Nimesima baadhi ya comments hapa halika Watanzania tunatakiwa kuwa na kiongozi mwenye maamuzi magumu hasa, yaani HASA.
Kwanza mtoa mada kagusia wafanyabiashara kama tu sehemu ya stendi ila wale si muhomu sana kwa sasa.
Ila muhimu ni matumizi ya stendi, hapo juzi tu 2000yr stendi zilikuwa tatu, ubungo, mnazi mmoja na kisutu ila Scandinavian Express alikuwa na ofisi yake pale kamata, ubungo ilikuwa stendi kuu na kuna mabasi ya mhindi yakiitwa Royal alikuwa anapakilia upanda, kisutu.
Kuna Taqwa na Tawaqal masafa marefu hawa walikuwa kule ilala, sharif shamba, mnazi mmoja na Magomeni mapipa.
Lakini mabasi yote hayo yalikuwa lazima yapitie kutoka au kuingia ubungo kwa sababi ndiyo ilikuwa Main Bus Terminal kwa jiji la Dar Es Salaam.
Baada ya kuonekana vurugu katikati ya mji ndipo serikali ikasitisha mabasi makubwa yote kuingia katikati ya mji ziishie ubungo na ilikuwa hivyo.
Na hata hii ya Magufuri Bus Terminal ni katika kupanua huduma na msongamano wa kila mtu kuwa na ofisi yake imetokana na kadhia ya vurugu mjini.
Binafsi naona ni jambo jema sana mabasi yote yaanzie pale JPM-BT Mbezi kwa sababu iliyolengwa.
Ukiwa nchini Kenya jijini Nairobi au hata mliofika Afrika ya kusini mnaweza kuelewa ukitaka kusafiri ndipo unaweza kuona umuhimu wa stendi moja ila kwa ambaye hajasafiri anaona ni ujuha.
Kuna watu hapa wanapiga kelele mkoa wa Arusha kukosa stendi, kwa nini kila bus lisipakie eneo lake, yaani watawanyike kila mtaa how come mnataka stendi ya kisasa?.
Sheria zichukue mkondo, mfano pale shekilango hadi manzese ni vurugu tu kwa mabasi makubwa, zile ni nyumba za kuishi watu ila leo mmegeuza ofisi na stendi za mabasi HOW?.