Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Mbona ndege huwa hamuombi mshushwe kwenu mnakubali kwenda airport? Utaratibu wa vituo ni muhimu sana, mkifanya shaghala baghala msilalamikie mfumo na utaratibu wa serikali.

Sasa Stand ya bus ya nini kama unaweza panda na kushuka popote?
Huo mfano wako wa ndege mbona una ukakasi sana.
 
Mimi na-support mabus kufuata abiria walipo na sio abiria kufuata mabus yalipo.
Bus haliwezi mfata mtu kila atakapokuwepo na sio bus tu hata daladala, hiyo sio uber au bolt ndugu yangu.

Ndio maana ikawepo center point ambayo ni stendi. Haikujengwa ili iachwe ikae hapo bila matumizi na isitoshe ni chanzo cha mapato kwa nchi na jamii pia.
 
Usingeitaja ccm nngeshangaa sana
Kiukweli ndo chanzo cha matatizo mengi ya nchi hii,
Lile soko linalojengwa pale Ubungo ilikuwa Lina uwezo wa kujengwa popote hata mambwe pande na bado lingepata wateja.
Hii stendi ilitakiwa isihame tena Ubungo Bali palitakiwa paboreshwe, maana ilihamishwa kutoka kisutu na mnazi mmoja
 
Ila nchi hii ina viongozi wa ajabu sana, hapo unakuta waziri anayehusika kwa kushirikiana na timu Msoga, kwakua tu stendi ina jina la Magufuli, basi kubadilisha jina, ikashindikana baada ya mchezo wao kuwekwa mitandaoni.

Wameona waje na mbinu ya kutofanya ulazima kwa wamiliki wa ma bus kuhakikisha wanashushia abiria na mizigo yao pale stendi...... Ili stendi ijifie yenyewe taratibu..... Jambo la aibu na linalopaswa kukemewa na jambo hili linaendelea kuonyesha kwa namna gani nchi hii inaongozwa wajinga waliopewa nafasi. Hivi JPM angekua hai, kuna mmiliki wa ma bus angeivimbia serikali namna hiii??.

Alafu hapo kuna dola, dola hiii hiii tunayosema kila siku iko mafunzoni kuhakikisha jicho lake linamulika kwa masilahi mapana ya taifa. Nadhani moja ya sehemu inayoitaji kufumuliwa ni mfumo mzima wa dola, umejaa wapigania matumbo tu .

Enyi wavivu, wazembe, wala rushwa na mafisadi wakubwa, jina la John pombe Magufuli, hili halitakaa kufutika mioyoni wa taifa hili, historia itayasahau majina yenu pale tu mtakapokufa, lakini haitokaa kumsahau JPM.
Hakuna haja ya wadau kuingia Stendi wao washushie popote na kupandishia abiria popote ikibidi wawe wanashushia abiria majumbani kabisaa😂.Mimi naona wamechelewa sana yaan muda wote huo walikuwa wanashushia Magufuli Stendi kweli mbali hivyo alaa jaman!Hao wafanyabiashara wanaomsifia na hapohapo kumlilia mama na kumpigia kampeni wahame waende huko mabasi yanaposhushia kwani wamekatazwa.Wafanyabiashara uchwara hao wanaolialia huku wanamsifia mkuu wa mkoa wajue hata huko mabasi yanakoshushia na kupandishia abiria kuna wafanyabiashara na wao wanataka kufanya biashara.Tusipangiane watu wazima kulialia kupiga magoti inatia hasira,hameni au ondokeni hapo au vaeni magwanda ya kijani muanze kampeni kabisaa maana tunaona mnafanya kampeni mixer kulialia.
(Fasihi)
 
Abiria wanaingia hiyo Stendi wakiwa wameshiba ama wamechoka, unataka wanunue nini saa 10 alfajiri? wakinunua mavyakula hovyo watachimba dawa njia nzima

Wakifika jioni wamechoka na kwao ni hapo kimara tu sasa wananunua nini hapo stendi ambacho nyumbani kwao hakipo? Wauzaji wenyewe afya zao ni mashaka matupu, unanunua ili ukaharishe?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ila nchi hii ina viongozi wa ajabu sana, hapo unakuta waziri anayehusika kwa kushirikiana na timu Msoga, kwakua tu stendi ina jina la Magufuli, basi kubadilisha jina, ikashindikana baada ya mchezo wao kuwekwa mitandaoni.

