Wafanyabiashara wa Kariakoo jiandaeni kisaikolojia kutokana na kituo cha biashara kinachojengwa pale Ubungo

Hili Soko la China linalojengwa pale Ubungo Msilichukulie poa kabisa mchina atauwa Biashara nyingi sana kuanzia za hawa Niagize china hadi Hawa Silent ocean ambao wanasafirisha mizigo ya watz kutoka china kuileta Tz maana China atakuwa na kampuni zake mwenyewe za usafirishajiusafirishaji na hakutakuwa tena na watu wengi wanaoenda chimbo china wakati wachina wenyewe wakefika hapa so watu wataishia hapo ubungo.

Dhumuni La Mchina pale ni kutambulisha na kuuza Bidhaa zake zote Afirca mashariki kwa bei ya china yaani badala ya kusema ngoja niende nikanunue china wachina wenyewe utakutana nao pale kwa bei zile zile za China.

Maana yake Mchina anakuja kuuwa kwa zile Biashara za Kona Kona unakuta Tv inch 32 inanunuliwa china kwa sh 80,000 ikifika bongo udalali ule wa Niagize china au watu wanaoziagiza China huko, hadi ikufikie we wewe ni sh 25000 hadi 300000.

Sasa wachina pale watakuja kuleta balaa kwa bei zao kitonga, Hili jambo silifurahii Ila kiuchumi sijui litakuwaje, Hapo kariakoo wateja wao wakubwa ni Wazambia, Wacongo, wamalawi , wa Zimbabwe

Na wazee wa kkkoo huwa hawapendi wacongo na wazmbabwe wawafaham wachina au wajue machimbo ili wauze , sasa mchina kaja wenyewe hapo ubungo Muda utaongea.

@🪈WAUZAJI WA VIFAA VYA UMEME NDIO WAWE MAKINI SANA
Acheni kushabikia hii kitu msichokijua. Kwa kuwa na hili soko la Ubungo, China wataongeza uwezo wao wa kuuza nje bidhaa zao za viwandani. Kwa kuwa bidhaa zao nyingi za viwandani zinategemea kwa kiasi kikubwa mali ghafi za mashambani na mali ghafi nyingine za kwao, soko la Ubungo pia litaongeza soko la mali ghafi zao kwenye viwanda vyao. Ongezeko hili la pamoja la bidhaa za viwandani na mali ghafi zitaongeza mara dufu nafasi za ajira kule China peke yake (kwa raia wa China na watu wengine wanaoishi China) mbali na kuongeza makusanyo ya kodi kwa serikali ya China. Utekelezaji wa sera ya viwanda ya nchi yetu umewekwa rehani! Sera ya kuanzisha na kuimarisha Export Processing Zones nayo iko mashakani. Kwa uchache kama soko hili litaongeza tani moja ya mauzo ya bidhaa za viwandani za China si chini ya nafasi za ajira laki moja zitatengenezwa kule China badala ya nafasi hizo kutengenezwa kwa ajili ya watanzania na hasa watanganyika. Tusubiri tuone! Aliyekuja na hili wazo la soko la Ubungo ameiweka rehani nchi yetu because it negates our country's industrialization policy. We are never too late.
 
Kariakoo ni muunganiko wa mitaa, ni kamji kadogo. Kituo cha ubungo ni kama ukumbi hauwezi ua biashara ya Kariakoo labda mtu asiyeijua Kariakoo ndio atakubali.

Zile block walizojenga na fremu zinavyolingana sio za kuua biashara ya Kariakoo. Na sidhani kama Ubungo watauza jumla, hata wakiuza jumla mbongo mwenye hiyo elfu tisini ya kununua TV uchwara hawezi uziwa moja.
Acheni kujilisha upepo
 
Hili Soko la China linalojengwa pale Ubungo Msilichukulie poa kabisa mchina atauwa Biashara nyingi sana kuanzia za hawa Niagize china hadi Hawa Silent ocean ambao wanasafirisha mizigo ya watz kutoka china kuileta Tz maana China atakuwa na kampuni zake mwenyewe za usafirishajiusafirishaji na hakutakuwa tena na watu wengi wanaoenda chimbo china wakati wachina wenyewe wakefika hapa so watu wataishia hapo ubungo.

Dhumuni La Mchina pale ni kutambulisha na kuuza Bidhaa zake zote Afirca mashariki kwa bei ya china yaani badala ya kusema ngoja niende nikanunue china wachina wenyewe utakutana nao pale kwa bei zile zile za China.

Maana yake Mchina anakuja kuuwa kwa zile Biashara za Kona Kona unakuta Tv inch 32 inanunuliwa china kwa sh 80,000 ikifika bongo udalali ule wa Niagize china au watu wanaoziagiza China huko, hadi ikufikie we wewe ni sh 25000 hadi 300000.

Sasa wachina pale watakuja kuleta balaa kwa bei zao kitonga, Hili jambo silifurahii Ila kiuchumi sijui litakuwaje, Hapo kariakoo wateja wao wakubwa ni Wazambia, Wacongo, wamalawi , wa Zimbabwe

Na wazee wa kkkoo huwa hawapendi wacongo na wazmbabwe wawafaham wachina au wajue machimbo ili wauze , sasa mchina kaja wenyewe hapo ubungo Muda utaongea.

@🪈WAUZAJI WA VIFAA VYA UMEME NDIO WAWE MAKINI SANA
Kariakoo hujaijua vizuri bado. Kariakoo ni habari nyingine ni soko kubwa mno, linaweza kuwa ndo soko kubwa la bidhaa mbali mbali east and central africa. Kwa population tu kariakoo ina watu wengi kuliko sehemu yoyote africa mashariki na kati
 
Back
Top Bottom