Wafanyabiashara wa Kariakoo jiandaeni kisaikolojia kutokana na kituo cha biashara kinachojengwa pale Ubungo

Wafanyabiashara wa Kariakoo jiandaeni kisaikolojia kutokana na kituo cha biashara kinachojengwa pale Ubungo

LICHADI

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2015
Posts
4,491
Reaction score
12,560
Hili Soko la China linalojengwa pale Ubungo Msilichukulie poa kabisa mchina atauwa Biashara nyingi sana kuanzia za hawa Niagize china hadi Hawa Silent ocean ambao wanasafirisha mizigo ya watz kutoka china kuileta Tz maana China atakuwa na kampuni zake mwenyewe za usafirishajiusafirishaji na hakutakuwa tena na watu wengi wanaoenda chimbo china wakati wachina wenyewe wakefika hapa so watu wataishia hapo ubungo.

Dhumuni La Mchina pale ni kutambulisha na kuuza Bidhaa zake zote Afirca mashariki kwa bei ya china yaani badala ya kusema ngoja niende nikanunue china wachina wenyewe utakutana nao pale kwa bei zile zile za China.

Maana yake Mchina anakuja kuuwa kwa zile Biashara za Kona Kona unakuta Tv inch 32 inanunuliwa china kwa sh 80,000 ikifika bongo udalali ule wa Niagize china au watu wanaoziagiza China huko, hadi ikufikie we wewe ni sh 25000 hadi 300000.

Sasa wachina pale watakuja kuleta balaa kwa bei zao kitonga, Hili jambo silifurahii Ila kiuchumi sijui litakuwaje, Hapo kariakoo wateja wao wakubwa ni Wazambia, Wacongo, wamalawi , wa Zimbabwe

Na wazee wa kkkoo huwa hawapendi wacongo na wazmbabwe wawafaham wachina au wajue machimbo ili wauze , sasa mchina kaja wenyewe hapo ubungo Muda utaongea.

@🪈WAUZAJI WA VIFAA VYA UMEME NDIO WAWE MAKINI SANA

PIA SOMA
- Wafanyabiashara watakiwa kuchangamkia fursa kuchukua maduka kwenye soko la Kimataifa la Biashara linalojengwa Ubungo na EACLC
 
Back
Top Bottom