyewe.

Mkurugenzi haji na hatupi ushirikiano mpaka imefika hatua tukatuma maomba katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya atukutanishe na Mkurugenzi lakini halijafanikiwa.

Hatupati ushirikiano wowote kutoka kwake lakini kuna siku alienda Bungeni kwenye Kamati ya Bunge akasema licha ya kuwa hakusanyi fedha kutoka hapa lakini anatoa fedha zake mfukoni kwa ajili ya kuzoa taka jambo ambalo ni uwongo.

Mkurugenzi anaitwa Beatrice amekusanya Tozo sokoni kwa miaka minne bila kufanya chochote, tangu 2016 hadi 2020 alikusanya tozo ila hakufanya chochote.

Historia kwa ufupi ya hili soko lilikuwa ni eneo la Kiwanda cha Urafiki na mpaka sasa hati haijatolewa rasmi.

Namna gani linaendeshwa, hati gani ipatikane hilo suala bado lina utata, hivyo bado ni soko la Wananchi lakini halina hati rasmi.

Wakati wa Utawala wa Rais Magufuli alilitoa eneo hili kuwa soko kwa Wananchi, alitoa kauli hiyo Oktoba 13, 2020 na ndiyo siku hiyo Manispaa wakaondoka hapa kwa kuwa walikuwa wanakusanya fedha huku hawafanyi chochote.

Serikali kupitia kwa Rais ilitamka kuwa imerudisha soko kwa Wananchi, tunaiomba irudishe kwa Wananchi kwa kuwa Taasisi mbalimbali zenye uwezo wa kujenga soko la kisasa zipo lakini haziwezi kuchukua hatua kama kuna vitu havipo sawa kama hivyo.

Tunaamini Rais Samia kwa namna alivyo na mapenzi ya Wananchi wake wa hali ya chini anao uwezo wa kutujengea soko zuri, kilichobaki ni hati ya eneo hilo ipatikane.

Tunaomba Rais atusaidie tupate hati, ili soko lijegwe. Soko linahudumia watu wengi.

Kuna malalamiko mengi yanayoendelea kuhusiana na uchakavu na mazingira ya soko hili ambayo hata sisi tunaona kuna hoja za msingi.

Sasa hivi Wafanyabiashara tunajikusanya kidogo kidogo tunajenga.. Hadi sasa kuna sehemu kadhaa tumejenga kwa muda mfupi.

Kuna wafanyabiashara wengi wa kipato cha chini na wote tunamtegemea Rais Samia katika kutuwezesha kulimaliza hili suala.

Uchaguzi 2020 - Rais Magufuli asema soko la Mabibo, maarufu kama Mahakama ya Ndizi kumilikiwa na wananchi
 
Back
Top Bottom