Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Tulichojitahidi ni kuhakikisha maeneo hayo yana ruti za daladala zinazokufikisha mbezi ukapande bus

Daladala ni usafiri binafsi labda ungesema mwendokasi ambazo kidogo zinamilikiwa na serikali lakini kwa bahati mbaya mwendokasi kuanzia saa tano au sita usiku hazitoi huduma.

Hao wamiliki wa Daladala asilimia 95 ikfika usiku kuanzia saa sita wanalaza magari yao. Na huwezi walazimisha kutoa huduma usiku.

Hivyo abiria anayeingia usiku kutokea labda mwanza, kigoma, Bukoba, na mara lazima apate chamoto akifika usiku. Kuanzia nauli kuwa juu kama atakodo Bodaboda, tex au bajaji.

Sasa kama Basi Limerahisisha usumbufu huo kwa abiria wake kwa nini iwe Nongwa?
 
Final destination ya nyoko, Tulishahama enzi za ujamaa na villagization.
Hahaaa!! Tanzania ni nchi ya umoja bana, wote tushukie sehem moja then tukaribishane majumbani tuelekeako.
 
Stend 3 hazistahili ndiyo ila bus kuwa nyingi ndo sahihi ili kuweza kumudu wingi wa abiria.
Wewe nawe una shida. Stendi zisiwe tatu ila mabasi yake mengi. Wingi wa mabasi ndio uanapelekea ujenzi wa stendi.
 
Umbali kutoka Stendi ya Moshi vijijini(Himo) to Moshi ni 35 Km
Umbali kutoka Bunju wilaya ya Kinondoni to Wilaya ya ubungo Mbezi luis stendi ni 33km.

Kutoka Mbagala kongowe wilaya ya temeke to Mbezi luis wilaya ya ubungo ni 35km
Kutoka Moshi mjini to Hai(boma ng'ombe stendi) 50km

Kuna magari yanaanzia wilayani pasipo kupitia makao makuu ya mkoa na moja kwa moja yanaenda mikoa au wilaya zingine.
Hakuna watendaji wa serikalini wabovu kama wa Dar es salaam

Tamisemi tuleteeni Dar watendaji wa mikoani achaneni na Hawa zero brain wa Dar es salaam ndugu zenu ,marafiki nk tuleteeni Wenye akili mliowasokomeza mikoani huko

Watendaji wote waliopo washugulikia mambo ya usafiri mikoani wengine wote waondoke wabakie wa LATRA tu wengine hata kama sio LATRA waendekeza huo ujinga wawe wanasiasa NK Mamlaka za uteuzi au waliowaleta wawafungashe virago

LATRA tu asiondoke Mfanyakazi hata mmoja wako vizuri
 
Daladala ni usafiri binafsi labda ungesema mwendokasi ambazo kidogo zinamilikiwa na serikali lakini kwa bahati mbaya mwendokasi kuanzia saa tano au sita usiku hazitoi huduma.

Hao wamiliki wa Daladala asilimia 95 ikfika usiku kuanzia saa sita wanalaza magari yao. Na huwezi walazimisha kutoa huduma usiku.

Hivyo abiria anayeingia usiku kutokea labda mwanza, kigoma, Bukoba, na mara lazima apate chamoto akifika usiku. Kuanzia nauli kuwa juu kama atakodo Bodaboda, tex au bajaji.

Sasa kama Basi Limerahisisha usumbufu huo kwa abiria wake kwa nini iwe Nongwa?
BAsi tufanye bus ziruhusiwe kusogeza abiria zikifika stendi muda ambao siyo rafiki hasa ambapo daladala na mwendokasi wamestop. Hii walau utasikilizika
 
Mbona una Airport moja na watu wanakwenda na kuondokea huko.mtu yoyote anayejua ana safari lazima ajiandae na safari hiyo huwezi kuwa na nchi kila mahala mabasi yanapaki hovyo hovyo.mabasi yote yalitakiwa yaishie stendi kuu-watu watafute means za kufika huko stendi.

Usafiri wa anga na Majini ni mbingu na ardhi.

Kwa kukusaidia tuu 99% ya watanzania hawajawahi kupanda ndege.
90% hawajawahi hata kuuona uwanja wa ndege.
 
Hakuna watendaji wa serikalini wabovu kama wa Dar es salaam

Tamisemi tuleteeninDar watendaji wa mikoani achaneni na Hawa zero brain wa Dar es salaam ndugu zenu ,marafiki nk Wenye akili mliowasokomeza mikoani huko

Watendaji wote waliopo washugulikiq mambo ya usafiri wengine wote waondoke wabakie wa LATRA tu wengine hata kama sio LATRA waendekezahuo ujinga wawe wanasiasa NK Mamlaka za uteuzi au waliowaleta waeafungashe virago

LATRA tu asiondoke Mfanyakazi hata mmoja wako vizuri

Ni kweli
 
BAsi tufanye bus ziruhusiwe kusogeza abiria zikifika stendi muda ambao siyo rafiki hasa ambapo daladala na mwendokasi wamestop. Hii walau utasikilizika

Kwani sasa zinafanyaje?

