Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Dar inawilaya sita kumbuka
Labda ungeshauri barabara ya Bunju kuwepo pia na stendi kisha barabara ya Mbagala mpaka kongowe kuwe na stendi

Ili kurahisha
Wilaya hizo tano sijui sita ziko karibu karibu kiasi kwamba hata kwa usafiri wa bajaji unatoboa. Mfano kuwa na stend moja dsm ni sahh kwa maana inazidiwa ukubwa na baadhi ya wilaya za morogoro. Mfano moro ina ukubwa wa km² 73000 huku dar ni almost km² 1600. 73000÷1600= 45 hivi. Kwa hiyo ktk moro moja unauwezo wa kuunda eneo la dar zikapatikana km 45. Dar eneo lake ni km tarafa ya wilaya ya ulanga
 
Hassan Bomboko, Dc wa wilaya ya Ubungo aache kuhangaika na machangudoa wa Riverside na Sinza badala yake ajikite hili suala linalotokea katika kata yake ya Mbezi na ubungo.

Aamke alfajiri akafunge ofisi za haya Mabadi pale urafiki na shekilango ayaamuru yakapakie mbezi, magufuli bus terminal
Hana mamlaka kufanya hivyo. Unafunga ofisi Kwa kosa gani. Atadaiwa fidia ambayo hawahi kudhania.
 
Tumia akili basi.
Kwa hyo unataka kusema kukiwa na Airport moja biashara inakua nzuri ktk hyo Airport.
Suala la usafiri ni zaidi ya biashara' ni kutoa huduma pia.
Sasa huduma haitakiwi kuwa ya gharama kubwa
Wangejua haihitaji kuwa na gharama wangewaambia kuongeza nauli yote ile?? Mbona walikaza hd mkapandishiwa nauli leo ndo waje kuwaonea huruma eti tunakusogeza hd ofsini
 
Kama latra imeruhusu kupanda na kushuka eneo fulani hilo halina shida. Shida ni hii ya kulazimisha kushusha kila sehemu kisa bus linapita eneo hilo, usimamaji wa bus usifanywe km wa hiace
Mbona mnapenda maisha ya tabu mno? Hivi mtu na mizigo yake akifikishwa karibu na anapokwenda mnapungukiwa nini? Unajua gharama ya kusafirisha mzigo kutoka mbezi hadi shekilango?
 
Bus haliwezi mfata mtu kila atakapokuwepo na sio bus tu hata daladala, hiyo sio uber au bolt ndugu yangu.

Ndio maana ikawepo center point ambayo ni stendi. Haikujengwa ili iachwe ikae hapo bila matumizi na isitoshe ni chanzo cha mapato kwa nchi na jamii pia.
Kwa Jiji kama Dar huwezi kuweka sehemu moja kuwa stendi ya mabasi. Inatakiwa stendi hata Tano.
Huyo Hassan ana ubavu wa kufunga ofisi za shabbiby au abood pale Ubungo?
Hana huo ubavu. Unafungaje ofisi bila kosa lolote. Kwenye soko huria demand na supply ndio regulators sio mihemuko.
 

Ila nchi hii ina viongozi wa ajabu sana, hapo unakuta waziri anayehusika kwa kushirikiana na timu Msoga, kwakua tu stendi ina jina la Magufuli, basi kubadilisha jina, ikashindikana baada ya mchezo wao kuwekwa mitandaoni.

Wameona waje na mbinu ya kutofanya ulazima kwa wamiliki wa ma bus kuhakikisha wanashushia abiria na mizigo yao pale stendi...... Ili stendi ijifie yenyewe taratibu..... Jambo la aibu na linalopaswa kukemewa na jambo hili linaendelea kuonyesha kwa namna gani nchi hii inaongozwa wajinga waliopewa nafasi. Hivi JPM angekua hai, kuna mmiliki wa mabasi angeivimbia serikali namna hiii?

Halafu hapo kuna dola, dola hiii hiii tunayosema kila siku iko mafunzoni kuhakikisha jicho lake linamulika kwa maslahi mapana ya taifa. Nadhani moja ya sehemu inayohitaji kufumuliwa ni mfumo mzima wa dola, umejaa wapigania matumbo tu .

Enyi wavivu, wazembe, wala rushwa na mafisadi wakubwa, jina la John Pombe Magufuli, hili halitakaa kufutika mioyoni wa taifa hili, historia itayasahau majina yenu pale tu mtakapokufa, lakini haitokaa kumsahau JPM.
Ungeweza kueleweka kama ungewasilisha hoja yako bila kushambulia na kutoa shutuma ambazo hauna ushaidi nazo. Hoja yako imelenga zaidi kumlinda Magufuli bila kufafanua ni hasara zipi zitajitokeza kwa hayo maamuzi yaliyofanywa.
Binafsi sikubaliani na hayo maamuzi kwa sababu yanawanyonya sana wasafiri sana sana eanaosafiri ni mizigo au wanatoka umbali mrefu.
 
