Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Ok sasa kila abiria atashushwa anapoishi Dar es Salaam hii?! mhmm haya ngoja nikae na ujinga wangu.
Ndio mtu ashushwe kwenye wilaya yake anapoishi

Mtu anaishi wilaya ya Kinondoni basi linatoka Moshi au Arusha linapita wilaya ya Kinondoni anapoishi liende likamshushe wilaya ya ubungo halafu aanze kutafuta Usafiri wa kutoka wilaya ya ubungo arudi nyuma kwake wilaya ya Kinondoni huo ni ujinga wa kiwango Cha lami
 
Bro naomba nitofautiane nawe kidogo. Jifikirie wewe ni abiria unaishi Upanga. Huna gari unategemea mwendokasi au daladala. Gari inaofisi tuseme Kigogo au Mnazi mmoja. Inakuja inakuacha Magufuli halafu wewe utafute usafiri kwenda Upanga.

Hapo hapo yenyewe inaenda tupu mpaka Mnazi mmoja. Ukitoka hapo stendi na mabegi yako mara uburute, ukabwe na kudondoka. Huu ni ukiritimba mkubwa mno. Au uneshafika level za kutembelea V8 linalowekwa mafuta na wananchi? Eti Daktari maana duh!
Acha taralira zako ndugu. Na treni na ndege unasemaje?
 
Mbona ndege huwa hamuombi mshushwe kwenu mnakubali kwenda airport? Utaratibu wa vituo ni muhimu sana, mkifanya shaghala baghala msilalamikie mfumo na utaratibu wa serikali.

Sasa Stand ya bus ya nini kama unaweza panda na kushuka popote?
Acha kufananisha abiria wa ndege nawa kwenye bus abiria wengi wapanda ndege wana vipato vizuri ndo maana wanakodi magari au kuja na magaria yao ila abiria wengi wa ma bus vipato vyetu ni vya kawaida sana, Kingine airport ni sehemu salama sio pale magufuri pamejaa wezi na matapeli.
 
Ila nchi hii ina viongozi wa ajabu sana, hapo unakuta waziri anayehusika kwa kushirikiana na timu Msoga, kwakua tu stendi ina jina la Magufuli, basi kubadilisha jina, ikashindikana baada ya mchezo wao kuwekwa mitandaoni.

Wameona waje na mbinu ya kutofanya ulazima kwa wamiliki wa ma bus kuhakikisha wanashushia abiria na mizigo yao pale stendi...... Ili stendi ijifie yenyewe taratibu..... Jambo la aibu na linalopaswa kukemewa na jambo hili linaendelea kuonyesha kwa namna gani nchi hii inaongozwa wajinga waliopewa nafasi. Hivi JPM angekua hai, kuna mmiliki wa ma bus angeivimbia serikali namna hiii??.

Alafu hapo kuna dola, dola hiii hiii tunayosema kila siku iko mafunzoni kuhakikisha jicho lake linamulika kwa masilahi mapana ya taifa. Nadhani moja ya sehemu inayoitaji kufumuliwa ni mfumo mzima wa dola, umejaa wapigania matumbo tu .

Enyi wavivu, wazembe, wala rushwa na mafisadi wakubwa, jina la John pombe Magufuli, hili halitakaa kufutika mioyoni wa taifa hili, historia itayasahau majina yenu pale tu mtakapokufa, lakini haitokaa kumsahau JPM.
Ujinga mtupu let nature work, huwezi kumlazimisha abiria kununua bidhaa, semeni mnataka bajaji na daladala zenu zipige pesa kama mnavyotoza abiria kiingilio cha stand wakati wana ticket, wizi mtupu
 
Kwani hapo mbezi hakuna watu wanaoishi hapo?
Hao ndio watapanda na kushuka hapo stendi kuu.
Au hakuna watu wanaosafiri wanaoishi Mbezi ?
Yaani basi la lindi limpitishe abiria nyumbani kwake Vikindu, na likamshushe Mbezi ilimradi tu anunue maji na tishu
Halafu aanze kutafuta usafiri mwingine wa kurudi Vikindu.

Kama hapo mbezi hakuna abiria wanaoishi hapo, basi aliyejenga hiyo stendi alikuwa mwehu.
 
Mbona ndege huwa hamuombi mshushwe kwenu mnakubali kwenda airport? Utaratibu wa vituo ni muhimu sana, mkifanya shaghala baghala msilalamikie mfumo na utaratibu wa serikali.