Wameona waje na mbinu ya kutofanya ulazima kwa wamiliki wa ma bus kuhakikisha wanashushia abiria na mizigo yao pale stendi...... Ili stendi ijifie yenyewe taratibu..... Jambo la aibu na linalopaswa kukemewa na jambo hili linaendelea kuonyesha kwa namna gani nchi hii inaongozwa wajinga waliopewa nafasi. Hivi JPM angekua hai, kuna mmiliki wa ma bus angeivimbia serikali namna hiii??.

Alafu hapo kuna dola, dola hiii hiii tunayosema kila siku iko mafunzoni kuhakikisha jicho lake linamulika kwa masilahi mapana ya taifa. Nadhani moja ya sehemu inayoitaji kufumuliwa ni mfumo mzima wa dola, umejaa wapigania matumbo tu .

Enyi wavivu, wazembe, wala rushwa na mafisadi wakubwa, jina la John pombe Magufuli, hili halitakaa kufutika mioyoni wa taifa hili, historia itayasahau majina yenu pale tu mtakapokufa, lakini haitokaa kumsahau JPM.
Umeongea ugoro tu
 
Hassan Bomboko, Dc wa wilaya ya Ubungo aache kuhangaika na machangudoa wa Riverside na Sinza badala yake ajikite hili suala linalotokea katika kata yake ya Mbezi na ubungo.

Aamke alfajiri akafunge ofisi za haya Mabadi pale urafiki na shekilango ayaamuru yakapakie mbezi, magufuli bus terminal
Huyo Hassan ana ubavu wa kufunga ofisi za shabbiby au abood pale Ubungo?
 
1. Kwani mtu anayeshuka uwanja wa ndege na anakaa Kunduchi huwa anafikaje nyumbani...?

2.Kwanini gari ziende Shekilango au Mnazi mmoja .....?
Bro kama hujawapi Panda daladala huwezi nielewa. Ukipanda ndege ya 250,000 huwezi linganishwa na mpanda gari wa 30,000 ambae hata njiani hajala kitu. Tofautisha hao watu wawili bro. Halafu kwenye ndege Kuna limit ya mizigo na bado wa shuttle za kupeleka watu cetre tofauti tofauti. Acheni kuwatesa masikini mkiwa kwenye V8 tulizowanunulia. Msitufungulie sisi biashara. Jifungulieni wenyewe lakini msitulazimishe tuvae vitenge maana una roboti lako la vitenge bandarini.
Tafuta njia mpya ya kupata wateja. Acheni ushamba wa kulazimisha vitu. Hatushuki huko kama hamtaki na mukufe!
 
Usitumie matako kufikiria...hakuna aliyesema kuwa abiria wa njiani asishushwe kabla ya basi kufika Magufuli bus terminal....kinachogusiwa hapa ni magari kugoma kupakia abiria hapo Magufuli
Mkuu magari hayajagoma, usitukane watu, kiuhalisia modality ya uendeshaji wa biashara hiyo kwa utaratibu huo inagoma.

Mkuu shida ni gari ilipie matumizi ya stendi, nina amini wenye mabasi wanalipa, kama sio serikali isingekubali.

Shida tunasahau kuwa ile ni stendi sio Soko. Wanaolalamika sio abiria, madereva, makondakta wala wapiga debe ambao ndio wadau wakuu.

Wenye mabasi wanayo mabasi mahsusi yanayoanzia na kumalizia ruti hapa Magufuli. Kila basi linahitaji abiria na stendi inahitaji ushuru, kama hela ya uhuru unalipwa na basi limejaza abiria kabla ya kufika hapo hamna sababu ya kulazimika kupita stendi.

Pia mabasi yanahitaji yadi ya kupaki na gereji ya kufanyiwa matengenezo, kitu ambacho hakipo hapo stendi. Kwa maana hiyo ni lazima mabasi yatoke nje.

Wanaolalamika hapa ni wachuuzi na wajasiriamali walio geuza stendi kuwa Soko. Kiusanifu hawakupaswa kuwepo pale, mahala pao ni kwenye Soko lililopo mkabala na stendi hapo

Haya ndio Madhara ya akili ya Mwendazake kutaka kufurahisha machinga! waelekezwe taratibu, kuwa wapo hapo kimakosa.

Tuache kufikiri kijamaa, tufikiri kibiashara zaidi, serikali ipate mapato, ajira zipatikane na huduma za jamiiii ziimarike na ziwe nafuu kama sio bure

Walalamikaji wasitake kublackmaili serikali kisa uchaguzi, wakubali walishaingizwa cha kike, na mganga wao kafa!!!
 
