Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Hiko sikatai lakini mfumo ilitakiwa Mfumo wote wa Mabasi makubwa:Kuanzia stendi hadi Karakana ni zikae nje ya mji....

Soko huru bila kufuata mipango mji ni ukichaa,,,,ndiyo maana sikuhizi kuna sheri mpaka karibu na Masoko....Shule zimejengwa karibu na Barabara
Mipango miji kapangeni kwanza Tandale, Buza, Vingunguti na Mbagala, acheni ujinga went wa kusumbua abiria. Huwezi kupeleka vituo vya mabasi porini eti useme ndio unapanga mji.
Stendi ya bus ilitakiwa iwepo hata hapo Kariakoo kabisa mtu akichukua mzigo wake anatupia kwenye gari na kusepa.
 
Mimi mfano nakaa mbezi ila nikifika kituoni nataka kwenda Moro naambiwa usafiri wa mabasi ya Abood haupatikani hapo ...Yapo Urafiki. Basi linajazia urafiki then linapita juu kwa juu Mbezi bila ya kuingia ndani stendi!

Zaidi ya asilimia 75-80 ya basi zinazoondoka alfajiri haziingii ndani ya stendi ya Magufuli badala yake zinapita juu kwa juu.

Wamiliki wa mabasi wanaihijumu serikali , wanaikosesha serikali mapato yake ya getini. Pia wanawahujumu watanzania kwa kuwakosesha ajira
Kwani lazima upande Abood kwenda Moro au ni masharti ya mganga wako??
 
Usitumie matako kufikiria...hakuna aliyesema kuwa abiria wa njiani asishushwe kabla ya basi kufika Magufuli bus terminal....kinachogusiwa hapa ni magari kugoma kupakia abiria hapo Magufuli
Kama lineshajaa tayari linakotokea aje Magufuli kupakia majini au?

Tiketi Sasa hivi zinakatwa Kwa njia ya mtandao ulioidhinishwa na LATRA kama mtandao Rasmi..ambao wenye mabasi lazima wautumie na uanaonyesha MTU atapandia au kushukia wapi mfano unaonyesha wazi kuwa uchague basi utapandia au kushukia wapi Shekilango au Maguful NK
Sio wenye mabasi ndio waliojiamulia kuweka hip mfumo hivyo ni LATRA

Sasa vyombo viwill vya serikali vinagongana LATRA anasema ruksa kupakia na kushusha mfano Shekilango au Urafiki hao wahuni wengine WA serikalini wanasema stendi mmoja Tu ya Magufuli vyombo viwilo cya serikali moja wanefanya KAZI kama wajinga Fulani hivi.Latra wako sahihi zaidi kuliko hao wajinga wengine mwaliko serikalini na hao wafanyabiashara

Kwa hiyo wanataka mfumo wote WA LATRA ufumuliwe ambao ulikubalika na Pande zote wenye mabasi ,Abiria na LATRA?

Hii nchi kuna upumbavu mwingi Sana Unaipa mlaka LATRA ifanye KAZI inafanya KAZI Yake vizuri anatokea mhuni huko anakuja na kupings KAZI yote kubwa na nzuri iliyofanywa na LATRA nini hicho?

Wafanyabiashara WA mabasi gomeni kabisa .Mpaki mabasi Abiria tunawaunga mkono .Haiwezekani watu wachache watese Abiria ambao wenyewe sio Abiria wala wamiliki WA mabasi
 
Wanashauri ujinga fikiria mtu anaishi Boko au Mwenge basi Lina Toka Arusha au Moshi au Tanga linalopita Njia hiyo Kwa hiyo linapita hapo Boko na hapo Mwenge linakwenda na abiria Hadi stendi ya Magufuli linawashusha kule waanze kutafuta usafiri wa kurudi Mwenge na Boko basi linarudi tupu hata kama linapaki Mwenge au boko si.biashara kichaa hiyo

Au mtu anaishi mbagala anatoka Lindi na Mtwara basi linafika mbagala linapitiliza mbagala na huyo abiria Hadi stendi ya magufuli linamshusha atafute usafiri wa kurudi mbagala basi linarudi mbagala tupu hata kama linapaki mbagala huo ni wendawazimu

Hakuna abiria atakubali Hilo
Kabisa....
 
Lazima utambue kwamba katika suala la usafiri abiria ndiye center ( ndiye customer) ya jambo hilo.

Chochote kinachofanywa ni lazima yaangaliwe masilahi yake.

