Wafanyabiashara wa Kariakoo jiandaeni kisaikolojia kutokana na kituo cha biashara kinachojengwa pale Ubungo

Pamoja na kwamba Chalamila ameeleza vizuri baadhi ya mambo, posting hii haina uhusiano na mada ya uanzishwaji wa soko la Ubungo.

Hata hivyo kati ya mambo yanayolalamikiwa kwa siku nyingi na wafanyabiashara ni Service Levy.

Mantiki ya Sevice Levy haijawahi kuelezwa na kueleweka hata kidogo. Kodi hii hutozwa kwa mauzo ghafi na ni kati ya kodi zinazo zorotesha "capital build up au capital accumulation" miongoni mwa wawekezaji watanzania kitu ambacho kingeweza kuhamasisha uwekezaji zaidi na kuongeza fursa za ajira kwa watu wetu.
 
Kariakoo utapeli na udalali mwingu, mara migomo.

Wanawashawishi wafanyabiashara kutoka nchi jirani wanunue bila risiti, wakikamatwa wanawaruka. Acha mchina aje
 
Litawezekana only km hakuna utitiri wa ushuru otherwise saving itakua ndogo sana Kwa aliopo kkoo na ubungo
 
Picha tafadhali
 
Mlioko dar sisi wa mikoani tunaomba hao masupplier wa kichina wakitia maguu mtusaidie kupata mawasiliano nao
 
Kuna wachina juzi nimewaona huku kwetu wanazunguka na begi za shule kwenye maduka ya jumla kutafuta masoko walikuwa na mbongo ndio anawaongoza siku kadha hapo nyuma niliwaona pia alikuwa mchina mmoja na huyo manzi nikajua labda manzi kaopoa tu mchina anajilia vyake kumbe bhana na kuna biashara hapo ndani juzi ndio nimesanuka baada ya kuona wako na mabegi kwenye toroli
 
Ushindani lazima uwepo wafanyabiashara wa kariakoo walibweteka sana. Vishoka wamekuwa wengi. Tushukuru hao wachina wamejenga Tanzania, wangejenga Kenya au Zambia?
 
Stop misled, pale ubungo patakuwa ni soko la ununuzi bidhaa China, wenye mitaji ndio watakaofanya biashara pale, wewe wa chini mambo yatakuwa yale yale tu, PALE UBUNGO ZAIDI PATAKUWA NI PAHALA PA UHAKIKA PA KUAGIZIA MIZIGO KUTOKA KWENYE SOURCE ZA UHAKIKA CHINA, SECTOR ZOTE ZITAFANYA KAZI KAMA KAWAIDA, MUNGU ASAIDIE MRADI HUU UANZE MAPEMA IWEZEKANAVYO
 
Huwa nashabgazwa na statement kama hizi. Nchi za watu masoko kama KKO yapo sehemu mbali mbali na kila mtu anafanya biashara kwa uwezo wake

KKO haiwezi kuja ku slow down , hizo kampuni unazosema ambazo zinaingiza mizigo zipo TZ miakq mingi saana….. na hakuna kilichoharibika
Wanaopaswa kuwa na hofu ni Hilo soko , sio kko. Je litapata Acceptability? Kuna masoko mengi yamejengwa na watu wakahofia KKO ita slow don …. Haijawahi kuwa hivo

Hofu ni hilo soko…. Watu wanaweza kuchukua ma frame halaf wakawa wanasinzia tu humo ndani

Pia prices zao I bet zitakuwa ni changamoto…… frame zinauzwa bei juu:… usitegemee prices zitakuwa kama za machimbo ya KKO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…