Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Tena haitakiwi iitwe stend kuu ya mabasi.
Inatakiwa iitwa stendi ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Kisha pawe na stand za Wilaya za aKinondoni,Ilala,Temeke na Kigamboni.
Yote ni kutanua wigo wa mapato na kuwapelekea huduma wananchi wanyonge.

Walitakiwa wajiuze palikua na sababu gani kujenga stend ya mkoa wa Pwani Kibaha halafu ya mkoa wa Dsm ijegwe Mita cha kutoka kibaha. Kwa nini stand ya mkoa wa Pwani isingejengee hata Kongowe au Mlandizi?
Sahihi kabisa.
 
Kwa hiyo na wenye lodge sasa nao waanze kulalamika bus kuruhusiwa kusafiri usiku imeharibu biashara na hizo blah blah nyingine ooh serikali sijui inakosa mapato??
Sio kila kinachokujia kichwani unaandika, kaangalie nilichoandika uje tujadili, wapi nimesema guest house? Niliongelea na kusisitiza kufanya biashara hiyo kwa utaratibu.

Stand ya bus imejengwa, lakini kuna watu badala ya kupakia na kushusha abiria ndani ya stand wanaanzisha vituo vya nje, kushusha na kupakia, hiyo siyo sawa.

Ndio maana nikauliza stand ilikuwa na haja gani kama kila mtu ataamua kushusha na kupakia popote? Hao watoa huduma hunufaika tu pale mteja anapolazimika kutumia huduma zao, hakuna mtu analazimishwa kutumia huduma yoyote ndani ya stand ya buses. Ila utaratibu ni ustaarabu, nini kinawafanya wasishushe abiria ndani ya stand au kupakia ndani ya stand maalum, badala yake kupandisha na kushusha abiria, Urafiki au vituo visivyo rasmi?
Unanishambulia lakini sijui hata kama unaelewa mantiki ya hoja yangu.

Anyway, fikiri utakavyo hayo yalikuwa mawazo yangu.
 
Mbona ndege huwa hamuombi mshushwe kwenu mnakubali kwenda airport? Utaratibu wa vituo ni muhimu sana, mkifanya shaghala baghala msilalamikie mfumo na utaratibu wa serikali.

Sasa Stand ya bus ya nini kama unaweza panda na kushuka popote?
Pia sijawahi kuona kwenye ndege wamachinga wanazungukazunguka kwenye madirisha kuuza karanga na maji au ndege inasimama ili watu kujisaidia njiani na kula.
 
Acha kukariri ujinga, Dar es Salaam nzima ya watu zaidi ya milioni tano haiwezi kuwa na kituo kimoja tu cha bus za mikoani. Mtu ametoka Lindi na anaishi Mbagala aje kushushiwa Mbezi! Huo utakuwa ujinga wa karne
Ok sasa kila abiria atashushwa anapoishi Dar es Salaam hii?! mhmm haya ngoja nikae na ujinga wangu.
 
Stand ya bus imejengwa, lakini kuna watu badala ya kupakia na kushusha abiria ndani ya stand wanaanzisha vituo vya nje, kushusha na kupakia, hiyo siyo sawa.

Ndio maana nikauliza stand ilikuwa na haja gani kama kila mtu ataamua kushusha na kupakia popote?
Kama naenda ubungo na bus linaelekea huko wakienda na mimi chukulia kama bus limenipa lift ili roho yako mbaya iridhike.
 
Tena haitakiwi iitwe stend kuu ya mabasi.
Inatakiwa iitwa stendi ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Kisha pawe na stand za Wilaya za aKinondoni,Ilala,Temeke na Kigamboni.
Yote ni kutanua wigo wa mapato na kuwapelekea huduma wananchi wanyonge.

Walitakiwa wajiuze palikua na sababu gani kujenga stend ya mkoa wa Pwani Kibaha halafu ya mkoa wa Dsm ijegwe Mita cha kutoka kibaha. Kwa nini stand ya mkoa wa Pwani isingejengee hata Kongowe au Mlandizi?
Na mikoa karibia yote kila wilaya ina stendi yake, Dar es Salaam ilipaswa kila wilaya kuwa na stendi hata tatu.
 
Labda hukuelewa. Stand ni ya bus na abiria, lakini baadhi ya wenye ma bus wanapakia abiria nje na kushusha abiria nje ya stand, hiyo siyo sawa. Washushe abiria ndani na wapakie abiria ndani ya stand.