Basi sio Daladala hiyo elewa. Linaenda na muda.
Kupakiza abiria wanatoa muongozo kuwa abiria wote wasubiri kituo fulani watakutwa hapo. Sio kwamba kila kituo anashushwa mtu. Vinginevyo yangekuwa yanachelewa huko yaendako
 
Wafanyakazi wa LATRA hongereni Kwa kazi nzuri ya kitaalamu mumefanya

Yeyote mtendaji asiye Mfanyakazi wa LATRA kuketa za kuleta za kuleta anayejaribu .kuvuruga vitu vya kitaalamu mlifanya Mamlaka iliyomteua ihangaike naye imwondoe Dar aende ampeleke huko anakojua mwenyewe kusikozingatia utaakamu

LATRA mko fit na wamiliki WA mabasi na Abiria Yuko pamoja na nyie
 
Kwani sasa zinafanyaje?

Basi sio Daladala hiyo elewa. Linaenda na muda.
Kupakiza abiria wanatoa muongozo kuwa abiria wote wasubiri kituo fulani watakutwa hapo. Sio kwamba kila kituo anashushwa mtu. Vinginevyo yangekuwa yanachelewa huko yaendako
Sasa hv hata bus ikifika jioni mnataka iwafikishe shekilango
 
Yani miafrika ni matahira yawe yamesoma au hayajasoma,yani una nchi kila bus lina Ofisi yake linashusha wanapotaka wao halafu kuna majitu yanaona ni sawa eti kisa tu sijui wengine wanaishi Bunju mara Mbagala.

Hivi huu uzezeta utakwisha lini jamani,kuna maana gani ya kujenga hizi stendi za mabasi sasa?? Ukienda pale manzese hadi magomemi ni Ofisi tu za mabasi-Ofisi zimekuwa kama taka taka utadhani hakuna Serikali.

Ukija Dodoma Kimbinyiko,Shabibihi,Satco,BM,Machame, na mengine mengi kila basi inaofisi na parking zake ya nini huku stendi zimejengwa na kuwekewa Ofisi.
Ondoa ujuha wako hapa, London ambayo ni ndogo kuliko Dar es Salaam ina vituo vikubwa zaidi ya 10 vya kupakia mabasi ya kwenda nje ya London. Vituo vya magari ya daladala yanayohudumia London ni zaidi ya 19,000 na hata magari yanayotoka nje ya London yanaweza kuvitumia vingi vya hivyo vituo kushusha abiria. Kushindwa kwenu kupanga miji kulikopeleka ujenzi holela ndio inakufanya uone Dar vituo vya gari ni vingi sana wakati ukweli ni kwamba ni vichache sana ukilinganisha na miji mingi inayokaribiana nayo kwa ukubwa.
 
Yani miafrika ni matahira yawe yamesoma au hayajasoma,yani una nchi kila bus lina Ofisi yake linashusha wanapotaka wao halafu kuna majitu yanaona ni sawa eti kisa tu sijui wengine wanaishi Bunju mara Mbagala.

Hivi huu uzezeta utakwisha lini jamani,kuna maana gani ya kujenga hizi stendi za mabasi sasa?? Ukienda pale manzese hadi magomemi ni Ofisi tu za mabasi-Ofisi zimekuwa kama taka taka utadhani hakuna Serikali.

Ukija Dodoma Kimbinyiko,Shabibihi,Satco,BM,Machame, na mengine mengi kila basi inaofisi na parking zake ya nini huku stendi zimejengwa na kuwekewa Ofisi.
Kwanini tunajenga stendi?
 
Mabasi yaingie stand ya Magufuli lakini isiwe lazima abiria wote kushukia stand. Tusilazimishe mambo yaani abiria anaishi chanika na basi inaenda chanika ashukie hapo ahangaike na usafiri kisa tu anunue sijui maji, soda au ale chakula hapo. Mi binafsi nimepandia hapo na kushukia hapo mara nyingi lakini sijawahi nunua chochote zaidi ya maji na hiyo ni wakati wa asubuhi tu magari yanaondoka lakini wakati wa kurudi usiku sijawahi nunua chochote
 
Kwa gharama ipi? Wewe huoni unafuu anaopata abiria kuepuka gharama ya kusafirisha mizigo hadi stand?
Mbona wakati stendi ipo ubungo mlikuwa mkienda na mizigo yenu!? Mbona ilivyokuwa kisutu na kisha mnazi mmoja mlikuwa mkienda stendi na mizigo yenu??

Mbona mabasi yalikuwa yakishusha na kupakia hapo stendi?
 
Back
Top Bottom