Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Tulichojitahidi ni kuhakikisha maeneo hayo yana ruti za daladala zinazokufikisha mbezi ukapande bus
Daladala ni usafiri binafsi labda ungesema mwendokasi ambazo kidogo zinamilikiwa na serikali lakini kwa bahati mbaya mwendokasi kuanzia saa tano au sita usiku hazitoi huduma.
Hao wamiliki wa Daladala asilimia 95 ikfika usiku kuanzia saa sita wanalaza magari yao. Na huwezi walazimisha kutoa huduma usiku.
Hivyo abiria anayeingia usiku kutokea labda mwanza, kigoma, Bukoba, na mara lazima apate chamoto akifika usiku. Kuanzia nauli kuwa juu kama atakodo Bodaboda, tex au bajaji.
Sasa kama Basi Limerahisisha usumbufu huo kwa abiria wake kwa nini iwe Nongwa?