Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Ila nchi hii ina viongozi wa ajabu sana, hapo unakuta waziri anayehusika kwa kushirikiana na timu Msoga, kwakua tu stendi ina jina la Magufuli, basi kubadilisha jina, ikashindikana baada ya mchezo wao kuwekwa mitandaoni.

Wameona waje na mbinu ya kutofanya ulazima kwa wamiliki wa ma bus kuhakikisha wanashushia abiria na mizigo yao pale stendi...... Ili stendi ijifie yenyewe taratibu..... Jambo la aibu na linalopaswa kukemewa na jambo hili linaendelea kuonyesha kwa namna gani nchi hii inaongozwa wajinga waliopewa nafasi. Hivi JPM angekua hai, kuna mmiliki wa ma bus angeivimbia serikali namna hiii??.

Alafu hapo kuna dola, dola hiii hiii tunayosema kila siku iko mafunzoni kuhakikisha jicho lake linamulika kwa masilahi mapana ya taifa. Nadhani moja ya sehemu inayoitaji kufumuliwa ni mfumo mzima wa dola, umejaa wapigania matumbo tu .

Enyi wavivu, wazembe, wala rushwa na mafisadi wakubwa, jina la John pombe Magufuli, hili halitakaa kufutika mioyoni wa taifa hili, historia itayasahau majina yenu pale tu mtakapokufa, lakini haitokaa kumsahau JPM.
Vile vizimba viliuzwe kwa Bei kubwa sana kama vile ni Fremu ya Dubai Airpot pale.
 
Enyi wavivu, wazembe, wala rushwa na mafisadi wakubwa, jina la John pombe Magufuli, hili halitakaa kufutika mioyoni wa taifa hili, historia itayasahau majina yenu pale tu mtakapokufa, lakini haitokaa kumsahau JPM.
Angalia hili sukuma gang lilivyofura! Mungu wa Chato kafa. Kaa kwa kutulia.

Uchaguzi ujao hata wabunge wa maeneo yenu watatoka huku mjini. Anatumwa mtu kuja kuvuta fomu huko, kura za maoni hata akiwa wa mwisho anapitishwa na watoto wa mjini kuwa mgombea. Halafu atatangzwa kwa nguvu ya dola.

Sukuma gang mwafwa!
 
Kwa hiyo na ndege zifuate abiria walipo? Kuna haja gani ya kutumia pesa nyingi kujenga stendi??
NB: Arusha mbaki na stendi yenu maana tumeona hazina umhimu.
Utafiti gani ulifanyika kabla ya kuijenga hio stendi ? Kufanya mambo kwa pupa hakuwezi kuleta faida. Unajenga SGR kwenda Mwanza wakati makontena mengi yanayoingia bandarini yanaelekea Congo na Zambia. Reli zilianza kujengwa kusafirisha watu au bidhaa ?Kuna maamuzi siasa inabidi iwekwe pembeni.
 
Siku zote biashara haitakiwi kutegemea Stendi, bali stendi ndio inapaswa kutegemea biashara yako, shida ni hawa wafanyabiashara walidanganywa na ccm

Nimepita hapo stendi zaidi ya mara 50 lakini sikuwahi kununua chochote, hii ni kwa sababu si lazima abiria kununua kitu hapo stendi, sasa wanacholilia ni nini?
images.jpeg-90.jpg
 
Ila nchi hii ina viongozi wa ajabu sana, hapo unakuta waziri anayehusika kwa kushirikiana na timu Msoga, kwakua tu stendi ina jina la Magufuli, basi kubadilisha jina, ikashindikana baada ya mchezo wao kuwekwa mitandaoni.

Wameona waje na mbinu ya kutofanya ulazima kwa wamiliki wa ma bus kuhakikisha wanashushia abiria na mizigo yao pale stendi...... Ili stendi ijifie yenyewe taratibu..... Jambo la aibu na linalopaswa kukemewa na jambo hili linaendelea kuonyesha kwa namna gani nchi hii inaongozwa wajinga waliopewa nafasi. Hivi JPM angekua hai, kuna mmiliki wa ma bus angeivimbia serikali namna hiii??.

Alafu hapo kuna dola, dola hiii hiii tunayosema kila siku iko mafunzoni kuhakikisha jicho lake linamulika kwa masilahi mapana ya taifa. Nadhani moja ya sehemu inayoitaji kufumuliwa ni mfumo mzima wa dola, umejaa wapigania matumbo tu .

Enyi wavivu, wazembe, wala rushwa na mafisadi wakubwa, jina la John pombe Magufuli, hili halitakaa kufutika mioyoni wa taifa hili, historia itayasahau majina yenu pale tu mtakapokufa, lakini haitokaa kumsahau JPM.
Mzee jiongeze ili biashara yako iende lakini sio kulazimisha mabasi yote yashushe magufuli
 
Utaratibu ni ustaarabu, wafuate utaratibu ma bus yote yapakie na kushusha abiria ndani ya stand ya ma bus na siyo vinginevyo. Kila siku tunalalamikia teuzi za rais, ni kwa sababu ya upuuzi kama huu.

Mkuu wa mkoa yupo, Mkuu wa wilaya yupo, Mkurugenzi yupo, afisa biashara wa mkoa na wilaya wapo, wachumi wa mkoa na wilaya wapo, Askari polisi na askari wa usalama barabarani wapo, kwanini bus lipakie abiria nje au kushusha abiria nje ya stand iliyojengwa kwa madhumuni hayo?

Wahusika wasimamie au watumbuliwe waje wengine wenye nia na kazi hizo.