Miundombinu ya usafiri mkubwa na uchukuzi(Uwanja wa ndege, stendi za Mabasi,Bandari kavu)huwa inatakiwa iwe nje kidogo ya mji....ili
  • kuondoa msongamano wa magari barabarani...
  • Kupunguza uharibifu wa barabara za ndani ya mji
Ndo maana ndege Kuna shuttle za kupeleka watu. Acheni kutakua kutesa masikini atoke mbagala saa nane ili awahi Magufuli saa kumi na Moja. Ukiwa hujawahi teseka wala hutamuonea huruma mwenzako.
Empathy Kwa masikini ni kitu ambacho tajiri au kiongozi wa serikali hawezi kuwa nacho kabisa. Aliyeshiba hajui karaha ya njaa.
 
Ila nchi hii ina viongozi wa ajabu sana, hapo unakuta waziri anayehusika kwa kushirikiana na timu Msoga, kwakua tu stendi ina jina la Magufuli, basi kubadilisha jina, ikashindikana baada ya mchezo wao kuwekwa mitandaoni.

Wameona waje na mbinu ya kutofanya ulazima kwa wamiliki wa ma bus kuhakikisha wanashushia abiria na mizigo yao pale stendi...... Ili stendi ijifie yenyewe taratibu..... Jambo la aibu na linalopaswa kukemewa na jambo hili linaendelea kuonyesha kwa namna gani nchi hii inaongozwa wajinga waliopewa nafasi. Hivi JPM angekua hai, kuna mmiliki wa ma bus angeivimbia serikali namna hiii??.

Alafu hapo kuna dola, dola hiii hiii tunayosema kila siku iko mafunzoni kuhakikisha jicho lake linamulika kwa masilahi mapana ya taifa. Nadhani moja ya sehemu inayoitaji kufumuliwa ni mfumo mzima wa dola, umejaa wapigania matumbo tu .

Enyi wavivu, wazembe, wala rushwa na mafisadi wakubwa, jina la John pombe Magufuli, hili halitakaa kufutika mioyoni wa taifa hili, historia itayasahau majina yenu pale tu mtakapokufa, lakini haitokaa kumsahau JPM.
Waambieni sisi Tunahitaji kusafiri hivyo wanavyoviuza hata mtaani tunakoishi vipo. Wakati wa kusafiri Sio Wakati wa shopping.
 
Abiria wanaingia hiyo Stendi wakiwa wameshiba ama wamechoka, unataka wanunue nini saa 10 alfajiri? wakinunua mavyakula hovyo watachimba dawa njia nzima

Wakifika jioni wamechoka na kwao ni hapo kimara tu sasa wananunua nini hapo stendi ambacho nyumbani kwao hakipo? Wauzaji wenyewe afya zao ni mashaka matupu, unanunua ili ukaharishe?
Mikate na Biscuit na Juice za Azam
 
Ila nchi hii ina viongozi wa ajabu sana, hapo unakuta waziri anayehusika kwa kushirikiana na timu Msoga, kwakua tu stendi ina jina la Magufuli, basi kubadilisha jina, ikashindikana baada ya mchezo wao kuwekwa mitandaoni.

Wameona waje na mbinu ya kutofanya ulazima kwa wamiliki wa ma bus kuhakikisha wanashushia abiria na mizigo yao pale stendi...... Ili stendi ijifie yenyewe taratibu..... Jambo la aibu na linalopaswa kukemewa na jambo hili linaendelea kuonyesha kwa namna gani nchi hii inaongozwa wajinga waliopewa nafasi. Hivi JPM angekua hai, kuna mmiliki wa ma bus angeivimbia serikali namna hiii??.

Alafu hapo kuna dola, dola hiii hiii tunayosema kila siku iko mafunzoni kuhakikisha jicho lake linamulika kwa masilahi mapana ya taifa. Nadhani moja ya sehemu inayoitaji kufumuliwa ni mfumo mzima wa dola, umejaa wapigania matumbo tu .

