Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Kariakoo au Dar ni wapi tutapata pochi, vitenge na viatu vya kike bei za jumla? Maana wenyeji wengi hawapendi kutupeleka kwenye machimbo

CC: charty.



 
Ngoja nikupe machimbo best. Kizuri kula na mwenzio. Vitenge mara nyingi machimbo yake yapo NIDA kule Mnazi Mmoja wengi wanaouza Kariakoo wanaenda kufuata huko. Viatu navyo vinapatikana huu Mtaa wa Narung'ombe na Congo pale nenda straight kwenye maduka ya Wachina yaani sio wale machinga wanaomwaga chini, nop. Unazama dukani utakuta zile simple wanauza 4000/pc na vile vi-sandles wanauza 2500/pc. Cheni zama Mchikichi katikati kuna Mchina anauza mpaka 2000-3000/dz na hazipauki. Magauni nayo ingia ndanindani kule Congo na Aggrey, wanauza nayo bei chee 6000-8000-1000-16000/pc. Vingine siku ingine nitakwambia nimechoka ku-type ah!
 
Tafta hela uende China. Kuna masoko yao kule vitu bei cheap kweli. Kuna vijana walianza kidgokidgo tu this day wanafanya vizuri kweli. Just know ur niche.

Vitu vingine in China the prices are lower kuliko hata hapo Kariakoo.
 
God bless you
 
Mi kuna machinga nilikuwa nachukua mzigo kwake,hivyo nampa pesa ye anazunguka kwenda kuchukua mzigo.Ukimuuliza asemi, siku nilienda na vijana wangu watatu ambapo yeye hakuwaona. Hivyo nilivyomkabidhi pesa akaondoka, vijana wangu wakamfuatilia mpaka wakajua maduka yote aliyoingia. Tangia siku hiyo hajaniona na majamaa wa madukani washanizoea hata bila pesa wananipa mzigo au wanatuma mkoani.
 
God bless you.
 
Inabidi nikutafute
 
Naona umeamua kumwaga UPUPU wote, maana yake kila mmoja aelekee straight kwa Mchina (muuzaji)...!!

Unataka/unategemea sisi Madalali tukale wapi..! anyway, najua tumefanya makosa sisi wenyewe kukupeleka kwenye Machimbo...

Naahidi atutarudia tena kufanya Makosa..!![emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Kariakoo, au Dar ni wapo tutapata pochi, vitenge na viatu vya kike bei za jumla? Mana wenyeji wengi hawapendi kutupeleka kwenye machimbo
Kariakoo ndio kila kitu kaka, karibu sana na ukishanunua mzigo nakusafirishia hadi Getini kwako.
 
Hahhahah sasa wewe mie mkali wa hizi kazi tokea nipo chuo kitamboo nimeivuruga sana hiyo Kariakoo hahah hadi leo nipo yaani na sibanduki ng'ooo inabidi tuwasaidie wenzetu bana maana haya maisha mtu akikuongezea jero kwenye product ni kubwa sanaaaa.Na hivi vyuma vimekaza acha tu na wenyewe wale. Ila si unajua mjini wasioujua bado wengi utawapata tu maana hawapo humu JF.

Kariakoo, au dar ni wapo tutapata pochi,vitenge na viatu vya kike bei za jumla? Mana wenyeji wengi hawapendi kutupeleka kwenye machimbo
Ngoja niwape chimbo la pochi za bei rahisi zile ronya na za kati 6000, 8000, 12000 lipo maeneo ya Nyamwezi karibu na soko la shimoni kale kamtaa cha kati uje utokee Msimbazi Kota, karibu wanapouza maturubali, lingine lipo mtaa wa Congo na Aggrey kwa juu ghorofani kama unataka kutoka Aongo kituo cha basi pale wanauza high quality PU zao 22k, 25k, 28k, 30 nk ambazo ukikuta kwenye botique ni mwendo wa 50k,70k hadi 100k. Pia tena hiyohiyo congo/mchikichi pale katikati kwa ghorofani wanauza pochi eh bei chee tatizo lenu mnapita juu juu tu ingieni maduka ya ndani na chini yana mambo mazuri Wallet nazo Mchikichi zipo za kumwaga za kiume na za kike bei chee hakikisha unaingia ndani kabisa kwenye vichochoro. Haya kwa wale wa mabegi ya kusafiria kuna mchina anazalisha mwenyewe maeneo ya Veta karibu na sofia house kule anakutengeneezea design unayotaka eh, pesa yako tu. Kuna kingine nimesahau? Danhappy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…