Hapo nyuma tulilalamikia ndege binafsi kutua kila mahali biula taarifa wala ukaguzi, viwanja vya ndege vimepanuliwa na mamlaka husika walisimamia hili, bandari bubu zilizokuwa zikiingiza vitu vya magendo kama sukari na bidhaa zingine, tulilalamika mamlaka zikashughulikia, sasa kwanini hawa wa mamlaka za usafirishaji wasishughulikie hili la buses na abiria?

Tusipende vitu vya shaghalabaghala, tujenge tabia za kufuata taratibu sisi wenyewe, tunaposhindwa mamlaka husika zisimamie turudi kwenye mstari ndiyo majukumu yao. Na kama waliopewa dhamana hizo wameshindwa na watumbuliwe tu.

Na kama hii ndiyo sababu ya kutumbua watu basi atumbue asubui na jioni na ikiwezekana kila siku mpaka tupate watendaji wanaoelewa majukumu yao.

Nchi zilizoendelea zinatushinda kwasababu wao raia wao kwanza wanapenda utaratibu, na mamlaka zao zina enforce sheria zilizowekwa. Kama ni kutupa uchafu kwenye ndoo wote watatupa uchafu kwenye ndoo, na atakayefanya tofauti anachukuliwa hatua, hapa kwetu watu wanatetea ujinga.

Stand imejengwa kwa madhumuni gani, ikiwa kila mtu atafanya anavyopenda? Miafrika tuone aibu, hivi ni vitu vidogo tujielekeze wenyewe, tusisubiri kusukumwa.

Vijana wanakimbilia south Afrika na Ulaya, au Amerika kupata fursa, sasa bila utaratibu huku nani angeenda?

Nasi tujifunze matumizi mazuri ya akili na vitu , Stand ya bus, ma bus yote yangie stand, na abiria wote washukie stand na kupanda ma bus stand, kama ilivyo kwa ndege, habiria hupanda na kushukia airport na buses iwe hivyo.

Tuache hizi tabia tuendelee.
Mzee tafuta location nyingine pale ni stand ya abiria na sio soko
 
Angalia hili sukuma gang lilivyofura! Mungu wa Chato kafa. Kaa kwa kutulia.

Uchaguzi ujao hata wabunge wa maeneo yenu watatoka huku mjini. Anatumwa mtu kuja kuvuta fomu huko, kura za maoni hata akiwa wa mwisho anapitishwa na watoto wa mjini kuwa mgombea. Halafu atatangzwa kwa nguvu ya dola.

Sukuma gang mwafwa!
Mwenye huo uwezo alikuwa JPM tu
 
Nami nimesema ni stand ya Bus, na sikusema liwe soko. Walioweka masoko ndio waliharibu, ila kuna bidhaa ndogo ndogo zikiwa bus stand siyo mbaya. kama maji ya kunywa, toilet paper, pipi , soda na kadhalika.
Hapana pale hapatakiwi kuuzwa chochote zaidi ya ticket ndo maana Leo mnataka watu wapate shida kisa wewe uuze maji na tissue
 
Hapana pale hapatakiwi kuuzwa chochote zaidi ya ticket ndo maana Leo mnataka watu wapate shida kisa wewe uuze maji na tissue
Kama kuna watu kunahitajika huduma muhimu, kama maji,soda na tissue paper. Huwezi kuwa na stand ukose huduma kwa wasafiri. Yani wajenge majengo ya abiria, waache kujenga vyoo, na wasiweke maeneo ya kutupa taka, au vinywaji baridi.
 
Binafsi nashauri hi!! Bus lazima ipite stendi husika, then inaweza kuendelea na ruti za ofsini kwake. Kutokupita kabisa si suala la kushabikia, huko ni kutumia pesa za watanzania ovyo. Na vitu kama stendi vinawapa ajira watanzania wengi sasa mkigeuza kuwa magofu wale walioko pale wakaibe??
Mfano kashusha abiria wote pale stendi anafuata Nini? Kama ni Kodi za serikali tayari ziko kwenye tiketi serikali imeshapata Kodi zake za abiria waliokata tiketi

Serikali inapungukiwa Nini? Kama ushuru wa kuingia stendi basi wawambie tu wenye mabasi wawalipe hata Kwa mwezi watawalipa hawana shida badala ya kupoteza muda kuwa basi lazima liingie upate ushuru ni kuwaambia tu mabasi yote ya mikoa yanayoanzia Dar lazima yalipe ushuru wa stendi ya Magufuli watalipa na kukiwa na abiria watapita hapo wawachukue au kushusha lakini ushuru ulishaingia.
 
Acheni ujinga. Mimi Ni mhaya, kila Mara nasafiri kwenda kwetu (usiniulize nakwenda kufanya Nini)
Hapa Dar naishi Ubungo national housing. Unataka kuniambia nikifika Mbezi saa Saba usiku niliache Basi nililokuja nalo liende tupu urafiki, Mimi na mikungu yangu ya ndizi Bukoba na suitcase yangu ya pesa nyingi nianze kutafuta Bajaj au nisubiri kukuche nipande mwendo Kasi? What type of reasoning is that?
Mwenye Basi amekubali kunipeleka urafiki bure, hata anaye fikiria kutumia sehemu ya haja kubwa hawezi kuwacha Basi liende tupu kisa apande mwendokasi.
Mara moja moja watanzania mu reason kutumia vichwa, tigo kazi yake Ni kupitishia mavi sio kufikiria.
 
Back
Top Bottom