Anapaswa asogezewe huduma hiyo kwa urahisi kila iwezekanavyo. Yahani ikitokea basi likasema lina magari ya kampuni ya kuwapeleka au kuwachukua majumbani hilo lipongezwe.

Ninyi mnataka mtu atumie shilingi 30,000 kutoka Mbezi kwenda Mbande usiku si ndiyo?
Inashangaza sana mkuu walalamikaji ndio wamejigeuza wao center na kipaumbele cha stendi wanajiita "wadau wa stendi"!🤣 Hawajui wadau wa stendi ni Abiria, wasafirishaji na serikali, wao wauza crisps, pipi na karanga ni watu wa ziada tu ambao hata wakiondolewa hakuna hasara yoyote.
 
Bus haliwezi mfata mtu kila atakapokuwepo na sio bus tu hata daladala, hiyo sio uber au bolt ndugu yangu.

Ndio maana ikawepo center point ambayo ni stendi. Haikujengwa ili iachwe ikae hapo bila matumizi na isitoshe ni chanzo cha mapato kwa nchi na jamii pia.
Sasa kama bus haliwezi kumfuata mteja mbona kuna vituo binafsi? Au ww Umeelewa kuwa bus kumfuata abiria nyumbani kwake?
 
Hassan Bomboko, Dc wa wilaya ya Ubungo aache kuhangaika na machangudoa wa Riverside na Sinza badala yake ajikite hili suala linalotokea katika kata yake ya Mbezi na ubungo.

Aamke alfajiri akafunge ofisi za haya Mabadi pale urafiki na shekilango ayaamuru yakapakie mbezi, magufuli bus terminal
Maamuzi Yake yatakuwa kinyume cha makubakuano Kati ya LATRA na wenye mabasi na Abiria

Ingia mtandao WA LATRA WA kukata Tiketi unaonyesha wazi vituo vipi vya kupandia na kushukia vituo vya Shekilango na Urafiki vimo kwenye mtandao

Akae chonjo muda wowote aweza ishia mahakamani.akienda pupa
 
Wakati mwingine watu wanamalalamiko tu kwakua wanajisikia kulalamika.

Mbona Airport ipo Dar tu na watu wanatoka mpaka mikoa ya jirani kuja kupanda ndege??

Kwanini tusiwe na kituo kikuu kimoja ambacho ndio hicho??

Haya mafisadi yameamua kubebana katika ujinga basi tusiokua na sauti mnatuburuza tu mtakavyo.
Kwa nini mikoa mengine kila wilaya ina stendi yake ila Dar unataka iwe na kituo kimoja tu?
Kwa nini Airport wauza karanga, crisps na maji hawaruhusiwi kuuzia wateja bidhaa zao ndani ya ndege au kwenye madirisha ya ndege?
 
Hii hata mimi nimeipenda.
Fikiria mtu anayekaa kimbiji kama anasafiri kwenda Mwanza na bus linatakiwa kuondoka saa 11 alfajiri stendi ya mbezi.
Sasa fikiria huyu mtu ataamka saa ngapi na apate usafiri gani wa kumfikisha mbezi saa 11 alfajiri?Au tufanye mtu anakaa Chanika akikodi taxi itamgharimu elfu 50 kumfikisha hadi mbezi,sasa wenye mabasi wameamua kujitolea kumfuata abiria alipo na abiria ataokoa hiyo pesa ya taxi hapa sioni tatizo ila itakuwa ni faida kwa wengi.
Na kama kuna abiria anayeishi mbezi ataingojea bus hiyohiyo kwenye stendi ya magufuli itampitia sioni ubaya wowote hapa.
Harafu hao wavivu ambacho hawajui ni kuwa msongamano umepungua kwa Kasi hapo magufuli ni kwasababu ya usafiri kuwa wa masala 24 na sio hayo mawazo yao mgando
 
Kwa nini mikoa mengine kila wilaya ina stendi yake ila Dar unataka iwe na kituo kimoja tu?
Tatizo la Dar es salaam kwenye uongozi ni mawili wengi wa viongozi WA Dar kuwepo huwekwa sababu wanapendelewa Wana connection lakini vichwani hamna kitu wenye akili hupelekwa mikoani ndio maana mikoani kunafanya vizuri

Pili viongozi wengine huhamishiwa Dar Kwa sababu za kiafya ili wakae karibu na hospital ya rufaa ya Mloganzila na Muhimbili wanakotakiwa kuwa wanahudhuria matibabu mara Kwa mara Kwa hiyo mkoa unakuta unaongozwa na wagonjwa wazima wako mikoani

Hii combination ya akili finyu na wagonjwa ndio inasababisha hizo chaos tunazoona

Jiji la Dar linahitaji watu wazima na wenye akili hasa
 
Mtu anaishi Ubungo,umekata ticket Kilimanjaro Express ofisi zake zilipo na safari inaanzia hapo.Kwamba abiria asiruhusiwe kupanda basi,liondoke tupu na abiria apande Bajaj au bodaboda wakakutane Magufuli?