Tusifanye mambo shaghalabaghala kwa kigezo cha kuwakimbia wafanya biashara. Wanapokuwa hawatumii stand hata serikali inakosa mapato.

Swala la abiria kupata mahitaji yao ndani ya stand siyo lazima lakini ikitokea anahitaji huduma hiyo ndani ya stand, iwepo, na ipo. Sio kwamba wafanya biashara wanalazimisha abiria kutumia huduma zao, hapana.

Habiria halazimishwi kutumia choo cha kulipia kama hahitaji huduma ya choo, halazimishwi kununua maji kama hayahitaji. Ilia ikiwa atahitaji zitakuwepo na atalipia, na itakuwa fursa kwa wenye biashara hizo.

Sijui kama umeelewa?
Kama abiria hajalalamika kushushwa nje ya standa na msafirishaji hajalalamika kwanini wewe muuza biscuits stand ulalamike?

Kuhusu mapato kwani mabasi hayalipi ushuru wa stand na manispaa zimelalamika kukosa mapato?
 
Mabasi hayakwepi stendi ya Mkoa, mabasi karibia yote huwa lazima yanapita hapo kuchukua au kushusha abira, hao vilaza walioshindwa kufikria njia nyingine za kuishi zaidi ya kuchuuza bidha stand wanachotaka ni kwamba mabasi yote ya Dar yaanzie na kuishia hapo stendi tu.
na kwa nini mabasi yanakwepa kuanzia na kuishia hapo stendi tu ?
 
Kama abiria hajalalamika kushushwa nje ya standa na msafirishaji hajalalamika kwanini wewe muuza biscuits stand ulalamike?

Kuhusu mapato kwani mabasi hayalipi ushuru wa stand na manispaa zimelalamika kukosa mapato?
Yakipaki nje hayalipi, na sio utaratibu. Abiria wanatakiwa kupanda na kushuka ndani ya bus stand terminal.
 
Hizo data umeziotoa wapi harafu unajua kuwa ile ni stand na sio packing ya mabus?
 
Ila nchi hii ina viongozi wa ajabu sana, hapo unakuta waziri anayehusika kwa kushirikiana na timu Msoga, kwakua tu stendi ina jina la Magufuli, basi kubadilisha jina, ikashindikana baada ya mchezo wao kuwekwa mitandaoni.

Wameona waje na mbinu ya kutofanya ulazima kwa wamiliki wa ma bus kuhakikisha wanashushia abiria na mizigo yao pale stendi...... Ili stendi ijifie yenyewe taratibu..... Jambo la aibu na linalopaswa kukemewa na jambo hili linaendelea kuonyesha kwa namna gani nchi hii inaongozwa wajinga waliopewa nafasi. Hivi JPM angekua hai, kuna mmiliki wa ma bus angeivimbia serikali namna hiii??.

Alafu hapo kuna dola, dola hiii hiii tunayosema kila siku iko mafunzoni kuhakikisha jicho lake linamulika kwa masilahi mapana ya taifa. Nadhani moja ya sehemu inayoitaji kufumuliwa ni mfumo mzima wa dola, umejaa wapigania matumbo tu .

Enyi wavivu, wazembe, wala rushwa na mafisadi wakubwa, jina la John pombe Magufuli, hili halitakaa kufutika mioyoni wa taifa hili, historia itayasahau majina yenu pale tu mtakapokufa, lakini haitokaa kumsahau JPM.
Watafute kazi ya kufanya au wahamie masokoni
 
Mbona ndege huwa hamuombi mshushwe kwenu mnakubali kwenda airport? Utaratibu wa vituo ni muhimu sana, mkifanya shaghala baghala msilalamikie mfumo na utaratibu wa serikali.
Tatizo ndege Haina barabara ya kufika abiria mitaani walipo usilinganishe na mabasi

Jengeni barabara za ndege zofike Hadi mitaani hatutaenda airport? Tufuate Nini Airport Tutapandia ndege Manzese Kwa Bi Kitumbo bila shida yeyote
 
Hao wajinga kweli, yani wanalazima abiria kushuka hapo wateseke ili wanunue tu crisps na maji yao, wengine wazee kabisa lakini hawana akili hata kidogo wamekimbia kulima kwao Tukuyu wamekuja Mbezi kugombea mia mbili mbili za abira.
Hahaaaaaa, unatuvunjia heshima watu wa Tukuyu bro. Tuombe radhi.
 
Back
Top Bottom