Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Alafu punguza uongo magari mengi yanayo pita njia ya mbezi yanaingia stendi kushusha na kulipa izo ada zako ndo yanaendelea na safari.
Mkuu kukuongezea, hata hayo yanayojaza nje ya bila kufika stendi yana lipa in advance ushuru wa gari na ushuru wa wasafiri.

Walalamikaji wanaona uchaguzi unakaribia wanaanza kutengeneza mtafaruku usio na kichwa wala miguu!
 
Aisee wewe kama ni ofisa WA serikali hakuna mjinga kama wewe Hivi unajua KAZI ya Sensa ni nini ? Kuwa unatala ujue idadi ya watu ili iweje?
Ili kuwasogezea huduma mhimu zinahitajika kwa idadi ya watu na si kwa ukubwa wa eneo. Stendi tunaweka kwa kufuata ukubwa wa eneo na si wingi wa watu. Watu wengi wanahitaji idadi kubwa ya vyombo vya usafiri na si wingi wa stendi
 
Daladala zinatakiwa kupakia level seats ndiyo na pia bus inatakiwa isiwe na vituo vingi vya kushusha abiria zinaongeza msongamano mjini. Tumien fursa ya kushindilia kuongeza daladala nyingi na hivyo mtakuwa mmetengeneza ajira zaidi. Bus za mwendokasi Mpya zitakuja very soon.
Boss unataka uturudishe enzi za ujima kwamba huduma zote za usafiri zilundikwe stand na daiwaka wapokee abiria.

Siku hizi kuna safari za usiku na abiria ni wengi, tiketi zinakatwa hadi mtandaoni kupitia simu, mabasi yanasafirisha mizigo n.k Mambo ni chap chap nowdays watu hawataki gharama zisizo na msingi.

Stand iwe kituo ambacho mabasi yanapita ila si lazima abiria wote wafuate mabasi hapo ili kupata huduma, kufanya hivyo ni kupotezeana muda na gharama zisizo na ulazima na tulishatoka huko.
 
Kwani hapo mbezi hakuna watu wanaoishi hapo?
Hao ndio watapanda na kushuka hapo stendi kuu.
Au hakuna watu wanaosafiri wanaoishi Mbezi ?
Yaani basi la lindi limpitishe abiria nyumbani kwake Vikindu, na likamshushe Mbezi ilimradi tu anunue maji na tishu
Halafu aanze kutafuta usafiri mwingine wa kurudi Vikindu.

Kama hapo mbezi hakuna abiria wanaoishi hapo, basi aliyejenga hiyo stendi alikuwa mwehu.
🙋‍♂️📝✍️👍👌👏👊🤝🙏
 
Ili kuwasogezea huduma mhimu zinahitajika kwa idadi ya watu na si kwa ukubwa wa eneo. Stendi tunaweka kwa kufuata ukubwa wa eneo na si wingi wa watu. Watu wengi wanahitaji idadi kubwa ya vyombo vya usafiri na si wingi wa stendi
Kwa hiyo jiji lenye watu milioni tano linahitaji stendi moja ya basi Kwa akili zako?
 
Kwenye soko huru na lenye ushindani, huwezi kulazimisha washindani wa kibiashara wafanye biashara kwa mbinu moja. Ndio maana stendi zipo nyingi, Kigamboni, magomeni, Urafiki, chanika etc. kulazimisha stendi iwe mmoja ni impracticable.
🙋‍♂️📝✍️👍👌👏👊🤝🙏
 
😄😄😄😄😄😄Lakini sababu nyingine pia dar ni mkoa uliojaa watu wa lawama sana kila kitu unachofanya hawakitaki yaani hawana jema.
Akija mkuu wa mkoa mchapakazi hawamtaki wanamuona katili kwa sababu watu wanataka kuishi kimazoea lakini baadae kuishi kwao kimazoea kukisababisha maafa fulani pia wanageuka na kuanza kulaumu serikali ina viongozi wazembe hawafuatilii raia.
Mfano mzuri ni wale raia wanaoishi sehemu za mafuriko kama jangwani na msimbazi serikali huwa inawatahadharisha kuhama maeneo ya mabondeni hawasikii na huwa wanapewa viwanja nje ya mji wakaishi huko wanakataa na kubeza kwamba hawawezi kwenda kuishi kijijini.
Baadae mafuriko yakija wanasombwa na maji wanaanza kulaumu serikali tena kwamba haijali raia wake watu wanasombwa na maji hao wanaangalia tu.
Mabasi yakisababisha msongamano mjini utasikia, bus zimegeuzwa kama daladala zinavituo vingi sana zinatuwekea jam mjini wkat stendi ipo
 
Labda hukuelewa. Stand ni ya bus na abiria, lakini baadhi ya wenye ma bus wanapakia abiria nje na kushusha abiria nje ya stand, hiyo siyo sawa. Washushe abiria ndani na wapakie abiria ndani ya stand.

Tusifanye mambo shaghalabaghala kwa kigezo cha kuwakimbia wafanya biashara. Wanapokuwa hawatumii stand hata serikali inakosa mapato.

Swala la abiria kupata mahitaji yao ndani ya stand siyo lazima lakini ikitokea anahitaji huduma hiyo ndani ya stand, iwepo, na ipo. Sio kwamba wafanya biashara wanalazimisha abiria kutumia huduma zao, hapana.

Habiria halazimishwi kutumia choo cha kulipia kama hahitaji huduma ya choo, halazimishwi kununua maji kama hayahitaji. Ilia ikiwa atahitaji zitakuwepo na atalipia, na itakuwa fursa kwa wenye biashara hizo.

Sijui kama umeelewa?

Hiyo stendi ipo wilaya ya Ubungo.
Temeke, Kinondoni, Ilala, Kigamboni hawana stendi ya Mabasi ya Mkoani.
Hivyo utaratibu wa sasa uendelee lakini iwe kwa sharti kuwa magari yote yatakayopotia barabara ya chalinze ambapo kuna halmashauri ya Ubungo basi yaingie Stendi ya Magufuli.

Umeelewa
 
Vituo gani? Mabasi yanakuwepo kwenye ofisi zao. Mfano pale shekilango, zile ofisi pale zinaleta uchafu gani? Pako kimyaaa hakuna makelele ya stand.
Ukianza kusgusha hapo shekilango si boda na hiace nazo zinaanza kutega hapo hapo kula vichwa ulivyoshusha?
 
Tena haitakiwi iitwe stend kuu ya mabasi.
Inatakiwa iitwa stendi ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Kisha pawe na stand za Wilaya za aKinondoni,Ilala,Temeke na Kigamboni.
Yote ni kutanua wigo wa mapato na kuwapelekea huduma wananchi wanyonge.

Walitakiwa wajiuze palikua na sababu gani kujenga stend ya mkoa wa Pwani Kibaha halafu ya mkoa wa Dsm ijegwe Mita cha kutoka kibaha. Kwa nini stand ya mkoa wa Pwani isingejengee hata Kongowe au Mlandizi?

Ndio nilikuwa namjibu mwingine hivi kumbe umekwisha tangulia kusema.
Unamawazo kama yangu
 
Kwa hiyo jiji lenye watu milioni tano linahitaji stendi moja ya basi Kwa akili zako?
Ndiyo linahtaji stendi moja yenye uwezo wa kuhudumia bus 200. Mkiwekewa stendi nyingi mtaanza pia kulalamika, nifike stebndi ya kwanza ushuru, ya pili ushuru na ya 3 ushuru wakati zote nazifikia ndani ya nusu saa.
 
Back
Top Bottom