Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Miji inakua lazima kuwe na transit route enyi wenye vichwa vigumu. Mbona mtu akiwa anasafiri kwa ndege anatoka kibaha kuwahi ndege ya saa nane usiku na halalamiki? Acheni uvivu wa kulala. Kuna ajabu gani hapo la kuamka mapema mbona bar mnakesha 😂️😂️😂️😂️
Ulishawahi kuona mtu anagombana na daladala ili awahi airport? Uelewe uchumi wa nchi kwanza kabla ya kugomba. Pia kama mnataka wekeni stand kila barabara ya kutoka nche ya mji. Msitese watu wakutanike sehemu Moja kama kumbikumbi.
 
Ni mazoea tu..kwani usafiri wa ndege inakuwaje??Watu wanakaa Kiluvya ..wanawahi ndege hapo JNIA...wanajiandaa mapema.
Tusiishi kwa mazoea tufuate utaratibu
Swali Kuna wapanda ndege wanakimbizana na daladala? Ukimuona huyo ni kapewa hiyo tiketi. Kuna standard ya wapanda gari ambayo haijafika mnakotaka. Pia usafiri wenu wa umma ni mbovu kiasi kwamba unaweza hata achwa na hilo gari.
Au unataka tupande bodaboda tugongwe tufe mbaki wenyewe huku duniani?. Kama abood ananichukua Mbagala ananipeleka Moshi nyie inawauma Nini?
 
Swali Kuna wapanda ndege wanakimbizana na daladala? Ukimuona huyo ni kapewa hiyo tiketi. Kuna standard ya wapanda gari ambayo haijafika mnakotaka. Pia usafiri wenu wa umma ni mbovu kiasi kwamba unaweza hata achwa na hilo gari.
Au unataka tupande bodaboda tugongwe tufe mbaki wenyewe huku duniani?. Kama abood ananichukua Mbagala ananipeleka Moshi nyie inawauma Nini?
Tatizo kuna baadhi ya viongozi wanataka tufikiri wanavyotaka wao hata kama uwezo wao wa kufikiri ni mdogo
 
Abood Bus service

BM

Ally's star

Katarama

Happynation

Kilimanjaro

Tilisho

Kimbinyiko

Shabiby

Newforce

N.k

Ni miongoni mwa kampuni nyingi ambazo hazitaki kuingia Magufuli Bus terminal....usafiri wa asubuhi ni kazi sana , wanapita juu kwa juu
Acha uvivu. Mabasi yote hayo yana mfumo wa online wa kukata ticket na kwenye huo mfumo wana options za kuonesha unataka kupandia kituo gani na kushukia kituo gani.

Usilazimishe turudi enzi za ujima.
 
Tutaangalia interest ya abiria. Ndio maana huko kote Kuna mabasi yanaanza huko. Kwa watu wa mbande, kimbiji etc Kuna stendi Kigamboni, chanika, Temeke nk. Kwa bunju mabasi yanapitia njia ya bagamoyo au anaweza kukimbilia basi magomeni au urafiki Lazima tuwa appreciate wenye mabasi kwa kuwajali abiria baadala ya kulaumu.
Hii hata mimi nimeipenda.
Fikiria mtu anayekaa kimbiji kama anasafiri kwenda Mwanza na bus linatakiwa kuondoka saa 11 alfajiri stendi ya mbezi.
Sasa fikiria huyu mtu ataamka saa ngapi na apate usafiri gani wa kumfikisha mbezi saa 11 alfajiri?Au tufanye mtu anakaa Chanika akikodi taxi itamgharimu elfu 50 kumfikisha hadi mbezi,sasa wenye mabasi wameamua kujitolea kumfuata abiria alipo na abiria ataokoa hiyo pesa ya taxi hapa sioni tatizo ila itakuwa ni faida kwa wengi.
Na kama kuna abiria anayeishi mbezi ataingojea bus hiyohiyo kwenye stendi ya magufuli itampitia sioni ubaya wowote hapa.
 
Binafsi nashauri hi!! Bus lazima ipite stendi husika, then inaweza kuendelea na ruti za ofsini kwake. Kutokupita kabisa si suala la kushabikia, huko ni kutumia pesa za watanzania ovyo. Na vitu kama stendi vinawapa ajira watanzania wengi sasa mkigeuza kuwa magofu wale walioko pale wakaibe??
Na hivyo ndivyo inavyofanyika siku zote, pakilia popote lakini lazima upite stendi kuu
 
S

Siyo kweli, biashara inategemea watu wanao kuzunguka pamoja na hao abiria, changamoto ya hizi biashara zilizoko kwenye stendi bidhaa huuzwa Kwa bei ya juu,(biashara nyingi ni za kulazimisha mteja anunue), hata mimi Huwa spendelei kununua vitu stendi, hata hivyo unatakiwa uuze bidhaa ambazo unajua wateja watazinunua na siyo unazo fikiria watanunua, (you have to sale what you know they are going to buy not what you what you think they are going to buy).
Sijui kama umenielewa, ni kweli kwamba biashara hutegemea watu, lakini Je lengo la watu wanaokuja pale ni nini? wanakuja kupanda mabasi tu, hawalazimiki kununua chochote zaidi ya tiketi, Usifananishe Stendi na Kariakoo, kupeleka biashara Stendi ni kamari ya kitoto sana, lambalamba saa 10 alfajiri utamuuzia nani?
 
