Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Kweli kabisa mkuu. Huyu utaratibu ni rafiki Kwa abiria , shida hao wauza soda na juisi wanalazimisha wote tuishie Mbezi ili tununue juisi zao.
Hao wauza soda na juice hiyo ni kesi ya watu wachache wanaweza wakatawanyika kwenda kwenye vituo vingine na hapo wakabaki wachache wanaoendana na idadi ya abiria wanaopita hapo.
Uzuri huduma zao zinahitajika kila mahali sio lazima mbezi tu
 
Wenye mabasi lazima wawe na mbinu za kukabiliana na ushindani, (changamoto),mojawapo ni hiyo njia ya kuwafuata wateja waliko ama karibu nao, hizo fikra za kwamba wateja wote waende mbezi ni dumavu, (primitive thinking)
yeah
 
Yaani watu badala ya kutatua kero za abiria wanatengenrza kero Kwa abiria Raisi anahimiza utatuaji kero.Wenye mabasi wanatua kero za abiria viongozi wanatengeneza kero Kwa abiria

Kuna kanuni inasema wengi wape abiria na Wenye mabasi ni wengi kuliko hao wafanyabiashara na maofisa wa serikalli.Abiria na Wenye mabasi Yuko pamoja hatuna shida tunafurahiana kinachofanyika Cha kupakia na kushusha abiria kwenye maeneo Yao .Hatuna tatizo.Tatizo linatengenezwa na kigenge Cha watu wachache wafanyabiashara stendi ya magufuli na viongozi wa serikali

Wasikilize walio wengi sio walio wachache.Walio wengi ndio hata kwenye kupiga kura ,kura nyingi ziko huko U apotengeneza kero Kwa walio wengi unajiweka nafasi mbaya hata kwenye kura nchi nzima sababu wasafiri watumia stendi ya Magufuli kwenda na kutoka mikoani ni wa nchi nzima
Kweli kabisa mkuu.
 
Wilaya hizo tano sijui sita ziko karibu karibu kiasi kwamba hata kwa usafiri wa bajaji unatoboa. Mfano kuwa na stend moja dsm ni sahh kwa maana inazidiwa ukubwa na baadhi ya wilaya za morogoro. Mfano moro ina ukubwa wa km² 73000 huku dar ni almost km² 1600. 73000÷1600= 45 hivi. Kwa hiyo ktk moro moja unauwezo wa kuunda eneo la dar zikapatikana km 45. Dar eneo lake ni km tarafa ya wilaya ya ulanga

Kwani hiyo Morogoro hakuna stendi za wilaya? Hata kama sio za kisasa?
 
Tulitoka Mnazi mmoja, wakasema tuhamie Ubungo, sasa Mbezi , sababu ni kukua kwa mji , sasa Mbezi haijakua? utashangaa tunafika mikumi
Unatoka zako kwenu Tukuyu na mikungu yako ya ndizi na viroba vya viazi mbatata wanakushushia Mikumi ujitafutie daladala za kufika kwenu Kibamba🤣
 
Kwani hiyo Morogoro hakuna stendi za wilaya? Hata kama sio za kisasa?
Ndo maana nikasema huko wanaziweka kwa sababu ya jographia yake moro ingekuwa ndogo km dar bas na stendi ingekuwepo moja tu maana baada ya kufika unaweza kufika popote kwa muda mfupi.
 
Lengo lao abiria washukie porini, haijulikani sababu
Sababu huwa ni kuitumia stand kubadilisha pori kuwa mji uliochangamka yaani zijengwe guest house, biashara zifanyike n.k

Lakini sasa hii si kazi kuu ya stand, stand kazi yake ni kurahisisha usafiri sio kuchangamsha eneo.

Ukifanya kazi kuu ya stand kuwa ni kubadilisha mapori kuwa mji ndo inafika mahali stand inakuwa gofu maana unajikuta una stand mbali na inaleta tatizo la usafiri kwa mkoa husika badala ya kulirahisisha.
 
Magari kupakia nje ya vituo kumepunguza vibaka. Mlitaka turundikane Mbezi mtuibie.
Hakika mkuu, na kuna mabasi yana vituo vikali sana unasuburia zako muda kuondoka umeri lax kabisa unakunywa pepsi yako bila karaha za vibaka na wapiga debe wanaovutavuta watu suruali na sketi.
 
