Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Na wewe huoni nafuu mbeba mzigo akipata pesa yako?
Kwani mimi ndio niliomleta hapa mjini hadi nimpe huo unafuu wa jasho langu??
Arudi kwao akalime au akafuge kuku.
 
Na wewe huoni nafuu mbeba mzigo akipata pesa yako?
Kwanini nione unafuu kwenye kuongeza gharama? Yaani unauliza kwanini nisione unafuu wa kulipia basi na mizigo 75elfu sababu ya kusafiri kulifata basi badala ya 45elfu kwa basi kuniletea huduma karibu?
 
Tundu lisuu na mbowe washaaungana tena...na wamekubaliana wale walioko Bungeni 19 wataendelea kuwa wanachama wa Chadema na watagombea Ubunge,vipi wewe washakupatia Kazi ya kufanya au utaendelea kuwapigia wezio uchawa humu?
 
Kwani mimi ndio niliomleta hapa mjini hadi nimpe huo unafuu wa jasho langu??
Arudi kwao akalime au akafuge kuku.
Hahaaa!! Hilo ni lako ila serikali haiwez kuhudumia wananchi wake hivyo. Tunaamn riziki popote hivyo kama yupo mjini acha tumtafutie namna kuliko akawe panya road
 
Tundu lisuu na mbowe washaaungana tena...na wamekubaliana wale walioko Bungeni 19 wataendelea kuwa wanachama wa Chadema na watagombea Ubunge,vipi wewe washakupatia Kazi ya kufanya au utaendelea kuwapigia wezio uchawa humu?
Achilia mbali kwamba hoja yako ni ya kijinga bali pia iko nje ya mada
 
Hahaaa!! Hilo ni lako ila serikali haiwez kuhudumia wananchi wake hivyo. Tunaamn riziki popote hivyo kama yupo mjini acha tumtafutie namna kuliko akawe panya road
Mwambie Hassan Bomboko mmepima maji ni marefu mno, raia wa Dar wamekataa kuwa watumwa kwenye nchi yao.
 
Tunajenga stand ili kurahisisha si kuongeza tatizo. Maamuzi magumu yanafanywa kabla hujaijenga sio baada ya kuijenga. Wanaotumia usafiri wa mabasi ndio wanaorahisishiwa na uwepo wa stand. Kufanya maamuzi magumu ili kuwaumiza wasafiri ni ukatili tu.
 
Kweli kabisa mkuu. Huyu utaratibu ni rafiki Kwa abiria , shida hao wauza soda na juisi wanalazimisha wote tuishie Mbezi ili tununue juisi zao.
 
Wenye mabasi lazima wawe na mbinu za kukabiliana na ushindani, (changamoto),mojawapo ni hiyo njia ya kuwafuata wateja waliko ama karibu nao, hizo fikra za kwamba wateja wote waende mbezi ni dumavu, (primitive thinking)
 
Ni wajinga wa kutupwa. Kwa nini abiria walazimishwe kushukia na kupakia hapo? Ili tu wafaidishe watu wengine? Nchi yetu ni nchi ya hovyo kweli kweli.
 
Punguzeni roho mbaya, Yani abiria kusogezwa Mpaka kigamboni au Magomeni au Shekilango unaona ni kosa? Hii roho ya wapi hii?
Hahaha, wanataka pipi na mikate inunuliwe stand.
 
Kama ndo mpango kwamba mkoa usiwe na stand shida ipo wapi sasa kulazimishana kwenda stand? Si mpango unatimia?
Tulitoka Mnazi mmoja, wakasema tuhamie Ubungo, sasa Mbezi , sababu ni kukua kwa mji , sasa Mbezi haijakua? utashangaa tunafika mikumi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…