Sijui kama umenielewa, ni kweli kwamba biashara hutegemea watu, lakini Je lengo la watu wanaokuja pale ni nini? wanakuja kupanda mabasi tu, hawalazimiki kununua chochote zaidi ya tiketi, Usifananishe Stendi na Kariakoo, kupeleka biashara Stendi ni kamari ya kitoto sana, lambalamba saa 10 alfajiri utamuuzia nani?
Soma ulicho andika mara ya kwanza na ndicho nimekujibu pia soma na kuelewa nilicho kiandika
 
Mbona ndege huwa hamuombi mshushwe kwenu mnakubali kwenda airport? Utaratibu wa vituo ni muhimu sana, mkifanya shaghala baghala msilalamikie mfumo na utaratibu wa serikali.

Sasa Stand ya bus ya nini kama unaweza panda na kushuka popote?

Mkuu tunaona ndege zinatoka Uholanzi KLM au Qatar kwa kuwa kuna abiria wa kushuka na kupanda Kilimanjaro Airport haziwapeleki Julius Nyerere International Airport DSM hii ina maana airlines hizo kutoka nje kutua uwanja wa Kilimanjaro kisha kushusha na kupakia zinaruka tena kutua Dar es Salaam na Amani Karume Intl Airport Zanzibar zikitoka hapo zinakwenda ulaya na Arabuni.

Tujiulize kwanini mashiriki hayo ya ndege isiwabwage abiria DSM halafu abiria watafute ndege au basi kurudi Kilimanjaro au wapande boti kwenda Zanzibar kukamilisha safari yao?

Mashirika haya ya ndege yameona wapo abiria Kilimanjaro, wapo wa DSM na pia Zanzibar hivyo wameamua kuwafuata na kuwafikisha waendapo au karibu na waendapo abiria.

Hivyo hivyo makampuni ya mabasi yameona kuwa abiria ni mfalme / malkia kuamua badala ya kuwabwaga wote Magufuli bus terminal Mbezi DSM wawashushe au kuwapakia karibu na maeneo ya abiria wanapotoka au kwenda.

Nchi ya Tanzania ni unique kwa kutoa huduma bora kwa abiria wa ndege kimataifa kiasi unapanda ndege ya kimataifa halafu mruko / flight inatua sehemu tatu KIA, JNIA na AAKIA ZNZ na kuelekea ngambo ulaya na Arabuni. Huduma za mabasi wamiliki wao nao wanakwenda kimataifa kwa kutoa huduma rafiki kwa wateja wake yaani abiria kama vile mashirika ya ndege wanavyojitahidi kuwafikisha abiria karibu zaidi wanapopenda kushuka au kupanda wakati wa kusafiri.


Tuache kulazimisha kufanya ugumu kwa abiria kisa kuna Magufuli International Bus Terminal. Mteja ni mfalme.
 
hakuna gar lisilo ingia terminal mkuu apo umeelewa vibaya wanataka watu washushwe wote hapo gari liondoke tupu na liingie hapo likiwa tupu
Ndivyo ilivyokuwa hapo mwanzo japo hata mimi huo utaratibu nautambua kwamba siyo rafiki Hawa kuangalia mfumo mzima wa biashara ya usafirishaji ukuwaji wa mji na ongezeko la watu
 
Sasa wenye Mabasi hawatakiwi waachwe huru kiasi hiko....
Lazima wafuate utaratibu,,,
Mana sasa hayo Mabasi hadi Chanika na Vijibweni nisha yaona.....

Hatakama tupo Soko huru lakini lazima vitu vifanyke kwa utaratibu...
Kama mabasi kutumia ofisi zake kupakia abiria inakuuma sana iambie serikali ijenge stendi za mabasi kama hiyo Magufuli kila wilaya, kote Temeke, Kigamboni, Ilala na Kinondoni kuwe na stendi za kupakia na kushusha abiria kama ilivyo mikoa mingine.
 
Acha uongo. Abood lazima aingie stendi ya Magufuli kupakia. Hakuna basi aliingii pale stendi kupakia, wanachofanya ni kuwapa abiria offer ya kuwabeba nje ya kituo Cha stendi ya Magufuli. Ilitakiwa wapongezwe kwa moyo mzuri.
Yaani watu badala ya kutatua kero za abiria wanatengenrza kero Kwa abiria Raisi anahimiza utatuaji kero.Wenye mabasi wanatua kero za abiria viongozi wanatengeneza kero Kwa abiria

Kuna kanuni inasema wengi wape abiria na Wenye mabasi ni wengi kuliko hao wafanyabiashara na maofisa wa serikalli.Abiria na Wenye mabasi Yuko pamoja hatuna shida tunafurahiana kinachofanyika Cha kupakia na kushusha abiria kwenye maeneo Yao .Hatuna tatizo.Tatizo linatengenezwa na kigenge Cha watu wachache wafanyabiashara stendi ya magufuli na viongozi wa serikali

Wasikilize walio wengi sio walio wachache.Walio wengi ndio hata kwenye kupiga kura ,kura nyingi ziko huko U apotengeneza kero Kwa walio wengi unajiweka nafasi mbaya hata kwenye kura nchi nzima sababu wasafiri watumia stendi ya Magufuli kwenda na kutoka mikoani ni wa nchi nzima
 
Back
Top Bottom