Sasa Stand ya bus ya nini kama unaweza panda na kushuka popote?
Mfano wa ndege ni irrelevant.
 
kurasa zote nimesoma sijaona aliyeongelea sababu za mabasi kukwepa stendi ya mkoa
Kwenye soko huru na lenye ushindani, huwezi kulazimisha washindani wa kibiashara wafanye biashara kwa mbinu moja. Ndio maana stendi zipo nyingi, Kigamboni, magomeni, Urafiki, chanika etc. kulazimisha stendi iwe mmoja ni impracticable.
 
Bro naomba nitofautiane nawe kidogo. Jifikirie wewe ni abiria unaishi Upanga. Huna gari unategemea mwendokasi au daladala. Gari inaofisi tuseme Kigogo au Mnazi mmoja. Inakuja inakuacha Magufuli halafu wewe utafute usafiri kwenda Upanga.

Hapo hapo yenyewe inaenda tupu mpaka Mnazi mmoja. Ukitoka hapo stendi na mabegi yako mara uburute, ukabwe na kudondoka. Huu ni ukiritimba mkubwa mno. Au uneshafika level za kutembelea V8 linalowekwa mafuta na wananchi? Eti Daktari maana duh!
1. Kwani mtu anayeshuka uwanja wa ndege na anakaa Kunduchi huwa anafikaje nyumbani...?

2.Kwanini gari ziende Shekilango au Mnazi mmoja .....?
 
Ila nchi hii ina viongozi wa ajabu sana, hapo unakuta waziri anayehusika kwa kushirikiana na timu Msoga, kwakua tu stendi ina jina la Magufuli, basi kubadilisha jina, ikashindikana baada ya mchezo wao kuwekwa mitandaoni.

Wameona waje na mbinu ya kutofanya ulazima kwa wamiliki wa ma bus kuhakikisha wanashushia abiria na mizigo yao pale stendi...... Ili stendi ijifie yenyewe taratibu..... Jambo la aibu na linalopaswa kukemewa na jambo hili linaendelea kuonyesha kwa namna gani nchi hii inaongozwa wajinga waliopewa nafasi. Hivi JPM angekua hai, kuna mmiliki wa ma bus angeivimbia serikali namna hiii??.

Alafu hapo kuna dola, dola hiii hiii tunayosema kila siku iko mafunzoni kuhakikisha jicho lake linamulika kwa masilahi mapana ya taifa. Nadhani moja ya sehemu inayoitaji kufumuliwa ni mfumo mzima wa dola, umejaa wapigania matumbo tu .

Enyi wavivu, wazembe, wala rushwa na mafisadi wakubwa, jina la John pombe Magufuli, hili halitakaa kufutika mioyoni wa taifa hili, historia itayasahau majina yenu pale tu mtakapokufa, lakini haitokaa kumsahau JPM.
Huu ni upumbavu wanawalipia nauli ,wajinga kweli hawa
 
Kwenye soko huru na lenye ushindani, huwezi kulazimisha washindani wa kibiashara wafanye biashara kwa mbinu moja. Ndio maana stendi zipo nyingi, Kigamboni, magomeni, Urafiki, chanika etc. kulazimisha stendi iwe mmoja ni impracticable.
Miundombinu ya usafiri mkubwa na uchukuzi(Uwanja wa ndege, stendi za Mabasi,Bandari kavu)huwa inatakiwa iwe nje kidogo ya mji....ili
  • kuondoa msongamano wa magari barabarani...
  • Kupunguza uharibifu wa barabara za ndani ya mji
 
Siku zote biashara haitakiwi kutegemea Stendi, bali stendi ndio inapaswa kutegemea biashara yako, shida ni hawa wafanyabiashara walidanganywa na ccm

Nimepita hapo stendi zaidi ya mara 50 lakini sikuwahi kununua chochote, hii ni kwa sababu si lazima abiria kununua kitu hapo stendi, sasa wanacholilia ni nini?
Biashara zenyewe ni maji ya kunywa, sambusa, Mikate ya zaidi ya siku 4 toka izalishwe, etc magazeti ya zamani na vitabu visivyo na tija! Chaja na vifaa vingine vya simu visivyo na ubora na pombe za kwenye vichupa vya plastic.Kuingia ndani ni Tzs 500 kwa abiria:
 
Yakipaki nje hayalipi, na sio utaratibu. Abiria wanatakiwa kupanda na kushuka ndani ya bus stand terminal.
Sikubaliani na hili. Hakuna basi linapaki nje ya stendi ya Magufuli, labda Kama unamaanisha stendi nyingine tofauti na ya Magufuli. Tulikosea kuhamisha stendi ubungo bila kutafakari.
 
Back
Top Bottom