Kwamba akitoka zake Marangu na ndizi na maparachichi yake ashushwe kwa lazima,basi liondoke tupu ili apande Tena Bajaj na bodaboda aende Ubungo? Kichaa kibichi hiki!
 
Inashangaza sana mkuu walalamikaji ndio wamejigeuza wao center na kipaumbele cha stendi wanajiita "wadau wa stendi"!🤣 Hawajui wadau wa stendi ni Abiria, wasafirishaji na serikali, wao wauza crisps, pipi na karanga ni watu wa ziada tu ambao hata wakiondolewa hakuna hasara yoyote.
Hata LATRA msimamizi mkuu WA usafiri WA nchi kavu hawatambui

Wanatambuliwa na wahuni Tu WA mjini
 
Harafu hao wavivu ambacho hawajui ni kuwa msongamano umepungua kwa Kasi hapo magufuli ni kwasababu ya usafiri kuwa wa masala 24 na sio hayo mawazo yao mgando
Hao vichwa panzi wakijua na hili utaona wameitisha mkutano mwingine wakitaka gari zote zianze safari kwa pamoja saa kumi na mbili asubuhi, hoja watakazokuja nazo sasa itakuwa vituko vitupu, wanaweza kusema hiyo lodge hapo ghorofani stendi haipati mapato hivyo serikali nayo inapoteza mapato.
 

Ila nchi hii ina viongozi wa ajabu sana, hapo unakuta waziri anayehusika kwa kushirikiana na timu Msoga, kwakua tu stendi ina jina la Magufuli, basi kubadilisha jina, ikashindikana baada ya mchezo wao kuwekwa mitandaoni.

Wameona waje na mbinu ya kutofanya ulazima kwa wamiliki wa ma bus kuhakikisha wanashushia abiria na mizigo yao pale stendi...... Ili stendi ijifie yenyewe taratibu..... Jambo la aibu na linalopaswa kukemewa na jambo hili linaendelea kuonyesha kwa namna gani nchi hii inaongozwa wajinga waliopewa nafasi. Hivi JPM angekua hai, kuna mmiliki wa mabasi angeivimbia serikali namna hiii?

Halafu hapo kuna dola, dola hiii hiii tunayosema kila siku iko mafunzoni kuhakikisha jicho lake linamulika kwa maslahi mapana ya taifa. Nadhani moja ya sehemu inayohitaji kufumuliwa ni mfumo mzima wa dola, umejaa wapigania matumbo tu .

Enyi wavivu, wazembe, wala rushwa na mafisadi wakubwa, jina la John Pombe Magufuli, hili halitakaa kufutika mioyoni wa taifa hili, historia itayasahau majina yenu pale tu mtakapokufa, lakini haitokaa kumsahau JPM.
Tatizo ni ushamba na kufanya mambo kwa sifa bila uhalisia. Darhaihitaji stand moja kubwa, bali inahitaji stand nyingi ndogo ndogo.
Huo ujenzi ulikuwa ni ufisadi tu.
 
Hii hata mimi nimeipenda.
Fikiria mtu anayekaa kimbiji kama anasafiri kwenda Mwanza na bus linatakiwa kuondoka saa 11 alfajiri stendi ya mbezi.
Sasa fikiria huyu mtu ataamka saa ngapi na apate usafiri gani wa kumfikisha mbezi saa 11 alfajiri?Au tufanye mtu anakaa Chanika akikodi taxi itamgharimu elfu 50 kumfikisha hadi mbezi,sasa wenye mabasi wameamua kujitolea kumfuata abiria alipo na abiria ataokoa hiyo pesa ya taxi hapa sioni tatizo ila itakuwa ni faida kwa wengi.
Na kama kuna abiria anayeishi mbezi ataingojea bus hiyohiyo kwenye stendi ya magufuli itampitia sioni ubaya wowote hapa.
Hatufikirii kabisa kabisa.
 
Back
Top Bottom