Siku zote biashara haitakiwi kutegemea Stendi, bali stendi ndio inapaswa kutegemea biashara yako, shida ni hawa wafanyabiashara walidanganywa na ccm

Nimepita hapo stendi zaidi ya mara 50 lakini sikuwahi kununua chochote, hii ni kwa sababu si lazima abiria kununua kitu hapo stendi, sasa wanacholilia ni nini?
Ni siku nyingi watu walisema kuwa ''Muda utaongea''
kipindi hicho kimefika,wananchi tuamke,mateso hayo ambayo wafanya biashara wanataka kutusababishia
tuyarudishe kwao kwa kuweka mgomo wa kutonunua chochote stand,tuone kama napo itakuwa lazima ukishuka kwenye gari utanunua kitu. Kama ni wale wabeba mizigo,unampanga mtu wako wa kubeba anakuja kukupokea kama ndugu kumbe mkitoka stand tu unamlipa unasepa.
 
Pikipiki zina vituo vyake vilivyosajiliwa ndiyo. Na namna ya bus huwa ni stendi ya bus mengineyo ni kumsaidia abiria tu lakini kituo cha bus huwa ni stendi na si ofsini kwao. Bus ni mhimu kushusha abiria stendi ili hiace nazo zile vichwa, tudigeuze bus kufanya kazi za daladala
Kwenye biashara Kuna offer Kwa mteja ili kumvutia awe mteja wa kudumu Kutokana na offer. Mabasi yametumia hiyo gap kupata loyal customers. Ni mfumo wa kibiashara.
 
Ni siku nyingi watu walisema kuwa ''Muda utaongea''
kipindi hicho kimefika,wananchi tuamke,mateso hayo ambayo wafanya biashara wanataka kutusababishia
tuyarudishe kwao kwa kuweka mgomo wa kutonunua chochote stand,tuone kama napo itakuwa lazima ukishuka kwenye gari utanunua kitu. Kama ni wale wabeba mizigo,unampanga mtu wako wa kubeba anakuja kukupokea kama ndugu kumbe mkitoka stand tu unamlipa unasepa.
Na wakiendelea na huu ujinga wao hao wamachinga na vibega hicho ndicho kitafuata.
 
Unatoka zako kwenu Tukuyu na mikungu yako ya ndizi na viroba vya viazi mbatata wanakushushia Mikumi ujitafutie daladala za kufika kwenu Kibamba🤣
Tatizo ni tunabadili matumizi ya stand kutoka kwenye kurahisisha usafiri kwa watu wa mkoa husika kuwa:

1. Soko kwa wamachinga.
2. Nyenzo ya kubadili kakijiji kuwa mji.

Pakichangamka stand inapelekwa mbali. Sasa ikienda mbali vya kutosha lengo la kurahisisha usafiri linapotea maana unakuwa na stand mkoa X iliyo karibu na mkoa Y kuliko mkoa X.
 
Stendi ndogondogo ni za daladala na si bus!! Shida yenu mnafikiria bus kuwafikisha nyumbani, bus zinapiga ruti ndefu zikikufikisha kituo husika shuka ukapande hiace zinazoenda mtaani kwenu. Tusigeuze kazi ya daladala kufanywa na bus
Hapo utakuwa unampangia mwenye basi Cha kufanya. Yeye kaamua kuwasaidia abiria wake basi.
 
Basi watu wa Bukoba wana akili kumbe. Wamejenga stendi palepale katikati ya mji ili mzunguko wa kibiashara uwepo. Japo watajenga nyingine nje ya mji lakin hapo mjini kati lazima kuwepo na stendi

Ujenzi wa stendi mbali na mji ilikuwa scam mfano Songea, Dar, Dodoma,Morogoro mafiga, na miji mingi nchi hii
 
Lakini pia ni nzuri wao kuuza pipi, vituo kama hivyo vilistahili kuwa fursa kwa vijana na mama zetu kujipatia kipato. Kama una kazi maalum usione wanaolalamikia hili kama wakosefu, iliwasaidia mkono kwenda kinywani
Muuza pipi ndio analazimisha abiria waanzie Mbezi?. Sio sahihi. Mimi ningeona la maana kama abiria wangelalamika kuwa mabasi yaanzie na kuishia Mbezi. Kama abiria halalamiki, huyo muuza pipi ni nani wa kulazimisha kuzuia watu pipi?.
 
Back
Top Bottom