Enyi wavivu, wazembe, wala rushwa na mafisadi wakubwa, jina la John pombe Magufuli, hili halitakaa kufutika mioyoni wa taifa hili, historia itayasahau majina yenu pale tu mtakapokufa, lakini haitokaa kumsahau JPM.
Waambieni sisi Tunahitaji kusafiri hivyo wanavyoviuza hata mtaani tunakoishi vipo. Wakati wa kusafiri Sio Wakati wa shopping
Ndo maana ndege Kuna shuttle za kupeleka watu. Acheni kutakua kutesa masikini atoke mbagala saa nane ili awahi Magufuli saa kumi na Moja. Ukiwa hujawahi teseka wala hutamuonea huruma mwenzako.
Empathy Kwa masikini ni kitu ambacho tajiri au kiongozi wa serikali hawezi kuwa nacho kabisa. Aliyeshiba hajui karaha ya njaa.
aliyekupa kibali cha kuwasemea Watu wa mbagala kuwa ni masikini ni nani? Takwimu kuwa mbahala kuna masikini ziko wapi
 
Bus haliwezi mfata mtu kila atakapokuwepo na sio bus tu hata daladala, hiyo sio uber au bolt ndugu yangu.

Ndio maana ikawepo center point ambayo ni stendi. Haikujengwa ili iachwe ikae hapo bila matumizi na isitoshe ni chanzo cha mapato kwa nchi na jamii pia.
Kwenye mji wenye watu milioni sita ni akili watu wafuate gari sehemu Moja? Hivi hata akili za kuzaliwa kwani tulinyimwa?
 
Wakati mwingine watu wanamalalamiko tu kwakua wanajisikia kulalamika.

Mbona Airport ipo Dar tu na watu wanatoka mpaka mikoa ya jirani kuja kupanda ndege??

Kwanini tusiwe na kituo kikuu kimoja ambacho ndio hicho??

Haya mafisadi yameamua kubebana katika ujinga basi tusiokua na sauti mnatuburuza tu mtakavyo.
 
Waambieni sisi Tunahitaji kusafiri hivyo wanavyoviuza hata mtaani tunakoishi vipo. Wakati wa kusafiri Sio Wakati wa shopping

aliyekupa kibali cha kuwasemea Watu wa mbagala kuwa ni masikini ni nani? Takwimu kuwa mbahala kuna masikini ziko wapi
Sio Kwa context hiyo ila fikiria umetoka Mbagala unafuata gari Magufuli Kwa sababu watu na viduka vyao havipati wateja. Au mtu atoke Tegeta Kuja Magufuli halafu gari lipite pale pale Tegeta likiwa linatoka. Ni umbuzi tu ndo unaweza kufanya mtu afikirie hivyo.
 
Miji inakua lazima kuwe na transit route enyi wenye vichwa vigumu. Mbona mtu akiwa anasafiri kwa ndege anatoka kibaha kuwahi ndege ya saa nane usiku na halalamiki? Acheni uvivu wa kulala. Kuna ajabu gani hapo la kuamka mapema mbona bar mnakesha 😂️😂️😂️😂️
 
Bro naomba nitofautiane nawe kidogo. Jifikirie wewe ni abiria unaishi Upanga. Huna gari unategemea mwendokasi au daladala. Gari inaofisi tuseme Kigogo au Mnazi mmoja. Inakuja inakuacha Magufuli halafu wewe utafute usafiri kwenda Upanga.

Hapo hapo yenyewe inaenda tupu mpaka Mnazi mmoja. Ukitoka hapo stendi na mabegi yako mara uburute, ukabwe na kudondoka. Huu ni ukiritimba mkubwa mno. Au uneshafika level za kutembelea V8 linalowekwa mafuta na wananchi? Eti Daktari maana duh!
Ni mazoea tu..kwani usafiri wa ndege inakuwaje??Watu wanakaa Kiluvya ..wanawahi ndege hapo JNIA...wanajiandaa mapema.
Tusiishi kwa mazoea tufuate utaratibu
 
Miji inakua lazima kuwe na transit route enyi wenye vichwa vigumu. Mbona mtu akiwa anasafiri kwa ndege anatoka kibaha kuwahi ndege ya saa nane usiku na halalamiki? Acheni uvivu wa kulala. Kuna ajabu gani hapo la kuamka mapema mbona bar mnakesha 😂️😂️😂️😂️
Uvivu wa kufikiri ingelipendeza zaidi badala ya uvivu wa kulala
 
Siku zote biashara haitakiwi kutegemea Stendi, bali stendi ndio inapaswa kutegemea biashara yako, shida ni hawa wafanyabiashara walidanganywa na ccm

Nimepita hapo stendi zaidi ya mara 50 lakini sikuwahi kununua chochote, hii ni kwa sababu si lazima abiria kununua kitu hapo stendi, sasa wanacholilia ni nini?
Hata mie nashangaa. Tulisemaga inawezekana Tanzania tukawa channel ya vituko mbinguni kuna watu wanatubishia. Ujinga ni kipaji
 
Back
Top Bottom