Mizigo ukiitoa kariakoo peleka ofsi ya bus husika then litapakia hyo mizigo. Elewa stendi ni kutuo cha bus za abiria na siyo kituo cha bus za mizigo. Mizigo inapakiwa ofsini kwenu na abiria wanapakiwa stendi.
Unasafiri uende Arusha, una mzigo, unaenda nao hadi shekilango, unawapa ofisi, ofisi inaupakia kwenye gari halafu wewe unafata gari mbezi, gari linatoka shekilango linakupakia.
 
Mbona mnapenda maisha ya tabu mno? Hivi mtu na mizigo yake akifikishwa karibu na anapokwenda mnapungukiwa nini? Unajua gharama ya kusafirisha mzigo kutoka mbezi hadi shekilango?
Ungekuwa huna bajeti nao ungeachana nao tu. Shusha stend ili mbeba mizigo apate buku ya kulisha familia yake
 
Unasafiri uende Arusha, una mzigo, unaenda nao hadi shekilango, unawapa ofisi, ofisi inaupakia kwenye gari halafu wewe unafata gari mbezi, gari linatoka shekilango linakupakia.
Nenda nao mbezi mpande pamoja na mzigo wako
 
Miji inakua lazima kuwe na transit route enyi wenye vichwa vigumu. Mbona mtu akiwa anasafiri kwa ndege anatoka kibaha kuwahi ndege ya saa nane usiku na halalamiki? Acheni uvivu wa kulala. Kuna ajabu gani hapo la kuamka mapema mbona bar mnakesha 😂️😂️😂️😂️
Mfano wa ndege ni irrelevant. Basi Ina abiria wengi kuliko ndege na hata mabasi ni mengi kuliko ndege, hivyo siku abiria wa ndege wakifika idadi ya basi itabidi tujenge viwanja vingi vya ndege Kwa Dar. Kenya wamejitahidi wanaviwanja viwili vya ndege. Ndege za ndani na nje. Maaana pale jomo Kenyatta pamejaa ndege na abiria ni wengi.
 
Namaanisha sehemu zenye msongamano mkubwa wa watu, magari, majengo n.k
Kwa hiyo mbezi ikishajaa watu majengo n.k stand utataka ipelekwe chalinze na utataka ni lazima kupandia huko?
 
Ni mazoea tu..kwani usafiri wa ndege inakuwaje??Watu wanakaa Kiluvya ..wanawahi ndege hapo JNIA...wanajiandaa mapema.
Tusiishi kwa mazoea tufuate utaratibu
Naona mnatoa mfano wa ndege na basi. Yani Leo usafiri wa ndege m auweka mizani sawa na basi. Tafuta mfano relevant usilazimishe mambo. Siku ndege zikifikia idadi ya mabasi au siku ndege ikifikia idadi ya abiria ndio ulete huo mfano wako.
 
Kwa gharama ipi? Wewe huoni unafuu anaopata abiria kuepuka gharama ya kusafirisha mizigo hadi stand?
Na wewe huoni nafuu mbeba mzigo akipata pesa yako? Ukitaka unafuu hakikisha utitiri wa kodi ktk mafuta unaondolewa ndo pona yako. Hkuna unafuu kisa umepakia mzgo kutokea shekilango kuliko mbezi
 
Wangejua haihitaji kuwa na gharama wangewaambia kuongeza nauli yote ile?? Mbona walikaza hd mkapandishiwa nauli leo ndo waje kuwaonea huruma eti tunakusogeza hd ofsini
Punguzeni roho mbaya, Yani abiria kusogezwa Mpaka kigamboni au Magomeni au Shekilango unaona ni kosa? Hii roho ya wapi hii?
 
Bro naomba nitofautiane nawe kidogo. Jifikirie wewe ni abiria unaishi Upanga. Huna gari unategemea mwendokasi au daladala. Gari inaofisi tuseme Kigogo au Mnazi mmoja. Inakuja inakuacha Magufuli halafu wewe utafute usafiri kwenda Upanga.

Hapo hapo yenyewe inaenda tupu mpaka Mnazi mmoja. Ukitoka hapo stendi na mabegi yako mara uburute, ukabwe na kudondoka. Huu ni ukiritimba mkubwa mno. Au uneshafika level za kutembelea V8 linalowekwa mafuta na wananchi? Eti Daktari maana duh!
Tanga kuna utaratibu mzuri sana...Wamiliki wa mabasi wanakaa stand kubwa alafu wana magari yao Madogo Coster unapandia town inakupeleka stand kuu...
 
Back
Top Bottom